UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI
Fasihi andishi ni tawi la fasihi linalotumia sanaa ya maneno kufikisha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya maandishi. Zipo aina nyingi za fasihi andishi, miongoni mwa hizo ni pamoja na hadithi fupi, riwaya, tamthiliya na mashairi.
Dhana ya Uhakiki
Fafanua dhana ya uhakiki
Uhakiki ni kitendo cha kutathimini, kueleza, kuainisha na kutoa maoni juu ya kazi fulani ya fasihi kwa kuongozwa na kaida maalum. Hii ina maana kwamba uhakiki wa kazi za fasihi hautoki katika ombwe, kuna kanuni na taratibu mbalimbali zinazoongoza kufanya uhakiki, na hii ndio sababu kuna nadharia kadha wa kadha za uhakiki wa kazi za kifaishi. AU kwa lugha rahisi tunaweza kusema, uhakiki ni uchambuzi wa kina wa kazi za fasihi kama vile riwaya, tamthiliya na mashairi kwa lengo la kufafanua vipengele vya fani na maudhui.
Misingi ya Uhakiki
Elezea misingi ya uhakiki
Kwa ujumla mhakiki wa kazi za fasihi anapofanya uhakiki wa kazi za kifasihi, huwa analenga vipengele viwili. Pengine analenga kuhakikifaniya kazi husika aumaudhuiya kazi hiyo na wakati mwingine vyote viwili. Kwa hiyo kupitia vipengele hivi ndipo atachambua vitu vingi kama vile ujumbe, falsafa, matumizi ya lugha, dhamira, mandhari na kadhalika.
Kuhakiki Fani
Katika utunzi wa kazi za kifasihi, Fani hutumika kama nyezo ya kuwasilisha mawazo ya mwandishi kwa njia ya kisanaa zaidi. Fani ni mbinu anayoitumia mwandshi ili kufikisha ujumbe kwa watu aliowakusudia.
Vipengele vya fani ni pamoja nawahusika, mandhari, lugha, muundonamtindo.
Mtindo
Mtindo ni mbinu ya kipekee kifani na kimaudhui, zinazotofautisha msanii mmoja na mwingine. Kwa mfano, namna msanii anavyotumia lugha, anavyoteua msamiati, namna anavyosimulia hadithi yake (anaweza kutumia nafsi ya kwanza, ya pili au ya tatu). Kwa mfano katika riwaya ya “Barua Ndefu kama hii” iliyoandikwa na Mariama Ba ametumia mtindo wa barua ya kirafiki kuanzia mwanzo hadi mwisho, hii pia inaonesha mtindo wake wa kipekee.
Muundo
Muundo ni mpangilio wa kiufundi anaoutumia mwandishi katika kupangilia kazi yake. mpangilio na mtiririko wa kazi ya fasihi, kwa upande wa visa na mtukio.
Kuna aina mbili za kupangilia matukio
  1. Msago; hii ni namana ya moja kwa moja ya kusimulia matukio, yaani kuanzia tukio la kwanza hadi la mwisho kwa namna yalivyotukia. Huu ni muundo wa moja kwa moja.
  2. Urejeshi; huu ni usimuliaji wa kurukaruka hatua, yaani msimuliaji anaweza kuanzia katikati, akaja mwisho na kumalizia na mwanzo
Wahusika
Wahusika; ni watu au viumbe ambavyo mwandishi wa fasihi huwatumia ili kufanikisha ujumbe kwa jamii husika. Katika kazi ya fasihi mwandishi huwagawa wahusika katika makundi mawili yaani wahusika wakuu na wahusika wadogo.
Wahusika wakuu ni wale ambao wanajitokeza kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa kazi ya fasihi. Wahusika wadogo ni wale wote ambao wanajitokeza sehemu mbalimbali katika kazi ya fasihi kwa mfano, mwanzoni mwa kitabu hadi mwishoni mwa kitabu.
Wahusika hawa wawe ni wakuu au wadogo wanaweza kugawanyika katika makundi yafuatayo:
  1. Mhusika mviringo ni mhusika ambaye anabadilika kitabia na kimawazo kulingana na hali halisi ya maisha. Kwa mfano wanaweza kuanza kama watu wema lakini hali ya maisha ikawabadilisha na kuwa watu wabaya au wanaweza kuanza kama watu wabaya na hali ya maisha ikawabadilisha na kuwa watu wema.
  2. Mhusika bapa ni mhusika ambaye habadiliki kulingana na hali halisi ya maisha. Mfano; kama ni mwema basi atakuwa mwema kuanzia mwanzo wa hadithi hadi mwisho na kama ni mbaya basi atakuwa mbaya kuanzia mwanzo wa hadithi hadi mwisho.
  3. Mhusika shinda yuko katikikati ya mhusika papa na mviringo. Huongozwa na matendo ya hao wahusika wawili. Hajitokezi na msimamo wake imara.
Mandhari
Mandhari; hii ni sehemu ambayo matukio ya hadithi au masimulizi hutokea. Mandhari huweza kuwa halisi kama vile baharini, njiani, msituni, kijijini, mijini au ya kufikirika kama vile kuzimu, mbinguni, peponi n.k.
Lugha
Lugha ndio nyenzo kubwa ya msanii katika kazi za fasihi, miongoni mwa vipengele vya lugha ni tamathali za semi pamoja na semi.
Fani za Lugha
  • Tanakali za Sauti:Ni mbinu ya kutumia maneno yanayoiga sauti au hali fulani au namna kitendo kilivyofanyika.
  • Tashbiha: Hii ni mbinu ya lugha inayolinganisha vitu au hali mbili tofauti kwa kutumia maneno ya kulinganisha; ‘kama’, ‘mithili ya’, ‘sawa na’, ‘ja’. mfano, Mwembamba kama sindano.
  • Tashihisi: Hii ni mbinu ya kupatia kitu kisicho hai sifa za kiumbe mwenye uhai (sifa za kibinadamu). Mfano, "Sungura aliposhindwa, akasema sizitaki hizi mbichi".
  • Takriri: Ni mbinu ya kurudiarudia neno moja au kifungu cha maneno ili kusisitiza ujumbe fulani. Mfano, alikimbia, alikimbia, alikimbia hadi akashika nafasi ya kwanza.
  • Ukinzani: Ukinzani ni mbinu ya kusisitiza ujumbe kwa kuambatanisha maneno ya kinyume au yanayokinzana.
  • Sitiari: Ni mbinu ya kulinganisha vitu viwili moja kwa moja kwa kutumia kiungo ‘ni’ ama ‘kuwa’. Mfano; Maisha ni mlima, juma ni mwamba.
  • Taswira: Ni matumizi ya lugha/maneno yanayojenga picha ya hali au jambo fulani kwa msomaji.
  • Taashira: Ni matumizi ya lugha ya ishara kuwakilisha ujumbe fulani. Jina au kitu fulani kinatumika kumaanisha kitu kingine chenye uhusiano na kile kilichotumiwa.
  • Jazanda: Ni kulinganisha vitu viwili moja kwa moja bila kutumia viunganishi.
  • Majazi: Majazi ni pale tabia za wahusika zinapoambatana na majina yao halisi.
  • Lakabu: Ni mbinu ya mhusika kupewa/kubandikwa jina na wahusika wengine ama yeye mwenyewe kujibandika jina linalooana na tabia/sifa zake.
  • Chuku: Ni kutumia maneno yaliyotiliwa chumvi ili kusisitiza ujumbe fulani au kusifia kitu, kutilia Chumvi.
Semi
Ni fungu la maneno linapotumika kutoa maana nyingine, badala ya ile ya maneno yaliyotumika. Semi hutumika kuficha ukali wa maneno au kupamba lugha. Kuna aina mbili za semi:
  • Nahau – ni usemi unaotumia maneno ya kawaida kwa lengo la kufikisha maana iliyotofauti na maana ya kawaida ya maneno hayo. Nahau huwa na vitenzi.
  • Misemo – ni semi fupifupi ambazo hutumiwa mara kwa mara kwa lengo la kuleta maana maalumu. Misemo haina vitenzi.
  • Maswali ya Balagha: Tashititi au maswali ya balagha ni maswali yanayoulizwa na msimulizi au mhusika ambayo hayahitaji jibu.
  • Uzungumzi Nafsiya: Mhusika hujizungumzia, ama kwa kuongea au kuwaza, bila kukusudia kusikika na yeyote.
  • Ritifaa: Mbinu ya kuzungumza na mtu aliyekufa (au asiyekuwepo) kana kwamba yuko pamoja nawe.
  • Kuchanganya Ndimi: Kuweka maneno yasiyo ya Kiswahili katika sentensi ya Kiswahili. Mfano, "alisimama kwanza kwa muda, before he went aliniambia nisimwambie mtu yeyote yule, you know!"
  • Kuhamisha Ndimi: Ni kuingiza sentensi ya lugha nyingine katika kifungu cha lugha ya Kiswahili. Kinyume na Kuchanganya ndimi (ambapo mwandishi huchanganya maneno katika sentensi moja, katika kuhamisha ndimi, sentensi kamilifu ya lugha nyingine hutumika miongoni mwa sentensi za Kiswahili sanifu. Mfano: Kazi hii ni ngumu sana, sitaweza kuifanya. People are trying to convince me to stay here but I think I can't, I must go!
  • Mathali: Methali ni misemo ya hekima yenye maana iliyofumbwa. Mhusika, mwandishi wa fasihi anaweza kutumia methali kupitisha ujumbe.
Mbinu nyingine za Kisanaa
  • Kinaya: Kinaya ni mambo katika sanaa kuwa kinyume na matarajio ya hadhira.
  • Kejeli; Kejeli ni mbinu ya sanaa inayotumia maneno kudharau au kukemea kitendo au mtu fulani.
  • Taharuki; Taharuki ni mbinu ya kusimulia au kuandika riwaya/hadithi kwa kufanya hadhira na/au wahusika wajawe na hamu ya kutaka kujua kitakachotokea baadaye; hamu ya kutaka kuendelea kusoma/kusikiliza. Baadhi ya hadithi huishia kwa taharuki na kuilazimisha hadhira yake ijikamilishie au ibaki ikijiuliza maswali.
  • Sadfa; Sadfa ni kugongana kwa vitendo viwili vinavyohusiana kana kwamba vilikuwa vimepangwa, japo havikuwa vimepangiwa.
  • Kisengere Nyuma; Mwandishi ‘hurudi nyuma’ na kuanza kusimulia kisa kilichokuwa kimetendeka kabla ya alichokuwa akisimulia. Aidha, mwandishi hubadilisha wakati wa masimulizi na kuwa wakati wa kisa hicho. Hutumika sana kuonyesha mhusika anapokumbuka kitu, au kutupatia msingi wa jinsi mambo yalivyoanza.
  • Kisengere Mbele; Mwandishi anapobadilisha wakati na kusimulia mambo yatakavyokuwa siku za usoni; au kutumia lugha isiyo moja kwa moja kutabiri yatakayojiri. Utabiri.
Kuhakiki Maudhui
Maudhui; Maudhui katika kazi ya fasihi ni jumla ya mawazo yote yanayozungumzwa pamoja na mtazamo wa mwandishi juu ya mawazo hayo. Maudhui hujumuisha mawazo pamoja na mafunzo mbalimbali yaliyomsukuma msanii hadi akatunga na kusanii kazi fulani ya kifasihi. Vipengele vya maudhui ni pamoja na dhamira, migogoro, falsafa ujumbe na msimamo.
  1. Dhamira; hili ni wazo kuu au mawazo mbalimbali yanayojitokeza katika kazi ya fasihi. Dhamira ni sehemu tu ya maudhui na aghalabu dhamira kuu ndio hujenga kiini cha kazi ya fasihi. Dhamira zimegawanyika katika makundi mawili, kuna dhamira kuu na dhamira ndogondogo.
  2. Migogoro; hii ni mivutano na misuguano mbalimbali katika kazi za fasihi. Migogoro inaweza kuwa kati ya wahusika, familia zao, matabaka yao, au hata katika nyadhifa mbalimbali. Vilevile migogoro yaweza kuwa ya kiuchumi, kijamii, mogogoro ya nafsi, na migogoro ya kisiasa ambayo hujitokeza katika mitazamo tofauti kulingana na mtiririko wa visa na matukio yanavyopangwa na mwandishi.
  3. Ujumbe; mwandishi anapoandika kazi yake huwa na ujumbe ambao hutaka uifikie jamii aliyoikusudia. Ujumbe katika kazi fasihi ni mafunzo mbalimbali ambayo hupatikana baada ya kusoma kazi ya fasihi. Katika kazi ya fasihi dhamira kuu hubeba ujumbe wa msingi na dhamira ndogondogo hubeba ujumbe ambao husaidia kuujenga au kuupa uzito zaidi ujumbe wa msingi.
  4. Msimamo; katika kazi ya fasihi, mawazo, mafunzo na falsafa ya msanii hubainisha msimamo wake kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii. Msimamo ni ile hali ya mwandishi kuamua kufuata na kushikilia jambo fulani. Jambo hili huweza kukataliwa na wengi lakini akalishikilia tu. Msimamo ndio huweza kuwatofautisha wasanii wawili au zaidi wanaoandika kuhusu mazingira yanayofanana. Kwa mfano, katika tamthilia ya “Pesa zako zinanuka” mwandishi anamsimamo wa kimapinduzi kwani amejadili matatizo yanayochangia kukwama kwa ujenzi wa jamii mpya.
  5. Falsafa ni mawazo ya busara yenye kutawaliwa na misingi mahususi juu ya asili na maana ya ulimwengu na maisha ya mwanadamu. Ni msimamo wa msanii katika maisha juu ya utatuzi wa matatizo katika jamii. Falsafa ya mwandishi inaweza kujulikana kwa kusoma kazi zake zaidi ya moja.
  6. Mtazamo ni hisia au uelewa wa mwandishi juu ya jambo fulani. Kwa mfano anaweza kutazama jambo fulani kwa mtazamo wa kidini, au anaweza kutazama jambo fulani kwa mtazamo wa kisiasa au kisayansi.
  7. Mafunzo; ni mawazo ya kuelimisha yanayopatikana katika dhamira mbalimbali za kazi ya fasihi.
Kufaulu na Kutofaulu kwa mwandishi
Kufaulu au kutofaulu kwa mwandishi kunategemea jinsi alivyoweka uwiano mzuri kati ya fani na maudhui kwa namna ambavyo inaleta uhalisia. Mfano, endapo msanii atakuwa na mhusika Mkongo lakini akawa anazungumza kiswahili kilichojaa misemo na nahau alafu kimenyooka kama mtu wa pwani itakuwa vigumu kusema amefaulu kwani hakuna uwiano mzuri kati ya mhusika mwenyewe na lugha anayoitumia. Kiswahili cha Kongo ni tofauti kabisa na kiswahili kinachozungumzwa na watu wa pwani (Tanzania).


Uhakiki wa Fani katika riwaya ya Takadini
Hakiki fani katika riwaya ya Takadini
MWANDISHI: BEN J. HANSON
WACHAPISHAJI: MATHEWS BOOKSTORE AND STATIONARIES
MWAKA: 2004
JINA LA KITABU
Jina la kitabu TAKADINI lina maana ya “Sisi tumefanya nini”. Hili ni jina ambalo Sekai alimpa mwanae mara baada ya kumzaa. Jina hili lilitokana na majonzi aliyokuwa nayo juu ya kutaka kuuawa kwa mwanae na yeye ilihali hawakuwa na hatia, ila tu kwa sababu ya mila za jamii yake zilivyotaka. Jina hili la kitabu ni sadifu kwani linasawiri vyema maudhui yaliyomo katika kitabu hiki. “Sisi tumefanya nini?’ ni swali ambalo linatokana na ukosefu wa haki ya kuishi, kubaguliwa kutopendwa, na hata kutengwa kwa watu wenye matatizo katika jamii. Swali hili linawalelekea wanajamii ambao bado wanashikilia mila potofu zinazowakandamiza na kuwanyanyasa watu wenye matatizo mfano, ulemavu wa ngozi, wagonjwa nk. Jina hili pia ni sadifu kwa maisha ya jamii yetu ya watanzania kwani watu bado wanashikilia mila potofu ambazo si nzuri. Mwandishi ametumia jina hili makusudi ili kutaka kuionesha jamii hali halisi ya vilio vya albino, wasichana wadogo wanaolazimishwa kuolewa nk. Kuwa huu sasa ni muda mwafaka wa jamii kuyaacha na kutupilia mbali mambo hayo.
MUUNDO
Muundo alioutumia mwandishi wa riwaya hii ni muundo wa msago au kwa jina lingine muundo wa moja kwa moja. Ameyapanga matukio katika mtiririko sahili kwani ameanza kutuonesha toka mwanzo mpaka mwisho wa maisha ya kijana Takadini “Msope”.Toka kutungwa kwa mimba yake, kuzaliwa kwake na kuishi kwake, matatizo na changamoto zinazomkumba na jinsi anavyokabiliana nazo na hatma ya maisha yake.
Mgawanyo wa visa na mtukio umepangwa katika sura ambapo visa vimejengwa kwa ufundi na kuvifanya vijengane na kukamilishana kuelekea kilele cha masimulizi. Matukio haya yamewekwa katika sura kumi na tatu.
  • Sura ya Kwanza:Sura hii inaanza kutuelezea kuhusu mwanamke Sekai anavotunga mimba, pia tunaelezwa kuhusu mtazamo mbaya wa wake wenzie juu ya mimba hiyo baada ya Sekai kukaa kwa muda mrefu bila ya kujaliwa mtoto.
  • Sura ya Pili:Hapa tunasimuliwa jinsi Sekai anavyofanikiwa kujifungua salama. Lakini kwa bahati mbaya kwa kawaida ya jamii yao anajifungua mtoto Zeruzeru ambaye kwa mila zao mtoto huyo ni laana. Hivyo alipaswa kutupwa mara moja ama kuuawa. Hakuna ambaye alikuwa tayari kumpokea mtoto yule kwani si baba yake wala jamii yake ila mama yake pekee.
  • Sura ya Tatu:Jamii bado haipo tayari kumpokea mtoto Sope, wanawake wenza wa Sekai wanasubiri kwa hamu kuona tukio la kutupwa kwa Takadini litakavokuwa, kwani ndio jinsi mila na taratibu za mababu zilivyotaka. Kutokana na hali hii ndipo Sekai anapata wazo la kutoroka. Anaamua kuondoka kwenda mbali ili kukinusuru kichanga kisicho na hatia kwani alisubiri kwa hamu na uchu wa muda mrefu kupata mtoto.
  • Sura ya Nne:Sekai anafanikiwa kutoroka na mwanae Takadini ili kumuepusha na kifo, jamii na Mtemi wanapata habari ya kutoroka kwake. Upelelezi unafanyika lakini juhudi hazikuzaa matunda kumpata Sekai na mwanae mchanga waliotakiwa kuuawa. Sekai anasafiri mbali na kufikia kijiji kingine na kupokelewa na mzee Chivero.
  • Sura ya Tano:Sekai anapokelewa katika kijiji cha mzee Chivero, jamii na wazee wanashitushwa sana na ujio huo lakini wanalazimika kumpokea tu baada ya malumbano ya muda mrefu. Kwani mila ziliwataka kutowatelekeza wageni katika kijiji chao, na hiyo ndiyo inakuwa mwanzo wa matumaini ya Sekai kuhusu kuishi kwa mwanae ambaye alionekana kuwa ni laana ya mababu na hakupaswa kuishi.
  • Sura ya sita:Baada ya Sekai kupokelewa katika kijiji cha mtemi Masasa, habari za ujio wake zinaenea kwa wanakijiji wote na wanaonekana kushtushwa sana, si hivo tu bali pia wanajiapiza katu kutomsogelea Sope kwani waliamini amelaaniwa. Lakini kwa juhudi za mzee Chivero baba mpya mlezi wa Takadini Sekai anapata rafiki. Tendai mke wa mtemi Masasa. Anajengewa kibanda cha kuishi yeye na mwanae na maisha yanaanza.
  • Sura ya saba:Sekai anaanza kujishughulisha na shughuli za kawaida kama mama na mwanamke, analima bustani na kufanya kazi ndogo za nyumbani. Siku moja katika safari ya kurudi nyumbani kwa bahati mbaya wanavamiwa na nyuki na kujeruhiwa vibaya yeye na mwanae, anaamua kumtupia mwanae kichakani ili kumuokoa na yeye kujitumbukiza mtoni. Wote wawili wanafanikiwa kutibiwa na kupona majeraha.
  • Sura ya nane:Taratibu Takadini anaanza kukua lakini anagundulika kuwa hawezi kutembea vyema kwa mguu mmoja, hii ilitokana na kuvunjika Mguu baada ya kurushwa kichakani na mamaye kama juhudi za kumwokoa. Hali hii inamhuzunisha zaidi Sekai na Chivero kwani walimpenda sana. Hapa ndipo mapenzi ya Chivero yalianza kudhihirika rasmi kwa Takadini kwani alijenga urafiki naye na kumpenda kama mwanae. Alimfundisha utabibu wa dawa za kienyeji na mambo mengine mengi. Pia tunaona watoto jinsi walivyombagua Takadini kutokana na hali yake, kwani waliambiwa na wazazi wao wasicheze naye amelaaniwa hivo hawakuthubutu.
  • Sura ya tisa:Katika sura hii, Mzee Masasi anafariki dunia na kumuacha mzee Chivero katika majonzi makuu. Hali ya mzee Chivero nayo inaanza kuzorota kwa uzee. Anampa Takadini usia mbalimbali na kumfunza. Pia tunaelezwa juu ya fikra mpya za Takadini za kupiga “mbira” kifaa cha muziki cha kijadi, hii baada ya kuvutiwa na sanaa hiyo aliposhiriki sherehe za mavuno za mwaka. Jamii bado ilimtenga Takadini na kumbagua, walimwona si binadamu bali mzuka tu! Na kwa bahati mbaya mzee Chivero naye aliaga dunia na kuacha simanzi kuu kwa Sekai na Takadini mbao alikuwa ni tegemeo na faraja kwao.
  • Sura ya kumi:Baada ya kifo cha mzee Chivero, Takadini anapata mwalimu maarufu mpiga mbira mzee Kutukwa, anamfundisha kupiga mbira, Takadini anaonesha juhudi kuu na kufanikiwa. Pia anmsaidia kifaa cha kumsaidia kutembea kutokana na mguu wake mbovu, hii inakuwa ni faraja kubwa kwa Takadini na mamaye.
  • Sura ya kumi na moja:Hapa tunaelezwa juu ya kijana Nhamo adui mkuu wa Takadini kwani hakumpenda na alimdhihaki na kumdhalilisha mara kwa mara. Kijana huyu anaonekana kuwa ni shujaa katika jamii yake kwa kitendo cha kumuua simba mla mifugo. Hiyo inamletea sifa kubwa na majivuno mengi hivo wasichana wengi kumtamani awaoe, hali ni tofauti kwa Shingai ambaye anaonesha hisia za mapenzi kwa Takadini pamoja na hali yake ya “Usope”. Chemchemi za mapenzi ya Takadini kwa Sekai zinaanza kumea jambo ambalo linamkera sana Nhamo na kuzidisha chuki kwa Takadini kwani pia alitamani kuwa na Shengai binti mrembo. Jamii inafanya kikao kujadili suala la Shengai kumpenda Takadini na wanalipinga vikali suala hilo.
  • Sura ya kumi na mbili:Nhamo anakata shauri na kwenda kumposa Shengai, wazazi wa pande zote mbili wanaliunga suala hilo mkono asilimia zote. Kwani hilo lingewanusuru aibu ya mwanao kuolewa na Sope, kwani walijua fika Shingai alimpenda Takadini na hakumtaka Nhoma. Nhoma anamuonya vikali Takadini kuwa asiendelee na lolote kwa Shengai. Pia hapa zinafanyika sherehe ya kijadi ya kumkaribisha hayati mzee Chivero tena nyumbani.
  • Sura ya kumi na Tatu:Wakati wa sherehe ya mavuno, binti Shengai anashindwa kuvumilia na kuamua kumfuata Takadini kibandani kwake. Anaamua kuvunja mila za kwao kwani alimpenda kwa dhati Takadini, pamoja na dharau, kejeli, kubaguliwa, ulemavu wake na kuonekana kuwa ni mtu aliyelaaniwa. Wazazi wake wanamtenga na kutomtambua kama ni mtoto wao tena. Suala hilo linatikisa jamii ya watu wa kijiji kile na hata kutaka kuwafukuza Sekai na mwanae lakini wanaokolewa na maamuzi ya busara ya wazee kwa kuwacha Shengai na mpenziwe Takadini waishi hali wakisubiri matokeo! Kuwa je mtoto atazaliwa sope? Na kuongeza ukoo wa masope na kijiji chao kuwa cha masope? Hapa ndio inapojulikana hatma ya Takadini na mkewe kwani anapata ujauzito na kufanikiwa kujifungua mtoto salama asiye Sope. Ilikuwa furaha kuu kwa mama na mtoto na wote pia. Wanaamua kurudi kijijini kwao walikotoroka ili kwenda kuwadhihirishia kuwa hata sope anaweza kuishi hapaswi kubaguliwa na kutengwa
MTINDO
Mwandishi ametumia mitindo kadha wa kadha ili kuipamba kazi yake na kuifanya ivutie wasomaji; mfano matumizi ya nafsi mbalimbali, matumizi ya nyimbo nk.
Matumizi ya nafsi
Kwa kiasi kikubwa yametawala matumizi ya nafsi ya tatu umoja na wingi katika sura zote.Mfano.uk. 30. “ aliingia ndani na kuanza kazi.”Piauk.3 “ Sekai alikoka moto nje ya kibanda, akaketi na kuzungumza na Pindai”.
Matumizi ya nafsi ya pili au dayalojia
Mfano uk 29 - 30. Mazungumzo kati ya Chivero na Sekai:“je umelala salama?je umelala salama?Sijambo mwanangu, sijui wewe?Sijambo Sekuru,Na mwanao je?Naye hajambo.”
Matumizi ya nafsi ya kwanza. Mfano uk. 82 na 83
“lakini ghafla nilipata nguvu mpya”;“nilikuwa na nguvu kama kijana….”
Pia mwandishi ametumia nyimbo katika baadhi ya sura ili kuwaburudisha na kuliwaza wasomaji. Mfano uk. 2 wimbo aliouimba mke mwenza wa Sekai Rumbdzai.
“Mashamba yetu yamelimwa mbegu nazo zimepandwa zimechipua na kumea, sisi watatu tumepanda mavuno yetu; mheshimiwa wetu amemiliki mavuno kwa mikono yake halisi kutoka mashamba yetu yote lakini ni kipi alichoambulia kutoka ardhi ile isiyomea kitu?”pia ametumia wimbo uk. 34, 57, 85.
Matumizi ya hadithi ndani ya hadithi pia ni mtindo mwingine wa usimulizi alioutumia mwandishi.Mfanouk82Kutukwa alisimulia vijana hadithi enzi ya ujana wake na jinsi alivopambana na maadui vitani.
Matumizi ya Lugha
Lugha aliyotumia mwandishi ni lugha fasaha na rahisi inayoeleweka kwa wasomaji wake. Ametumia pia lugha nyinginezo kama vile lugha za kikabila.Maneno kama vile“Amai”,lenye maana yamama, “Sope”lenye maana yazeruzeru, “shumba”- simba, “mbira” – chombo cha asili cha muziki, “gudza” – blanketi lililotengenezwa kwa nyuzi za magome ya miti.nk.Hivyo mwandishi ametumia lugha hii ili kuwaleta wasomaji kwenye mazingira halisi ya kiutamaduni ya jamii ile.
Matumizi ya tamathali za Semi
  • Tashibiha:Mfanouk. 6 “ muda huenda polepole mithili ya mwendo wa kakakuona Uk.15 “ habari njema huchechemea kwa mguu mmoja lakina mbaya hukimbia kama Sungura”Uk.16 “….. alibaki kama kinyago cha mpingo”.Uk.28 “ sio kufurika kama Chura”Uk.33 “aligeuza shingo yake sawa na Mbuni”Uk.42 “ nywele kama vinyweleo vya mahindi yaliyokaribia kukomaa”Uk.82 “muziki ulikuwa kama chemchemi ya maji mwilini mwake”
  • Tashihisi:Mfanouk. 5 “ndege mbalimbali wakiimba kuikaribisha siku mpya”Uk. 7 “vivuli vya jioni viliongezeka urefu”Uk. 18 “maneno yananila mifupa yangu”Uk 25 “kifo kilinukia”
  • Tafsida:Mfano, uk. 83 “sehemu zake za siri”
  • Sitiari:Mfano, uk. 88 “Tapfumaneyialigeukambogo” Uk.97“mwana Mbwa hakuiba mfupa”, Tawanda mfupa ulikwenda wenyewe kuchezanaye.” Hapa mfupa umefananishwa na Shingai na Takadini ndio mwanambwa
Matumizi ya Semi
  • Methali:Uk. 45 “ kipofu huwa hachagui shimo la kutegea wanyama”uk.33 “ moyo mwema utakufanya uuwawe”
  • Misemo:Mfano.Uk. 12 “kufikiri katika siri ni sawa na safari ya mbwa”Uk. 100 “kanga hawezi kutua juu ya bua la mtama”Uk.101 “kibuyu kikubwa hakikosi mbegu ndani”Uk. 125 “fuvu la nyanilimekuwa kijiko kwa mlo wa mahindi”
  • Nahau:uk. 27 “ penzi langu kwake halikufua dafu”Uk. 88 “kutiana moyo wa ari”
Matumizi ya mbinu nyinginezo za kisanaa
  • Nidaa:Mfano,Uk.4 “Ha!” , “Ha! Atimuliwe tena? Mchawi?” Uk.16 “Mai, Wee!” Uk.39. “Ha! Iwe! Ha!”
  • Mdokezo:MfanoUk.3 “ndiyo Pindai, ninaogopa……….” Uk.42 “mtu mzima kama watu wenine ameamua………”
  • Takriri:Mfano,uk 57 “ mwanangu, mwanangu, mwanangu, wamekufanya nini?”
Wahusika
Sekai
  • Ni mke wa Makwati wa kwanza.
  • Ni mwanamke jasiri.
  • Anapinga mila potofu na mbaya za jamii yake.
  • Ni mvumilivu.
  • Ni mchapakazi mzuri.
  • Anajifungua mtoto zeruzeru ambaye ni laana kwa jamii yake.
  • Ni mtiifu na mwenye adabu.
  • Ana huruma na mnyenyekevu.
  • Ana mapenzi ya dhati.
  • Anafaaa kuigwa na jamii.
Takadini
  • Ni mtoto anayezaliwa na ulemavu wa ngozi( albino)
  • Anasadikika kuwa ni laana kwa jamii yake hivyo kupaswa kuuawa au kutupwa mbali.
  • Anaokolewa na mama yake kwa kutoroshewa katika kijiji kingine.
  • Anapokua anakua kijana jasiri.
  • Hapendwi na jamii.
  • Anabaguliwa na jamii, hana rafiki.
  • Ni mvumilivu na msikivu mwenye heshima.
  • Alimpenda Chivero sana.
  • Alikuwa mpiga mbira (chombo cha muziki cha kijadi) maarufu.
  • Alimuoa Shingai na kupata mtoto asiye Sope.
Makwati
  • Mume wa Sekai.
  • Ameoa ndoa ya mitara ana wake wanne.
  • Anashikilia mila na desturi potofu.
  • Hana mapenzi ya dhati kwa mwanae.
  • Hafai kuigwa na jamii.
Dadirai na Rumbidzai
  • Wake wengine wa mzee Makwati.
  • Wana wivu.
  • Hawampendi Sekai.
  • Wana roho mbaya kwani wanamwombea Sekai mabaya.
  • Ni katili kwani wanashinikiza Sekai na mwanae wauawe bila huruma.
  • Wasengenyaji.
  • Hawafai kuigwa na jamiii.
Pindai
  • Mke wa pili wa Makwati.
  • Ana upendo wa dhati kwa Sekai.
  • Ni mkweli.
  • Hana wivu.
  • Ni mshauri mzuri.
  • Anafaa kuigwa na jamii.
Chivero
  • Ni mzee wa kijiji cha mzee Masasa.
  • Anawapokea Sekai na mwanae baada ya kutoroka kwao kwa ukarimu mkubwa.
  • Ni mwenye roho nzuri.
  • Ana huruma sana.
  • Ni mganga wa tiba za asili.
  • Ana mapenzi ya dhati kwa Takadini na Sekai.
  • Anamrithisha Takadini uganga.
  • Ana busara na hekima.
  • Ni mshauri mkuu wa Mtemi Masasa.
  • Anafaa kuigwa na jamii.
Mtemi Masasa
  • Ana busara na hekima.
  • Ana huruma.
  • Anafuata mila na desturi ya jamii yake.
  • Ni msikivu.
  • Ni rafiki mkubwa wa Chivero.
  • Ni kiongozi bora.
Nhamo
  • Ni kijana katika kijiji cha mtemi Masasa.
  • Ana majivuno na jeuri.
  • Hampendi Takadini kwani alimbagua kumpiga na hata kumdhalilisha.
  • Hafai kuigwa n ajamii.
Tendai
  • Mke mdogo wa mwisho wa mtemi Masasa.
  • Aliolewa bila kupenda, hakumpenda mtemi Masasa kwani alimzidi umri.
  • Alikuwa rafiki mzuri wa Sekai.
  • Ana mapenzi ya dhati kwa Takadini.
  • Ana bidii na mvumilivu.
Nhariswa na mkewe
  • Ni wazazi wa Shingai
  • Wanashikilia mila desturi potofu
  • Hawakupenda kabisa kitendo cha mtoto wao kumpenda Takadini
  • Walimlazimisha kuolewa na Nhamo kwani walitaka sifa na maujiko
  • Walimtenga Shingai baada ya kutoroka na kuolewa na Takadini
  • Si wazazi wazuri
  • Hawafai kuigwa na jamii
Kutukwa
  • Ni mzee katika kijiji cha mtemi Masasa
  • Ni mpigaji mbira maarufu
  • Alimfundisha Takadini kupiga mbira
  • Alitoa mtazamo mbaya kwa wanakijiji wenzake kwa kuwaeleza sifa nzuri za Takadini
  • Alimpenda Takadini. Anafaa kuigwa na jamii
Mandhari
Mandhari aliyotumia Ben J Hanson ni mandhari ya kijijini kwani maisha ya watu na mazingira yanayoelezwa ni ya kijijini, masuala kama ya kilimo, ufugaji, sherehe za mavuno, makazi ya watu kukaa katika jumuiya ya pamoja kijamaa inayoongozwa na mtemi mmoja. Mfano mtemi Masasa, yote haya ni viashiria kuwa mandhari ni ya kijini. Mandahari ambayo mwandishi ameijengea mawazo yake na kuyaibua ni sadifu na halisi. Kwani maeneo ya vijijini ndiko kulikokithiri mambo ya imani potofu na za kishirikina kama vile kuwaua watoto Sope au albino.
Fani katika Riwaya ya Joka la Mdimu
Hakiki fani katika Riwaya ya Joka la Mdimu
MWANDISHI: ABDALLAH J. SAFARI
MCHAPISHAJI: HUDA PUBLISHERS
MWAKA: 2007
UTANGULIZI WA KITABU
Joka la mdimu ni riwaya iliyojengwa kwa visa tofautitofauti vinavojengana kukamilisha masimulizi. Ni riwaya inayosawiri au kuakisi mambo yaliyopita ya nyakati za nyuma ambapo kulikuwa na shida kama vile za mafuta ya petroli, Nguo, vyakula nk. Pamoja na hayo zipo pia dhamira au mawazo ambayo yanasawiri maisha ya Mtanzania wa leo kama vile masuala ya rushwa na uhujumu uchumi.
Kwa upande wa fani ni riwaya ambayo mwandishi amewaumba vyema wahusika wake kwa kuwavika uhalisia vyema, amepanga visa vyake na amejitahidi kutumia lugha yenye mvuto na vionjo vya kisanaa huku akiwaburudisha wasomaji kwa mtindo wa kipekee.
JINA LAKITABU
Jina la kitabu limewekwa katika lugha ya picha, JOKA LA MDIMU ni nyoka anayeishi katika miti ya kijani. Nyoka huyu hupendelea kuishi katika miti ya Minyaa na Midimu inayofanana na rangi yake. Nyoka huyu awapo kwenye miti hiyo si rahisi kumtambua kutokana na rangi yake kufanana sana na miti hiyo. Hivyo ni nyoka hatari sana kwa binadamu.
Mwandishi anatumia taswira ya Joka la Mdimu kufananisha na viongozi ambao ni wananchi wenzetu, wanafanana na sisi, ni ndugu zetu damu yetu. Lakini ni hatari mno kwani hutugeuka na kuwa mafisadi, wala rushwa, hawatimizi majukumu yao, ni walaghai nk. Badala ya kusaidia wananchi wao hujali maslahi yao kwanza na hivyo kusababisha mifumo ya kiuchumi kuendelea kuwa migumu kwa wananchi na kupelekea kuongezeka kwa kiasi kikubwa cha watu walio maskini au hohehahe. Hivyo jina la kitabu linasawiri yaliyomo ndani ya kitabu na katika jamii.
MUUNDO
Riwaya ya Joka la Mdimu imetumia muundo changamani yaani kwa kiasi fulani ametumia rejea au rukia pia ametumia muundo sahili au msago.
Mfano ametumia muundo warejeakatika sura ya Mindule ambapo anaanza kutueleza juu ya habari za Amani dereva wa taxi na adha anazopata kutokana na ukosefu wa mafuta na jinsi anavyoiendesha biashara yake hiyo. Lakini ndani ya sura hiyohiyo anaturudisha nyuma na kuanza kutuelezea namna Amani alivyopata kazi ya udereva Taxi na kutueleza juu ya mmiliki wa Taxi hiyo ambaye ni Shiraz Bhanj. Pia katika sura ya Boko anatueleza juu ya Safari ya Tino kwenda kumuona mwanae mgonjwa uk.73 ila hatuelezi inavyoendelea lakini anarukia kisa kingine cha Brown Kwacha na sura ya Kwale halafu badae anaturudisha nyuma na kuendelea kutuelezea juu ya habari za kuuguliwa kwa Cheche na Tino anapofika kumuona katika sura ya Dakta Makwati. Pia ametumia muundo wa moja kwa moja katika sura zingine kwani ameyapanga matukio yake katika usahili bila kuruka.
Pia mwandishi amegawanya visa na mtukio katika sura kumi ambapo kila sura ameipa jina kwa kutumia majina ya wahusika.
  • Sura ya kwanza, MINDULE:Hapa mwandishi anatueleza kuhusu habari za Amani dereva Taxi, masaibu anayopata katika kazi yake kutokana na uhaba wa mafuta katika vituo vya mafuta.
  • Sura ya pili, TINO:Hapa tunaelezwa kuhusu maisha ya Tino na kazi anazofanya ya kuvuta kwama. Tunaambiwa kuhusu hali ngumu ya maisha ya Tino na wakazi wengine wa Sega, hapa tunaelezwa pia kuhusu masuala ya uongozi jinsi ulivyo mbovu na ugawanywaji mbovu wa vyanzo vya uchumi na bidhaa.
  • Sura ya tatu, JINJA MALONI:Katika sura hii tunaelezwa kuhusu maisha ya Jinja Maloni, hapa anaibua dhamira kama vile za uvamizi, uhalifu na mauaji pia anaendela kutueleza kuhusu hali ngumu ya maisha.
  • Sura ya nne SEGA:Maisha ya wakazi wa Sega yanaelezewa hapa jinsi yalivyo ya dhiki, pia tunaelezwa kuhusu Tino na mkewe maisha yao yalivyo na familia yao, anaibua dhamira ya mapenzi ya dhati na upendo kwa familia.
  • Sura ya tano, BOKO:Hapa tunaelezwa kuhusu adha ya usafiri kwa watu, shida ya mafuta, ubovu wa miuondmbinu kama vile barabara, vinasemwa hapa.
  • Sura ya sita, BROWN KWACHA:Sura hii inaeleza habari za Brown maisha yake na tabia zake, anaibua dhamira kama vile uhujumu uchumi, biashara za magendo, suala la kutowajibika kwa watumishi, suala la kukosekana kwa uaminifu katika ndoa na mapenzi ya pesa ambapo sifa zote hizi alizibeba Kwacha.
  • Sura ya saba, KWALE:Hapa yanaelezwa mambo kuhusu hifadhi ya Kwale, safari ya Brown na Leila kwenda kutembea kwale. Hapa yanatajwa mambo ya udhalimu wa kuharibu mali za umma (maliasili za taifa) mfano pembe za ndovu, vipusa pia mapenzi yasiyo ya kweli.
  • Sura ya nane, DAKTA MIKWALA:Dakta Mikwala ndiye mhusika mkuu anayeelezwa hapa, tunalezwa juu ya ugumu wa upatikanaji wa huduma za afya kwani Cheche anashindwa kutibiwa kutokana na ukosefu wa fedha za kigeni.
  • Sura ya tisa, CHECHE:Tunaelezwa juu ya juhudi za Amani na Tino ili kumsaidia Cheche aweze kwenda kutibiwa Uingereza. Wanafanikiwa kupora benki na kupata pesa za kumtibu Cheche.
  • Sura ya kumi, MOTO:Hapa hatma ya visa vidogo vidogo imeelezwa kwa kutolewa hatma ya maisha ya Cheche na Brown Kwacha. Cheche alipata matibabu na kupona na Browna anafanikiwa kuirubuni serikali kwa kuipanga mahesabu ya uongo.
MTINDO
Mwandishi ametumia mitindo ya aina tofautitofauti ili kuweza kuipamba kazi yake ivutie.
  • Matumizi ya nafsi ya tatu Umoja. Imetawala: Mfanouk.5“Amani aliangalia…….” Uk.25 “Amani alijizuia” .Nafsi ya tatuwingi;mfano uk. 63“ wote walitoka nje kuelekea klabuni”.Piauk.53 “wale wanaume walimvamia”
  • Matumizi ya nafsi ya pili: Mfanouk.106 “ mmechoka kuangalia video?” “aa tumeshaziona mara nyingi tunaombaainanyingine.” Mazungumzo baina ya mke wa Brown na wanae.Pia mazungumzo baina ya Brown na Leila.Uk.113. “habari za asubuhi”“ Nzuri sijui wewe” alijibu“Uliota njozi njema?”"Wapi?""Kwa nini?"
  • Matumizi ya nafsi ya kwanza: Mfanouk. 39 “mimi nimemaliza” “….kuiba nimeiba sana….”
  • Matumizi ya nyimbo.Uk.70. wimbo wa Chaupele: “Chaupele mpenzi, haya usemayoKama ni maradhi, yapeleke kwa DaktariWanambia niache rumba,na mimi sikuzoeaSitaweza kuliacha rumba, kwa sababu yakoKama wanipenda, nenda kwa baba”Piauk.58 “sega! Sega! Sega!, usioogope” wimbo waliouimba washabiki wa michezo.
  • Masimulizi ya hadithi ndani ya hadithi: Hapa mwandishi amemtumia muhusika kusimulia kisa kingine kidogo ndani ya kisa kikuu. Mfanouk.39mhusika Tino anamsimulia mteja wake maisha yake ya mwanzo kabla hajaanza kazi ya kuvuta kwama.
MATUMIZI YA LUGHA
Mwandishi A. Safari ametumia lugha fasaha na inayoeleweka kwa wasomaji wake. Kuna matumizi ya lugha nyinginezo kama vile kiingereza.Uk.55 “city devils” uk.155 “I miss my family”, uk.24 “Hey man you will pay extra money”, uk.99 consignment”.Pia kuna matumizi ya lugha ya kiarabu, mfanouk.45 “Salaam aleikum mayitun” uk.42 “Inna Ilayhi Raajiunna!”, uk.13, “Insha Allah!”. Vilevile kuna matumizi ya lugha ya mtaaniuk.39 “msela”, “ndito”, “kashkash”.
Matumizi ya tamathali za semi.
  • Tashibiha:Uk.117 “ngozi yake nyeusi kama udongo wa mfinyanzi”Uk.122 “mweusi kama sizi la chungu”Uk.9 “Zepher 6 ile iliunguruma kama simba dume”Uk.10 “mteuzi mithili ya Mbega”Uk.35 “……miguu yake ikakazana mithili ya upinde uliotaka kufyatuliwa”
  • Sitiari:Uk.91 “Brown Kwacha alikuwa kinyonga”Uk.15 “sarahange wetu mboga kweli siku hizi”Uk.40 “huku twakaa vinyama vya mwitu”Uk.72 “sote ni kobe”
  • Tashihisi:Uk.109 “……gari lile zuri lilioondoka kwa madaha” Uk.143 “ kuta nyeusi za nyumba zaidi ya kumi zilisimama twe!kuomboleza” Uk.91 “pua zake zikalakiwa na riha na ashrafu ya manukato”;Uk.12 “utumbo ulimlaumu”; Uk.27 “mvua ikapiga kwa kiburi na kuviadhibu vibati vibovu”.
  • Tafsida:Uk. 49 “isijekuwa nimekukatiza haja!”,piauk.hohuo“kinyesi”.
Mbinu nyingine za kisanaa.
  • Takriri:Uk.151 “mwizi! Mwizi! Jambazi! Jambazi!”Uk.57 “shinda! Shinda! Shinda!”Uk.33 “karibu baba, kariibu kaka, karibu mkwe” Uk.72 “uhuru upi? Uhuru gani? Uhuru wa nini na nani?”
  • Mdokezo:Uk.149 “lakini……..”
  • Onomatopea au tanakali sauti:Uk. 1 “saa mezani niliendelea kugonga taratibu ta! ta! ta!”; Uk.10 “ikatoka sauti kali tupu ta nye nye”;Uk.67 “upepo wa stova uliolia shshsh”;
  • Tashtiti:Uk.113. leila anamuuliza Brown maswali ambayo anayajua majibu yake. Brown:“uliota njozi njema? Leila: Wapi?” Leila:Kwanini? Brown:Mwenywe unajua”
  • Nidaa:Uk.39 “Aaa! Limbukeni wa jiji anataka kunitia kashkash”: Uk 30 “nguo zangu Mungu wee!” Uk.42 “Inna Lillah wa Inna Ilayhi Raajiunna!” Uk.92 “Ah! Leila kwacha alimsalimia kwa furaha” Uk. 105 “Lahaula”
Matumizi ya Semi.
  • Methali:Uk.78 “asilojua mtu ni usiku wa kiza”Uk.83 “ukiona mwenzako anyolewa zako tia maji”Uk.98 “mtaka waridi sharti avumilie miiba”Uk. 99 “biashara haigombi”Uk.43 “ajizi nuksani huzaa mwana kisirani”
  • Misemo:Uk.10 “asiye na bahati habahatishi”Uk.47. “asiyezika hazikwi”Uk.64 “mmetupa Jongoo na mtiwe”Uk.98 “asali haichomvwi umoja”Uk.111 “ajali haina kinga”Uk.115 “mwenye macho haambiwi tazama”Uk.120 “matendo hushinda maneno”Uk.47. “asiyezika hazikwi”
  • Nahau:Uk.11 “sio unanilalia kila mara” –kunidhulumuUk.107 “alikonda akajipa moyo” –kujifariji moyo
Matumizi ya taswira
Taswira mwonekano imetumika, ambayo inatujengea picha kutokana na vitu tunavyovifahamu. Mfanouk.76 “alisema kijana mmoja wa kiume kavaa sketi, blauzi na sidiria iliyopachikwa juu yake. Kichwani alifunga kilemba.”Hii inatupa picha halisi ya huyo kaka kwani tunaposoma ni kama kweli tunamuona kutokana na jinsi mwandishi alivyoelezea. Piauk.135 “mwambie yule jamaa pale atayarishe kuku mzuri wa kukaanga”……… na kachumbari yenye pilipili”hii inamfanya msomaji ahisi ladha ya kuku na hiyo pilipili kwa maneno ambayo mwandishi ameyajengea taswira na hii ni taswira hisi.
Joka lamdimuni taswira ya nyoka mbaya ambaye amefananishwa na viongozi wabaya.
WAHUSIKA
AMANI
  • Ni dereva taxi
  • Ana upendo wa dhati
  • Ni mchapakazi
  • Ana hekima na busara
  • Ana huruma
  • Ni rafiki wa kweli wa Tino
  • Kutokana na hizo sifa amani ni mhusika bapa
  • Anafaa kuigwa na jamii
TINO (mhusikabapa)
  • Ni mchapakzi
  • Mlezi bora wa familia
  • Baba wa Cheche
  • Ana huruma
  • Ana upendo wa dhati
  • Ni makini
  • Ni jasiri
  • Ni mwanamichezo
  • Anafaa kuigwa na jamii
BROWN KWACHA
  • Ni mkurugenzi wa idara ya fedha za kigeni
  • Ni muhuni na Malaya
  • Fisadi na mla rushwa
  • Anafanya biashara haramu
  • Hana mapenzi kwa familia yake
  • Anapenda anasa
  • Si muaminifu kwa mkewe
  • Si muadilifu
  • Hafai kuigwa na jamii
  • Ni mhusika bapa
JINJA MALONI
  • Ni jasiri na mwenye nguvu
  • Ana huruma na upendo
  • Mchapakzi
  • Mlevi
  • Maskini
  • Ni mhusika duara
DAKTARI MIKWALA
  • Ni daktari bingwa wa mifupa
  • Anapenda rushwa
  • Si muwajibikaji katika kazi yake
  • Ni mlevi
  • Hafai kuigwa na jamii
  • Ni mhusika bapa
SHIRAZ BHANJ
  • Ni mfanyabiashara
  • Ni mtoa rushwa
  • Ana biashara za magendo
  • Rafiki wa Brown
  • Hafai kuigwa na jamii
  • Ni mhusika bapa
ZITTO
  • Ni mfanyakazi bandarini
  • Ni mwanamichezo
  • Ni jasiri ana kipato duni
  • Rafiki wa Tino na Aman
CHECHE
  • Ni mtoto wa Tino
  • Ana nidhamu na bidii
  • Ni mwanamichezo
  • Ana upendo kwa wazazi wake
  • Ni mtiifu na msikivu
  • Mcheshi na mudadisi
  • Alivunjika kiuno michezoni
  • Ni mhusika bapa
MWEMA
  • Ni mke wa Tino
  • Mvumilivu
  • Ana mapendo ya dhati kwa familia yake
  • Ni mchapakazi
  • Ni mhusika bapa
JOSEPHINE NA LEILA
  • Wasichana wahuni waliojiuza kwa Brown Kwacha
  • Hawafai kuigwa na jamii
MANDHARI
Mandhari aliyoitumia mwandishi ni ya mjini, anataja baadhi ya maeneo ya nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kama vile Boko, Sega, Mindule. Mandhari hii ni sadifu kwa yale ambayo mwandishi ameyaeleza kwani masuala ya rushwa, upotevu wa haki, hali ngumu ya uchumi na maisha kwa ujumla, ni matatizo halisi ya jamii ya Tanzania.
Fani katika Riwaya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe
Hakiki fani katika Riwaya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe
JINA LA KITABU: NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE
MWANDISHI: EDWIN SEMZABA
WACHAPISHAJI: NYAMBARI NYANGWINE PUBLISHERS
MWAKA:2006
UTANGULIZI WA KITABU
Ngoswe penzi kitovu cha uzembe ni tamthiliya maarufu sana ambayo imewahi kuigizwa katika redio Tanzania na katika majukwaa mbalimbali hapa nchini. Ni tamthiliya ambayo imeundwa vyema katika vipengele vya fani na maudhui. Ameteua lugha nzuri na yenye mvuto kwa wasomaji yenye mbinu za kifasihi zilizosheheni, muundo wenye mtiririko mzuri, unaoakisi kuanza kuchipuka kwa matukio mpaka kilele cha matukio. Wahusika wamebeba vyema uhusika wao mfano Ngoswe.
Ameibua dhamira kuhusu mambo yanayoigusa jamii ya leo kama vile uzembe, madhara ya ulevi, uzembe kazini, suala la matabaka kati ya mjini na vijijini. Mtazamo, falsafa na msimamo wake ni kulenga kuibadilisha jamii na kuleta maendeleo.
JINA LA KITABU
Jina la kitabu “Ngoswe penzi kitovu cha uzembe” ni jina ambalo limesawiri vyema yaliyomo ndani ya kitabu hicho, kwani Ngoswe ndio jina la mhusika mkuu anayebeba dhamira kuu ya tamthiliya. Pia penzi limeonekana kuwa ni kitovu cha uzembe kwani ndio yaliyopelekea kuteketezwa kwa karatasi za takwimu za sensa. Hivyo jina la kitabu si tu kwamba limesawiri yaliyomo katika kitabu bali pia katika jamii.
MTINDO
Mtindo alioutumia mwandishi ni dayalojia au majibizano. Mwandishi amepanga visa na masimulizi kwa kutumia majibizano ya wahusika.
  • Matumizi ya nafsi ya kwanza. Mwandishi ndiye ameyafafanua na kuelezea baadhi ya matukio. Katika karibu kurasa zote mwandishi ameonekana kuwa ndiye msimuliaji wa matukio.
  • Matumizi ya nafsi ya pili. Hapa watu wawili na zaidi wanajibizana. Tamthilya hii wahusika wanaojibizana kuibua dhamira na migogoro. Kuna majibizano baina ya mzee Mitomingi, Ngoswe na Mazoea nk.unaweza kupata mfano uk. wowote kwani ndio mtindo uliotawala.
MUUNDO
Muundo uliotumika ni muundo wa mojakwamoja au sahili. Kwani ameonesha tangu mwanzo wa mambo mpaka mwisho, anajenga visa vidogo mpaka visa vikuu au kileleni.Amepanga visa na matukio yake katika maonesho matano. Kila kichwa kina maelezo yaliyojadiliwa katika onesho hilo.
  • KIJITO:Hapa yanaeleza jinsi mambo yanavyoanza. Jinsi Ngoswe anavyoingia kijijini anavyopokelewa na kuanza kufahamiana na wenyeji wake.
  • VIJITO:Hapa Ngoswe anaanza kufanya kazi iliyompeleka kijijini na tunaanza kuoneshwa changamoto anazokumbana nazo.
  • MTO:Ni mwendelezo wa matukio ya mwanzo hapa visa vinazidi kukua.
  • JITO:Hapa Ngoswe anakumbana na changamoto nyingi zaidi katika kazi yake. Na hapa anazidi kuanguka kwani anajiingiza katika mapenzi na msichana Mazoea, anaendekeza ulevi na kuharibu kazi kabisa.
  • BAHARINI:Hapa inaoneshwa mwisho wa mambo jinsi yalivyokuwa. Yanaonekana mahojiano baina ya Serikali na Ngoswe na Mitomingi juu ya uzembe uliofanyika wa kupoteza takwimu na hapa ndipo suluhisho linapotolewa juu ya matatizo hayo.
WAHUSIKA
NGOSWE
  • Kijana wa kiume umri kati yamiaka 20-25
  • Ameelimika na amestaarabika
  • Anatumwa na serikali kufanya sensa kijijini
  • Anajihusisha na mapenzi na msichana mazoea
  • Ni mlevi
  • Hana umakini katika kazi
  • Aliharibu kazi ya serikali
  • Hafai kuigwa na jamii
MAZOEA
  • Ni msichana mwenye umri kati ya miaka 18-20
  • Ni binti wa Mzee Ngengemkeni Mitomingi
  • Hana elimu na hajastaarabika
  • Ana nidhamu ya woga
  • Ana tama
  • Hana msimamo alikubali kuchukuliwa na Ngoswe hali akijua alishatolewa mahari
  • Hafai kuigwa na jamii.
NGENGEMKENI MITOMINGI
  • Ni balozi katika kijiji chake
  • Ni baba mzazi wa Mazoea
  • Ameoa ndoa ya mitara, ana wake wawili
  • Hajaelimika
  • Anashikilia mila na desturi za kale
  • Mlevi
  • Mkali sana
  • Anateketeza karatasi za takwimu
MZEE JIMBI
  • Mwanakijiji
  • Hajaelimika kwani hajui hata umri wake
  • Ni mlevi
  • Ana wake wawili
  • Anashikilia ukale
MAMA MAZOEA
  • Mke mkubwa wa Mitomingi
  • Mama yake Mazoea
  • Mlezi wa familia
  • Hapewi nafasi ya kutoa maamuzi katika familia
MAMA INDA
  • Mke wa pili Mzee Mitomingi
  • Mama yake Huzuni
  • Hapewi nafasi ya kutoa maamuzi
  • Ni mlezi wa familia.
MANDHARI
Mandhari ya tamthiliya hii imechorwa katika mazingira ya kijijini. Mambo yanayoelezwa ni ya kijijini mfano kilimo, hali ya watu kimaisha, huduma duni sana za kijamii kama vile shule, umbali wa makazi toka nyumba moja hadi nyingine. Haya yanatudhihirishia vyema mandhari hiyo ambayo kwayo imeibua dhamira mbalimbali kama vile umaskini, ukosefu wa elimu, huduma duni za afya vijijini, masuala ya imani potofu nk.
MATUMIZI YA LUGHA
Lugha aliyotumia mwandishi ni lugha fasaha na rahisi kueleweka kwa wasomaji. Pia kuna matumizi ya lugha nyingine mfanouk. 1 “bell bottom”
Matumizi ya semi
  • Methali:Uk.22 “Penye nia pana njia”.Uk.27 “Waona vyaelea vyaundwa.”
  • Misemo:Uk.14 “Akuwaniae ujovu haji kweupe”
  • Nahau:Uk.11 “hebu keti tutupe mawe pangoni” –tule chakulaUk.7 “mbongo zimelala”-ana maarifaUk.14 “pombe na yeye ni pete na chanda”- anapenda pombe sana.
Matumizi ya tamathali za semi
  • Tafsida:Uk.21 “Wala hajarudi, kama ingekuwa ni kujisaidia si angekuwa amekwishamaliza?”
  • Tashbiha:Uk.1 “vumbi jekundu kama ugoro wa subiana”Uk.8 “sarawili yake miguuni kama kengele ya bomani”Uk.17 “wanaondoka huku wakitazamwa kama vile mizuka”
  • Sitiari:Uk.7 Mama Mazoea : “kiziwi mkubwa wee!”Uk.14 “pombe na yeye ni pete na chanda!”Uk.26. “karatasi? za takwimu? Ndio wanyama gani hao?”
  • Mubaalagha:Uk.11 Mama Mazoea : “kupeleka chakula ndio umefanya makao!”Mama mazoea : “Kujibu swali ndio ukachukua mwaka mzima!”
Mbinu nyingine za kisanaa
  • Mdokezo:Uk.22 Mazoea : “sijui….. siwezi….. namuogopa baba”Uk.16 Ngoswe : “huyo mtoto wenu wa kwanza anaishi hapa au…..”
  • Takriri:Uk.9 “Mama Masikio! We Mama Masikio!”Uk.13. “Hodi! Hodi!”Uk.2 “karibu karibu”
  • Tashtiti:Uk.5 Ngoswe: “hivyo waitwa nani?”Mazoea: “mie?”Uk.22 Ngoswe: “mchumba? Kwani mchumba ni kitu gani?”Uk.26 Mitomingi: “karatasi? Za takwimu? Ndio wanyama gani hao?Hapa wahusika waliuliza maswali ambayo majibu yake waliyaelewa ila kutokana na kutaka kudhihirisha hasira, msisitizo nk. Ndio maana wametumia tashtiti.
  • Onomatopea/tanakali sauti:Uk.7 Kifaruhande anacheka “Ha! ha! ha!
Ujenzi wa taswira
Mwandishi ametumia taswira ya mto kuelezea visa vyake. Sehemu ya kwanza ni sehemu ya kijito, kijito ni kimto kidigo mwandishi hapa anaanza kueleza mambo yakiwa machanga kabisa ndio yanaanza.
Sehemu ya pili ni vijito. Huu ni muunganiko wa vijito vidogovidogo hapa mwandishi anaanza kueleza visa vidogovidogo. Sehemu inayofuata ni sehemu ya Mto. Hii inaashiria mambo yameanza kuwa mazito, visa vinakua zaidi na Ngoswe anazidi kuingia katika changamoto kubwa zaidi.
Pia Jito ni taswira ambayo mwandishi ameitumia kuashiria hatari zaidi mambo makubwa zaidi na hapa ndipo tunaona Ngoswe anaanguka kabisa katika kazi yake kwani Jito ni lenye maji mengi na yanayoenda kwa kasi hivyo huhitaji umakini mkubwa zaidi.
Mwisho sehemu ya Bahari ambapo hapa ndipo hatima ya mambo inaelezwa Ngoswe anazama na kupotea kabisa! Hafanikiwi kutoa takwimu kwani karatasi zilichomwa moto.

Fani katika Tamthiliya ya Kilio Chetu
Hakiki fani katika tamthiliya ya Kilio Chetu
MWANDISHI: MEDICAL AID FOUNDATION
WACHAPISHAJI: TANZANIA PUBLISHING HOUSE (TPH)
MWAKA: 1996
JINA LA KITABU
KILIO CHETU ni jina ambalo linaasadifu yaliyomo katika kitabu. Masuala yanayotajwa mule kama vile upotofu wa maadili kwa vijana wadogo kama Suzi na Joti, suala la mimba za utotoni, madhara ya gonjwa hatari la UKIMWI kwa jamii kweli ni kilio chetu ni kilio cha Taifa zima. Kwani katika mambo yanayoiyumbisha jamii kimaendeleo ni upotovu wa maaadili.
Jina hili ni sadifu katika jamii. Mwandishi amelitumia wakati muafaka kabisa kwani mambo anayoyaeleza ndio changamoto katika jamii ya leo. Hivyo kupitia hili jamii si budi kubadilika.
UTANGULIZI WA KITABU
Kilio chetu ni tamthiliya ambayo imejieleza vyema katika fani na maudhui. Tamthiliya hii inamuhusu mhusika Suzi na Joti ambao ni watoto wadogo sana. Wanajiingiza katika mapenzi katika umri mdogo kutokana na ukosefu wa elimu ya kijinsia. Inatueleza kuhusu athari za ugonjwa huu usiobagua. Pia tunafahamishwa kuhusu mtazamo wa wazazi na walezi kuhusu utoaji wa elimu ya jinsia kwa vijana wao. Wapo wanaolipokea kwa mtazamo chanya na wengine hasi.
Kwa ujumla ni tamthiliya nzuri kwani ina mtazamo wa kimabadiliko unaolenga kuwakomboa vijana wetu kutoka katika janga la ugonjwa hatari wa UKIMWI.
MUUNDO
  • Sehemu ya kwanza:Inaonesha jinsi gonjwa la UKIMWI linavyoikumba jamii. Mwandishi anaeleza kuhusu Dubwana linaloikumba jamii.
  • Sehemu ya pili:Mwandishi anaeleza kuhusu athari za UKIMWI, jambo ambalo lilipelekea kifo cha Fausta. Pia Suzi agundulika kujihusisha na mapenzi baada ya kukutwa na vidonge vya kuzuia mimba.
  • Sehemu ya tatu:Inaeleza juu ya watoto ambao wameshajiingiza katika suala la mapenzi licha ya kuwa na umri mdogo mfano ni Joti na Suzi. Pia madhara ya utandawazi yanaelezwa hapa mfano kuoneshwa kwa picha za ngono.
  • Sehemu ya nne:Tunaelezwa juu ya tabia hatarishi za Joti za kuwa na mahusiano na wasichana wengi mfano Chausiku, Yoranda, Gelda na Suzi. Hapa Joti anafanikiwa kumrubuni tena Suzi. Pia tunaoneshwa jinsi Ana anavopingana na vishawishi kutokana na kupata elimu ya jinsia.
  • Sehemu ya tano:Suzi anagundulika kuwa na mimba ya Joti, anajutia kosa hilo anajilaumu sana.
  • Sehemu ya sita:Inatuonesha jinsi Joti alivyokuwa magonjwa tayari kutokana na UKIMWI. Hapa ushauri mzuri unatolewa kuhusu namna ya kumtunza mgonjwa wa UKIMWI na kumfanya aishi kwa matumaini. Hapa mwandishi anapinga mila potofu kuhusu UKIMWI kuwa si kurogwa bali ni ugonjwa unaoambukizwa.
MTINDO
Tamthiliya hii imesheheni katika mitindo kadha wa kadha inayopamba kazi hii. Mtindo uliotumika ni dayalojia au majibizano.
Mwandishi ametumia mtindo wa mianzo na miisho ya kifomula ya usimulizi ambao ni mtindo wa usimulizi wa fasihi ya kiafrika. Mfanouk.1 mwandishi anasema “paukwa….. pakawaa…. Niendelee…. nisiendelee? ….. au mmechoka? Uk.113,piauk.36 mwandishi anasema “na hadithi yangu imeishia hapo”.Pia mwandishi ametumia mtindo wa utambaji kwani ndiye anayesimulia na kuelezea matukio.
Matumizi ya nafsi
Nafsi ya pili ndiyo iliyotawala, mwandishi ametumia majibizano ya watu wawili mfano Suzi na Joti, pia watu watatu n.k.Pia mwandishi ametumia tanzu nyingine za fasihi mfano wimbo uk.27
Wahusika
SUZI
  • Ni binti mdogo wa darasa la sita
  • Anajihusisha na mapenzi na Joti
  • Hana msimamo
  • Anapata mimba katika umri mdogo
  • Ana hatari ya kuwa na UKIMWI
  • Hakupewa elimu ya jinsia
  • Ana tamaa kwani alitamani vitu alivyohongwa na Joti.
JOTI
  • Ni kijana mdogo wa kiume
  • Ana mahusianao ya mapenzi na wasichana wengi Suzi, Gelda, Yoranda na Chausiku
  • Hana elimu ya jinsia
  • Ana makundi mabaya ya marafiki
  • Anaathirika na kufa kwa gonjwa la UKIMWI
  • Amechangia kuharibu maisha ya Suzi kwa kumrubuni
  • Ni mlaghai
  • Hafai kuigwa na jamii
MAMA SUZI
  • Ni mzazi wa Suzi
  • Anashikilia ukale hataki mabadiliko
  • Hampi mwanae elimu ya jinsia
  • Alichangia kuharibu maisha ya Suzi
  • Ni mkali sana katika malezi hatumii busara bali hasira
  • Hafai kuigwa na jamii
BABA JOTI
  • Ni mzazi wa Joti
  • Hayupo tayari kutoa elimua ya jinsia
  • Anashikilia ukale
  • Ni mkali anatumia viboko kuelimisha jambo ambalo si sahihi
  • Amechangia kuharibu maisha ya Joti
  • Ni muhuni, si muaminifu katika ndoa yake
  • Hafai kuigwa na jamii
ANNA
  • Ni binti mdogo wa shule
  • Ana elimu ya jinsia
  • Ana msimamo mzuri anashinda vishawishi
  • Anatoa elimu kwa vijana wenzake kuhusu athari za kujiingiza katika mapenzi katika umri mdogo
  • Ana tabia njema
  • Hana tama
  • Anafaa kuigwa na jamii.
BABA ANNA
  • Ni mzazi wa Anna
  • Anatoa elimu ya jinsia kwa wazazi na watoto
  • Ni mlezi bora
  • Alichangia maisha ya Anna kuwa ya mafanikio
  • Anafaa kuigwa na jamii
MJOMBA
  • Ni kaka yake Mama Suzi
  • Anaendana na wakati wa sasa
  • Anatoa elimu ya jinsia kwa vijana na wazazi
  • Ni mlezi bora ni mshauri bora
  • Anatoa elimu ya UKIMWI kwa Baba Joti anapinga mila potofu
  • Anafaa kuigwa na jamii
MAMA JOTI
  • Mzazi wa Joti
  • Ndoa yake ipo matatani kuingiliwa na mke mwingine
  • Anaelewa kuwa jamii imebadilika na wazazi wanapaswa kuwaelimisha watoto
JIRANI
  • Ni jirani wa Baba Joti
  • Ana imani potofu za kishirikina, anaamini Joti alilogwa
  • Haamini kuwa UKIMWI upo
CHAUSIKU
  • Ni msichana wa mtaani
  • Mfanyabiashara wa vitumbua
  • Ni jirani wa Suzi
  • Ana tabia mbaya ni muhuni
  • Alichangia kuharibu maisha ya Joti
  • Ana mahusiano ya kimpenzi na vijana wadogo mfano Joti na watu wazima pia, mfano Mpemba.
CHOGO, MWARAMI NA JUMBE
  • Ni marafiki wa Joti
  • Ni wanafunzi wadogo
  • Si marafiki wazuri
  • Wana tabia mbaya wanashauriana kuhusu mambo mabaya
  • Hawafai kuigwa na jamii
MANDHARI
Mandhari aliyoitumia mwandishi ni ya mjini, hii ni kutokana na maelezo ya mhusika jirani anaposemauk.32 “……mie toka siku ile nimwone hospitali sijakaa mjini. Nilikwenda zangu shamba kupambana na Nyani wala nafaka.”Pia lugha ya mtaani iliyotumiwa na vijana Joti, Mwarami na wenzake, masuala ya picha ya “X” yaani viashiria vya mambo ya mjini kwani yamekithiri sana mijini. Maeneo yanayotajwa kama vile uwanja wa Sabasaba ni uwanja uliopo mjini, masuala ya lifti kwa wasichana hasa wanafunzi yapo mijini. Mfano.uk.27 pia kuna mandhari ya nyumbani na mtaani.
Mandhari aliyotumia mwandishi inasawiri maudhui yake katika jamii. Kwani anaibua mambo yaliyo katika jamii.
MATUMZI YA LUGHA
Lugha iliyotumika ni lugha iliyo na ubunifu wa kipekee wenye mvuto wa kisanaa. Lugha ni rahisi na inayoeleweka vyema kwa hadhira lengwa. Pia kuna matumizi ya lugha nyingine mfano kiingereza na lugha za kikabila. Kiingereza mfanouk.21 “tuition” uk.16 “come”.Lugha za kikabila mfano wimbo uk.35“Joti afitwe sanda salauya; Ena ena salauya …………………….”
Matumizi ya lugha ya mtaani
Mfanouk.16 “mshefa” “mshikaji”-rafiki.Uk.17 “kamba” –kudanganya jambo;Uk.22 “vidosho” –wasichana;Uk.16 “kanitolea nje”– kukataa jambo fulani.
Matumizi ya tamathali za semi
  • Tashibiha:Uk.1 “wakapukutika kama majani”Uk.5 “mgumu kama mpingo”Uk.6 “miti inaungua kama mabua”Uk.13 “Dubwana limetanda kama utando wa Buibui”
  • Tashihisi:Uk.2 “vifo vikawazoa”kifo huua tu lakini kimepewa uwezo wa kuzoa
  • Sitiari:Uk.8 “We Mbwa mweusi”Uk.9 “Nyoka wee”Uk.21 “huyo kinyago wako anakimbia nini?”
  • Tafsida:Uk.4 “kafa kwa kukanyaga nyaya”– kafa kwa UKIMWI
  • Mubaalagha:Uk.4 “Mtu si mtu, kizuka si kizuka”
Matumizi ya mbinu nyingine za kisanaa
  • Tanakali sauti/ Onomatopea:Uk. Joti akasema“….acha moyo unipwite “Pwi! Pwi! Pwi!”Uk.25 “….hebu nitolee uchafu wako mie ptuu!”
  • Tashtiti:Uk.15 “….huyu ni Suzi kweli au nani?”Uk.36 “kwanini Joti……… kwanini Joti afe?”
  • Takriri:Uk.1 “watu wakapukutika, wakapukutika…..” “tunakwisha, tunakwisha”Uk.2 “vifo vikawzoa, vikawazoa .…. vikawazoa”Uk.16 “piga domo, piga domo”
Matumizi ya semi
  • Methali:Uk.6 “wembamba wa Reli Treni inapita”Uk.11 “mzazi usipomfunza walimwengu watamfundisha”Uk.19 “shukrani ya Punda ni mateke”Uk.24 ‘Ndege mjanja ananaswa na tundu bovu
  • Nahau:Uk.6 “nimekuvulia kofia”-nakuheshimuUk.21 “anajigongagonga” –anajipendekeza
  • Misemo:Uk.4 “kuwa nyumanyuma kama koti”Uk.6 “kifua simkingii maana siwi naye”Uk.7 “makapera kibao Mume wangu wa nini?”Uk.22 “mapenzi ni tiba”Uk.26 “…..unakimbilia suti na nepi hujavaa”
Matumizi ya taswira
uk.1 “dubwana” –ugonjwa wa UKIMWI;Uk.7 “Nguru” –aina ya Samaki wabayaamefananishwa na mtu mbaya;Uk.21 “kinyago”- Suzi.
Fani katika Tamthiliya ya Orodha
Hakiki fani katika tamthiliya ya Orodha
JINA LA KITABU
Jina la kitabu ORODHA ni sadifu kwa yaliyomo. Katika kitabu inatajwa orodha ya mambo ambayo yanaweza kusaidia kuepusha UKIMWI. Orodha hii inatolewa na mhusika Furaha ambaye aliomba isomwe katika mazishi yake. Mambo hayo au orodha hiyo ni pamoja na uwazi, ukweli, uadilifu, matumizi ya kondom, uelewa, upendo, elimu, uwajibikaji na msamaha. Mwandishi anaona kuwa endapo mambo haya yatazingatiwa hakika tutapunguza maambukizi zaidi ya virusi vya UKIMWI.
UTANGULIZI
Tamthiliya ya Orodha ni tamthiliya inayohusu suala zima la ugonjwa wa UKIMWI na madhara yake katika jamii. Mwandishi anaweka wazi kuhusu gonjwa hili. Mhusika mkuu Furaha anaathirika na gonjwa hili na kufariki dunia. Kimaudhui tamthiliya hii imesawiri maisha ya sasa ya jamii ya Watanzania kwani ugonjwa huu bado ni tishio. Kwa upande wa fani, mwandishi amewaumba vyema wahusika wake, muundo wake ni unaomvutia msomaji kujua ni nini kingeendelea mbeleni, ameteua lugha nzuri ya kisanaa. Haya yote yanajielekeza katika uchambuzi tutaoenda kuufanya.
MUUNDO
Mwandishi ametumia muundo changamano kwani katika sehemu ya 1 na 2 anatuonesha mazishini ambapo yanafanyika mazishi ya Furaha. Sehemu ya 3-20 anaanza kutuelezea juu ya maisha ya Furaha mpaka kifo chake ambao huu ni msago au muundo sahili. Halafu sehemu ya 17-19 na ishirini 20 anatuonesha juu ya mzozo wa orodha na hatma ya mazishi ya Furaha.
Mwandishi ameweka kazi yake katika onyesho moja. Na katika onyesho hilo ameweka sehemu ndogondogo ishirini zinazojengana kukamilisha tamthiliya nzima.
  • Sehemu ya kwanza:Inaanza kwa kuonesha vifani vinne vimeganda kifani cha kwanza, wahusika wameganda katika mikao inayotambulisha wasifu wa wahusika. Kifani cha pili kinaonesha wagonjwa wakiwa katika mateso. Kifani cha tatu kinaonesha wagonjwa wakiwa katika maumivu makali sana.
  • Sehemu ya pili:Hapa inaelezwa juu ya siku ya msiba wa Furaha. Mama yake Furaha anaeleza watu kuwa Furaha aliacha orodha ambayo alitaka isomwe hadharani katika mazishi yake. Suala hili linazua mgogoro na hofu kuu kwa watu. Padre James anaweka juhudi kuzuia barua isisomwe.
  • Sehemu ya tatu:Sehemu hii tunaoneshwa juu ya maisha ya Furaha nyumbani kwao, baba na mama yake na wadogo zake. Baba yake anaonekana kutofurahishwa na mwenendo wa Furaha kwani anamkanya kwa maneno makali ya laana. Kama vile hatopata mtu wa kumuoa. Anamuasa Furaha kuonesha mfano mzuri kwa wadogo zake.
  • Sehemu ya nne:Hapa Furaha kwa mara ya kwanza anatoroka nyumbani kwao usiku wa manane pamoja na Mery kwenda baa. Mdogo wake anabaini kitendo hicho na kutishia kushitaki kwa wazazi lakini Furaha anamtishia kumchinja.
  • Sehemu ya tano:Wanaonekana Mery na Furaha wako baa wakinywa pombe na kucheza na wanaume. Hapa Furaha anajifunza mambo mapya mabaya kama vile ulevi kupitia rafiki yake Mery. Pia anaanza mahusiano ya mapenzi na wanaume mfano Bw. Ecko.
  • Sehemu ya sita:Hapa Furaha anamwendea Padre James kwa ajili ya maungamo kwani alikunywa pombe na kulala na wanaume, lakini Padre James anamwambia Furaha aende kesho yake katika chumba chake cha kujisomea nyuma ya kanisa na taa zitakuwa zimezimwa kuficha utambulisho. Na hapa ndipo Furaha anapozini na Padre kwani Padre alishikwa na tamaa.
  • Sehemu ya saba:Baba na Mama Furaha wanamkanya Furaha kuhusu tabia yake ya umalaya na ulevi. Furaha anaomba msamaha.
  • Sehemu ya nane:Furaha anakutana na Kitunda aendapo sokoni, katumwa na mama yake. Lakini anamkuta Kitunda akisikiliza mziki Furaha anashawishika, Kitunda anamshawishi zaidi na hata avute bangi ila hakubali. Pia wanazungumzia juu ya jiji la Dar es Salaam. Habari hizo zinampagawisha Furaha na kutamani sana aende.
  • Sehemu ya tisa:Salim anarudi toka masomoni Dar es Salaam. Anaonana na mpenzi wake wa zamani Furaha. Wanasalimiana kwa hamu na furaha tele.
  • Sehemu ya kumi:Salim na Furaha wanakutana na kuelezana habari za kitambo kwani walitengana kwa muda mrefu, wanapanga mipango juu ya mahusiano yao.
  • Sehemu ya kumi na moja:Wanakijiji wanazungumzia juu ya tabia ya umalaya ya Furaha, pia wanazungumzia juu ya mahusiano ya Furaha na Salim. Hawapendezwi na tabia ya Furaha na kuamua kumtaarifu mama yake.
  • Sehemu ya kumi na mbili:Mama Furaha anachukua jukumu la kumhoji mwanae juu ya tabia yake. Furaha hakubaliani na lolote. Hali ya Furaha inaanza kudhoofu na mama yake anaaingiwa hofu.
  • Sehemu ya kumi na tatu:Furaha yupo sebuleni akisali. Baba yake anamuonya zaidi na kumshauri aolewe na Salim kwani ni kijana mzuri anayefaa.
  • Sehemu ya kumi na nne:Hapa hali ya Furaha inazidi kutetereka, anachukuliwa vipimo vya damu na kugundulika kuwa ana virusi vya UKIMWI. Hali hii inamshitua sana mama yake. Anamuhoji kama aliwahi kutembea na mwanaume yeyote, anamueleza njia za upataji wa UKIMWI na Furaha naanza kulia kwa kutambua kosa lake.
  • Sehemu ya kumi na tano:Wanakijiji wanapata habari juu ya kuumwa kwa Furaha na wanazieneza. Juma, Kitunda, Padre James, Salim, Bw. Ecko wanapata pia habari hizi. Wanaingiwa na hofu kubwa endapo watakuwa wameambukizwa UKIMWI au majina yao yamo kwenye orodha?
  • Sehemu ya kumi na sita:Salim anaamua kumtembelea Furaha nyumbani. Akiwa katika hali mbaya sana ya ugonjwa Furaha anamuweka wazi Salim juu ya kuathirika kwake kwa UKIMWI. Salim anaingiwa hofu anamuomba Furaha barua yenye orodha kwa shauku lakini hampatii. Hali hii inamuudhi Salim. Na hapa ndipo Furaha anapokata roho!
  • Sehemu ya kumi na saba:Hapa tunaelezwa juu ya juhudi za Bw. Ecko, na Juma za kutaka kuiba barua yenye orodha katika chumba alicholazwa maiti ya Furaha. Lakini hawafanikiwi. Familia ya Furaha wanaamini kuwa kuna mizimu katika chumba cha maiti kutokana na kelele za Juma na Bw. Ecko, na Kitunda.
  • Sehemu ya kumi na nane:Padre James anaomba kusomewa barua hiyo kabla ya mazishi lakini mama furaha anakataa. Anaamua kuitafuta mwenyewe sebuleni bila mafanikio.
  • Sehemu ya kumi na tisa:Asubuhi siku ya mazishi. Ecko, Juma na Salim wanaonekana wakitafuta suluhu ya namna ya kuzuia orodha isisomwe ila hawafanikiwi.
  • Sehemu ya ishirini:Ni siku ya mazishi ambapo Mama Furaha anaisoma barua ya orodha. Padre James anajitahidi kumpinga mama Furaha asiisome orodha lakini hafanikiwi. Salim anapora barua na kuchana baadhi ya sehemu lakini hiyo haiharibu kitu kwani anaunga vipande na kusoma mbele ya wanakijiji wote. Ndani ya orodha hakuna jina la mtu yeyote lililotajwa bali mambo yatakayosaidia kuuepuka UKIMWI.
MTINDO
Mtindo aliotumia mwandishi ni wa dayalojia au majibizano. Mwandishi ameunda visa na masimulizi yake kupitia majibizano ya wahusika. Pia kwa kiasi kidogo ametumia mtindo wa monolojia, mfano uk. 27 padre James anasema:
“Bwana natazamiwa kuiendesha sala hiyo! Ni kitu ambacho hakikubaliki! Shetani yu kazini kjijini hapa! Furaha anavuna mbegu ya kifo aliyoipanda! Oh! Njia ya mtumishi wa bwana ni ngumu. Imejaa majaribu! Mtu lazima awe na nguvu na kuileta kazi ya bwana kwa watu hawa wa kawaida. Nimepewa kazi iliyo rahisi lakini ni ngumu sana! ni kazi ya upweke!!! Mwili ni mdhoofu! Oh Bwana utulinde.”
Hapa padre James aliongea mwenyewe akifikiri kuwaza na kujutia kazi anayofanya. Pia uk. Huohuo tunaona maneno ya Salim anaongea mwenyewe, pia uk.10, 23,37 na 40.
Pia mwandishi ametumia mtindo wa barua katika kazi yake lengo ikiwa ni kuweka mkazo katika mambo muhimu ya kuzingatia ili kuiepuka UKIMWI. Barua yenyewe ilisema hivi, uk.44“Kwa Kijiji changu kipendwa,
Nawasukuru kwa kufika kwenu na kuyasikiliza maneno yangu ya mwisho. Msiogope kwani nadhani maneno haya yanaweza kuwasaidia. Katika hii miezi ya mwisho nimelala kitandani nikifa, nikizidi kuugua. Nilipata muda mwingi wa kufikiri, kubadilika kukua kama mtu; hata ninapokuwa nakufa. Katika ukurasa unaofuata kuna Orodha ya vitu amabvyo vilisaidia kuyafupisha maisha yangu, orodha ambayo inaonesha kwenu nyote ukweli juu ya kifo changu. Mama, tafadhali wasomee watu wote orodha hii.
  • Uepukaji
  • Kondomu,
  • uaminifu ,
  • elimu,
  • welewa,
  • uwazi,
  • uadilifu,
  • uwajibikaji,
  • ukweli,
  • upendo,
  • msamaha.
Ukosefu wa mambo yote haya ndio ulioniua. Ufuatiliaji wa mambo yote haya unaweza kuwaokoa ninyi nyote. Chukueni orodha yangu na muinakili. Ipelekeni kwenye vijiji vingine, miji mingine na majiji mengine katika nchi yetu hii nzuri. Wanusuruni watu wetu ili waweze kuyafaidia maisha kikamilifu .Wanusuruni watoto wetu ili wasiwe yatima. Muinusuru Afrika…. Afrika yetu nzuri
Kwa kijiji changu kiishi maisha marefu na kiwe na furaha! Msihukukumu mapema mno. Kwa Mama, baba dada zangu, nawapenda. Jaribuni kuwa wenye furaha wakati mnaweza kufanya hivyo.Wenu awapendae Furaha.”
Matumizi ya nafsi
Mwandishi ametumia nafsi mbalimbali na hii ni mifano:
  • Nafsi ya kwanza umoja na wingi:Uk.28 Salim: “nilidhani sitakuona tena sijakuona muda mrefu”Uk.42 “oh huwezi kuamini jinsi tulivyojaribu”.
  • Nafsi ya pili:Salim : usifurahi kupita kiasiSalim: hufai kuhukumu unalala kama…..Mama Furaha: usiwe hivyo wewe u mtoto mzuri.
  • Nafsi ya tatu:Mama Furaha: kabla Furaha hajafa alitaka niahidi kumfanyia kitu fulani hapa kwenye mazishi ingawaje alikuwa na maumivu na mateso aliandika barua hii hapa na kunipa.
MATUMIZI YA LUGHA
Lugha aliyotumia mwandishi ni lugha fasaha na inayoleweka kwa wasomaji wake.
Matumizi ya tamathali za semi
  • Sitiari:Uk.2 “Waridi changa” “Ua kavu” –Mama anamfananisha Furaha na waridi au ua.Uk.4 “Nyie Mbu mlolaaniwa” –Baba Furaha anawaita wadogo zake Furaha;Uk.6 “Ua” –Furaha.Uk.25 “Slim”- UKIMWI. Wanakijiji wanaufananisha ugonjwa huu na jina hili kutokana na sifa yake ya kukondesha mwili.
  • Tashibiha:Uk.18 “yeye ni kama Punda wa kijiji”.Mwanakijiji wa 1 anamfananisha Furaha na Punda kutokana na tabia yake ya kuwa na wanume wengi. Malaya.Uk.13. “kisura ni kama jiji la New York…”Uk.43 “…vipande vinaanguka kama theluji”.
  • Mubaalagha:Uk.13 “kisura ni kama Jiji la New York ya Afrika Mashariki. Kule kuna majengoMajengo makubwa kiasi kwamba unaweza kuona mlima Kilimanjaro kwaJuu” pia anasema“Ndiyo mpenzi na Maduka… wana moja linaloitwaShoppers Plaza…! Pengine ndilo eneo kubwa lenye maduka makubwaKuliko yote katika Afrika”Uk.20 Furaha: nani aliyesema mambo hayo?Mama Furaha: Nusu ya kijiji kizima badala ya watu wengi. Mama Furahaanazidisha chumvi Kuonesha ukubwa wa hilo jambo.
  • Tafsida:Uk.7 maongezi kati ya wahusika;Mary: hiyo ni bia yake ya mwanzo.Furaha: ni chunguMary: ladha yake utaizoea tuBw. Juma: kama ulivyizoea wewe mayai yangu madogo!Bw. Ecko: Unaona! Inashangaza jinsi ambavyo mtu unaizoea haraka ladha hiyo!Bw. Juma:(kwa mary) kama ulivyofaanya wewe, mishikaki yangu midogo….Mazungumzo haya yamepunguza ukali wa maneno, maneno kama vile “Mishikaki” na “Mayai” ni sehemu za siri.
Mbinu nyingine za kisanaa
  • Mdokezo:Uk.8 “ndiyo padre….. ni …..”Uk.9 “Furaha…..fur….tuta…..”Uk.20 “ame…..tuseme…..”Uk.36 “misamaha padre mi…”Uk.44 “uepukaji….”
  • Nidaa:Uk.15 “Ooo!”Uk.34 “Oh!”Uk.41 “Eee”
  • Takriri:Uk.28 “Hapana hapana hapana nitauona!” “mpumbavu mpumbavu mimi”Uk.9 “hili ni jambo zito sana… sanasana…..sana hasa…”Uk 44 na 45 maneno haya yamerudiwa kuonesha msisitizo.Mwanakijiji wa 2: kondomMwanakijiji wa 3: elimuMwanakijiji wa 4: elimuMwanakijiji wa 1: uwaziKitunda: uadilifuPadre James: ukweliMary: upendoSalim: msamaha.
  • Tashtiti:Uk.20 mama Furaha: wewe na marafiki zako wa kiumeFuraha: marafiki gani wa kiume?Furaha anauliza swali ambalo majibu yake anayo ila tu anataka kuupindisha ukweli.Uk.38 baba: msalaba wako, padri. Uko shingoni mwako!Padre James: kweli?Baba: padre!Padre James: hakika?Padre James alijua wazi kuwa msalaba ulikuwa shingoni lakini kutokana na kutaka kuuficha ukweli alipokutwa katika pilika za kutafuta barua na kusingizia amedondosha msalaba. Alijifanya kuuliza kama vile hajui.
  • Onomatopea au tanakali sauti:Uk.33-34 “Myaau!” Uk.35 “Oooowww!”
Matumizi ya semi
  • Misemo:Uk.27 “Furaha anavuna mbegu ya kifo aliyopanda”
WAHUSIKA
FURAHA
  • Ni binti mdogo wa miaka kati ya 13-19
  • Ni Malaya
  • Anaathirika kwa ugonjwa wa UKIMWI
  • Alikuwa na bidii na mwenye kujituma
  • Ana tama
  • Ni mlevi
  • Ni mkweli na muwazi
  • Ni jasiri
BABA
  • Ni baba yake Furaha
  • Ni mkali
  • Ana upendo
MAMA FURAHA
  • Ni mama yake Furaha
  • Ni mkweli na muwazi
  • Ana upendo
  • Ni jasiri
  • Ni mchapakazi
  • Ni mpole
  • Ana msimamo
  • Anafaa kuigwa na jami
MARY
  • Ni binti mdogo
  • Ni Malaya
  • Si rafiki mwema
  • Anachangia kuharibu maisha ya Furaha
  • Ni mlevi
  • Anapenda anasa
  • Ana tama
  • Hafai kuigwa na jamii

BW. ECKO
  • Ni mwanaume mtu mzima
  • Ni Malaya
  • Si muaminifu katika ndoa yake
  • Ni mrubinifu kwa mabinti wadogo
  • Ni mlevi
  • Ni mfanyabiashara
  • Ni muathirika wa UKIMWI
JUMA
  • Ni mwanaume mtu mzima
  • Ni Malaya
  • Ni laghai kwa mabinti wadogo
  • Ni mlevi
  • Anapenda anasa
  • Ana tama
  • Ni rafiki wa Bw. Ecko
PADRI JAMES
  • Ni mtumishi wa Mungu katika kanisa katoliki
  • Si muadilifu
  • Anaogopa ukweli na uwazi
  • Ni dhaifu kwa wanawake
  • Anaweza kuwa ni muathirika wa UKIMWI
KITUNDA
  • Ni kijana wa mtaani
  • Anapenda anasa
  • Ana tama
  • Ni mlaghai kwa wasichana
  • Ni muhuni
  • Ni mlevi na mvuta bangi
  • Ana lugha ya kihuni
SALIM
  • Ni kijana wa kiume
  • Ni msomi
  • Ni mchumba wa Furaha
  • Anaweza kuwa ni muathirika wa UKIMWI
  • Si mkweli na muwazi
  • Si muadilifu
  • Wanakijiji 1,2 na 3
  • Ni wanakijiji katika kijiji cha Furaha
  • Hawana elimu juu ya UKIMWI
  • Ni wambea
  • Wana imani potofu
DADA MDOGO
  • Ni mdogo wake Furaha
  • Ana tabia njema
  • Ni mkweli lakini muoga
  • Hapendezwi na tabia ya dada yake
MANDHARI
Mandhari aliyotumia mwandishi ni ya vijiji vya Afrika Mashariki kwa ujumla wake. Mwandishi ametumia mandhari hii makusudi kwani imeendana na yale anayoyazungumza katika kitabu. Suala la ujinga na upotofu wa dhana kuhusu UKIMWI lipo zaidi vijijini. Wanakijiji hawaelewi juu ya UKIMWI. Mambo anayoyaibua mwandishi yanaendana na jamii ya watu wa vijiji hivyo mandhari ni sadifu.
Fani katika Tamthiliya ya Watoto wa Mama N’tiliye
Hakaiki fani katika tamthiliya ya Watoto wa Mama N’tiliye
MWANDISHI: EMMANUEL MBOGO
WACHAPISHAJI: HEKO PUBLISHERS
MWAKA: 2002
JINA LA KITABU
Jina la kitabu WATOTO WA MAMA NTILIE limesadifu yaliyomo ndani ya kitabu, kinaeleza kuhusu maisha ya watoto wa mama ntilie. Maisha ya dhiki, umaskini uliokithiri, maisha yasiyo ya faraja yaliyokosa malezi bora, chakula bora, elimu, huduma ya afya nk. Jina la kitabu linaakisi yaliyomo ndani ya kitabu na katika jamii yetu ya leo kwani akina mama wengi hawana kazi nzuri za kuwaingizia kipato kikubwa na bado wanategemewa katika malezi. Mwandishi ametumia jina hili ili kibua kero na matatizo yaliyoko katika jamii.
UTANGULIZI WA KITABU
Riwaya ya Watoto wa Mama N’tilie ni riwaya ambayo inasadifu maisha ya Mtanzania wa leo. Inaangazia suala la umaskini na hali ngumu ya maisha, wimbi la watoto wa mitaani, masuala ya uhalifu wizi na ujambazi, malezi nk. Mwandishi Mbogo amejitahidi sana. Pia katika fani ametumia muundo na mtindo wenye kuwavutia wasomaji pia kawaumba wahusika wake kwa usadifu wa hali ya juu huku mandhari yake ikiwa ni halisi inayosawiri maisha ya Tanzania.
MUUNDO
Muundo uliotawala katika riwaya hii ni muundo wa rukia au rejea. Mfano sura ya tatu mwandishi anatuelezea juu ya safari ya Mama ntilie kwenda matombo uk.34. Lakini anaacha kisa hicho ndani ya sura hiyohiyo anaanza kutuelezea juu ya kuzaliwa kwa watoto Kurwa na Doto na asili yao. Pia uk.80 mwandishi anatudokeza juu ya safari ya kwenda kwa Musa na hatuoneshi hatma ya safari yake bali anarukia kisa kingine na kuanza kutuelezea juu ya Zita kupandwa na kichaa uk.81. Vilevile uk.85-86 anatusimulia juu ya safari ya Mama Zita na Zenabu kuelekea hospitali kumwona Zita lakini hatuoneshi hatma ya safari yao bali anarukia kisa kingine na kuturudisha nyumbani kwa Mzee Lomolomo na jinsi anavyofakamia pombe alafu anaturudisha tena kutuambia juu ya kifo cha Zita hospitalini Muhimbili.
Mwandishi amegawa visa na matukio katika sura tano. Sura hizi zimejengwa katika muundo unaotegemeana ili kukamilisha kilele cha masimulizi.
MTINDO
Mtindo aliotumia mwandishi ni wa masimulizi ya mjazo au lugha ya nathari ameeleza visa mwenyewe na vingine wahusika wamevielezea. Pia ametumia mitindo kadha wa kadha. Mfano;Matumizi ya nafsi.
  • Nafsi ya tatu wingi na umoja:Uk.15 “Peter aliokota kipande cha muhogo” “alisafisha kipande cha muhogo”Uk.27 “walisaidiana wakaubeba” uk.26 “watu walisongamana walisukumana…..”.Kwa kiasi kikubwa matumizi ya nafsi ya tatu ndiyo yaliyotawala.
  • Nafsi ya kwanza umoja na wingi:Uk.58 “nitasema nitasema!”Uk.58 “njoo tuongee”Uk.56 “twende tule”.
  • Matumizi ya nafsi ya pili au dayalojia:Uk.89 pale Mama ntilie alipokumbuka majibizano yake na Zita.MAMA NTILIE: na hiyo nguo namna gani? Mbona chafu hivyo na leo ndio kwanza.Jumanne.PETER: mbwa Mama……ZITA: amenikwaruza kidogo na makucha yake.
  • Matumizi ya tanzu nyingine za kifasihi, mfano wimbo;Uk.78 “Jua ni moto,Tena ni mwangazaWa Dunia,Nadina yooNadina mama,Tumwombe Mungu Baba”Uk.10 wimbo alouimba mzee Lomolomo. “Kuleni nae,Hata bangi vuteni nae,Lakini ni kazi bure,Mwenzenu nimezaa naye,Pepepe kijani cha mbaazi,Kijaluba na msondoKiboko yao”.
Hivyo mwandishi ametumia mitindo hiyo ili kutomchosha msomaji mfano wimbo unamburudisha msomaji, majibizano yanavuta umakini zaidi na matumizi ya nafsi mbalimbali.
MATUMIZI YA LUGHA
Riwaya ya Watoto wa Mama Ntilie imetumia lugha rahisi, fasaha na inayoeleweka kwa wasomaji. Kuna matumizi ya lugha ya kiingereza mfano.Uk.36 “chloroquine”, “RosewinenaQueenElizabeth”,Uk.83 “faster faster mama” uk.1 “landrover”. Pia kuna matumizi ya lugha ya miitaaniuk.41 “kudeku…..”
Matumizi ya tamathali za semi
  • Tashibiha:uk.10 “mdomo wake ulio kaa kama bakuli la pombe”Uk.12 “mama ntilie alikaa kama kapigwa na radi”Uk.15 “miguu kama ya mamba”Uk.46 “aliinamisha shingo nayo ikapinda kama mforosadi” “kichwa kama stafeli”Uk.40. “kitovu chake kama jicho chongo”Uk.23 “Kurwa aliruka nyuma kama Chui”Uk.45 “akaruka kama Paa”
  • Tashihisi:Uk. 10 “mabega yenyewe tayari yalikuwa yamechongwa kwa pombe ya gongo.Yameangalia juu karibu yakutane na masikio”Uk.17 “aliziona nywele za kipilipili za Musa ngumu kama katani hazijaonja maji walasabuni”Uk.19 “ moshi wenye harufu ya kuudhi ulilelea hewani na kumlaki mtoto Peter.”Uk.35 “…… visogo vitatu vilikata kona na kupotea”Uk.46 “koo lilimsaliti”Uk.40 “miguuni raba zinazocheka kwa huzuni”Uk.46 “mlango ule wa kuungwa na gundi ulitika labeka”
  • Sitiari:Uk.10 “Nyama nyie”Uk.86 “…… wakatembea mwendo wa Farasi”
  • Ritifaa:Uk.38 “Mama? Mama yuko wapi, Baba yuko wapi? Mapenzi yao yako wapi?”Uk.92 “Zita! Zita! Zita! Zita umekwenda! Umenitoroka, Zita mwanangu”Uk.93 “Baba! Baba watoto? Mwenzangu! Ee! Amka, simama! Usiniachie tanzia hii peke Yangu”
  • Tafsida:Uk.91 “haja kubwa”
Matumizi ya mbinu nyingine za kisanaa
  • Onomatopea /tanakali sauti:Uk.5 “….. aliupinda mgongo kwa mbele akausikia unalia ka-ka-ka-ka, alitema mate tena Phuuuu”Uk.11 “alikohoa ukho! okho!”Uk.19 “…. Kwa kupiga chafya mbili au tatu Tcha! Tcha! Tcha!”Uk.50 “Bwee! Bwee! Bwee! Mbwa ….”Uk.50 “Hali … vicheko Woo! Woo! Weee! Weee! Heheheee! Leooo!”
  • Takriri:Uk.12 “twende! Twende! Nakuwacha nakauwacha!”Uk.58 “ Nivione! Nivione! Nivione vya kazi gani!”Uk.60 “ Nipishe! Nipishe! Nipishe!Uk.61 “kukurukakara, kukurukakara,kukurkakara”Uk.91 “ Baba! Baba! amka Baba”
  • Mjalizo:Uk. 40 “… akapata pesa, akala, akashiba”
  • Mdokezo:Uk.58 “usiseme hivyo! Unasikia ee! Usi……”Uk.71mara akaanza kuimba tena uleule wimbo wake wa “siwezi kuuwa mtu mama”Uk.73 “lakini…….”Uk.79 “ alikumbuka jaa laa jiji na ………”
  • Nidaa:Uk.44 “ Oh! Mungu wangu!”Uk.91 “ Mama wee!”Uk.90 “Hamadi! Mtume!”
Matumizi ya semi
  • Nahau:Uk.43 “…. Kupiga usingizi”
  • Methali:Uk.34 “ kamba hukatikia pembamba”Uk. 69 “fadhila za Punda”
  • Misemo:Uk.35 “ mtu wa maji” – mlevi.Uk.13 “kwake pombe ya mataputapu na gongo alivifanya dini”.
Matumizi ya taswira
  • Taswira mwonekano mfano:Uk.1 “ Mbwa huyu mweusi mwenye mkia mweupe, alionekana akitembea mwendo wa polepole. Ulimi wake mrefu ulionekana ukidondoka mate ya utelezi” hii inatufanya tupate picha halisi ya jinsi Mbwa huyo alivyo kupitia maneno ya msanii”.Uk.5 “….. hatua tatu mbele yake Sufuria, Vikombe na Sahani chafu zilizagaa pale nje zikimtazama. Akawaona nzi wakitembea na kurukaruka juu ya vyombo vichafu.Uk.10 “ mabega yenyewe tayari yalikuwa yamechonngoka kwa pombe ya gongo yameangalia juu karibu yakutane na masikio.”Uk.69 “Zenabu alibaki pale mlangoni kavaa gauni aina ya shifti, kitambaa cha Hariri”
  • Taswira hisi:Uk.91 “ Mzee Lomolomo alilala mdomo wazi Nzi wakubwa wa kijani kibichi wamejaa tele mdomoni mwake”.Hii inamfanya msomaji ajisikie kinyaa kutokana na hali hiyo ya Mzee Lomolomo anaposema nzi wa kijani kibichi, kwani hao ni nzi wanaokaa sana chooni na kwenye uchafu.
WAHUSIKA
Mama Ntilie
  • Ni mama mzazi wa Peter na Zita
  • Ni mke wa Mzee Lomolomo
  • Mlezi mzuri wa familia
  • Ni mvumilivu sana
  • Ana huruma
  • Ni mchapakazi na anayejituma
  • Ana hali ngumu kimaisha
Mzee Lomolomo
  • Ni mme wa mama ntilie
  • Baba wa Peter na Zita
  • Mlevi
  • Mvivu
  • Si mlezi bora hajali familia
  • Anakufa kwa sababu ya kunywa sana pombe
Peter
  • Mtoto wa mama ntilie
  • Anakosa elimu kwa sababu ya umaskini
  • Ana bidii na mchapakazi
  • Ana huruma
  • Anafungwa jela sababu ya kufanya biashara haramu ya madawa ya kulevya
Zita
  • Mtoto wa kike wa mama ntilie
  • Anakosa elimu sababu ya umaskini
  • Ni mchapakazi
  • Anagombana na Kurwa hakupenda aje kwao, roho mbaya
  • Anakufa kwa ugonjwa wa kichaa cha mbwa
Doto
  • Ni mtoto yatima
  • Mtoto wa mtaani
  • Doto anauawa baada ya kujiingiza katika uhalifu wa wizi
  • Ni mgomvi na katili
Kurwa
  • Ni ndugu yake Doto
  • Anaishi mtaani
  • Ni yatima
  • Ana huruma
  • Ana nguvu na jasiri
  • Ni mchapakazi
  • Anaishia jela kwa sababu ya makosa ya Musa na Peter
Musa
  • Ni mtoto aliyekosa elimu baada ya kukosa sare na ada
  • Alikosa malezi mazuri ya wazazi
  • Mhalifu, anafanya biashara haramu za madawa ya kulevya
  • Ana tamaa ya pesa
  • Ni rafiki mbaya kwani alimshauri Peter kuuza madawa ya kulevya
Mwalimu Chikoya
  • Ni mwalimu wa akina Peter na Zita
  • Aliwafukuza Peter na Zita shule sababu ya kukosa ada
  • Si mwalimu mzuri
MANDHARI
Mandhari iliyotumika katika riwaya hii ni mandhari ya jiji la Dar es Salaam. Hii ni kutokana na kutajwa kwa maeneo ya jiji mfano, Manzese, Tabata, Kiwanda cha Urafiki, Kisutu, Muhimbili nk. Pia ametumia mandhari ya nyumbani mfano nyumbani kwa Mama Ntilie uk.5, mandhari ya hospitali ya Muhimbili uk.89, mandhari ya jaani-jaa la Tabata uk.20.
Kwa hiyo mwandishi ametumia mandhari inayosadifu aliyoyaeleza anaibua dhamira halisi zinazosawiri maisha ya Mtanzania wa leo kwa mandhari hiyo mfano suala la umaskini na wimbi la watoto wa mitaani.

Fani katika Ushairi wa Wasakatonge
Hakiki fani katika Ushairi wa Wasakatonge
MWANDISHI: TAASISI YA KISWAHILI, ZANZIBAR
WACHAPISHAJI: OXFORD UNIVERSITY PRESS
MWAKA: 2001
JINA LA KITABU
Jina la kitabu linasadifu yaliyomo katika kitabu. Kwa upande wa maudhui mambo yanayoelezwa mengi yanaigusa jamii ya sasa. Masuala ya maadili, siasa, uchumi, ukombozi wa kiutamaduni changamoto na suluhisho ya matatizo yanayoikumba jamii yanaendana na wakati wa sasa. Hivyo upya wa malenga wapya ni kweli. Kifani pia Malenga wapya wameweka muundo na mtindo wa kisasa.
MUUNDO
Tunapohakiki muundo katika ushairi tunaangalia idadi ya mistari katika ubeti. Ubeti huweza kuwa na mistari miwili, mitatu, minne na kuendelea. Aina za muundo zimepewa istilahi maalum kuutofautisha aina moja na nyingine mfano mashiri yenye mistari miwili katika ubeti ni Tathnia. Imetumika miundo tofautitofauti katika diwani hii. Mfano:
  • Tathlitha:Haya ni mashairi ambayo yana mistari mitatu kwa kila beti, mengi ya mashairi haya ni ya kisasa. Mfano ni shairi la“Hali halisi”, “Puuzo”, “Ua”, “Kuunge”, “Tunzo”.Shairi la Ua.“Ua limejituliza mtini laning’inia,Mwenyewe laniliwaza, furahani lanitia, Ua sasa limepea, macho walikodolea.”
  • Tarbia:Haya ni mashairi yenye mistari mine. Mfano ni shairi la“Kitendawili”, “Mkulima”, “Majonzi”, “Bahari”, “Samaki mtungoni” “Kifungo”,na mengine mengi.Shairi la“Kifungo.” “Miaka imeshapita, sasa najiamkia,Naanza bila kusita, bahati kujitafutia,Hapo nitapoipata, mola jishukuria,Kifungo kimenichosha, minyororo nafungua.
  • Takhmisa:Haya huwa na muundo wa mistari mitano katika kila ubeti. Mfano ni mashairi ya“Siharakie maisha”, na “Israfu”.Shairi la“Israfu”. “Mali ulojichumia,Ni yako nakubalia,Lakini kiangalia,Vipi unaitumia,Mwenzangu nakuusia israfu haifai.”
  • Sabilia:Haya ni mashairi yenye mistari kuanzia sita na kuendelea. Mfano ni shairi la“Punda”na “Pasua uwape ukweli”.Shairi la“Punda”. “Toka ulipozaliwa, maishayo ni kizogo,Hujapata kuenziwa, waishi tiriigivyogo,Nawe hujajielewa, u kiumbe hu kigogo,Kama ungefadhiliwa, usingebeba mzigo, Hakika ulionewa, hustahili kipigo,Haki umeitambua, idadi japo kidogo.”
MTINDO
Imetumika mitindo ya aina zote mbili. Kwanza wametumia mtindo wa kisasa. Huu ni mtindo ambao haufuati kanuni za urari wa vina na mizani katika beti pia huitwa mashairi huru. Mtindo mwingine ni mtindo wa kimapokeo, huu hufuata kanuni na sheria zote za vina na mizani katika utunzi wake. Mara nyingi huwa na mistari minne katika kila ubeti.
Mfano wa mashairi yaliyotumia mtindo wa kisasa ni mashairi ya“Pasua uwape ukweli”, “Haki” “Payuka
Pia mfano wa mashairi ya kimapokeo ni shairi la“Mkulima”, “Bahari”, “Tuyazingatie haya” “Nipate wapi mwingine”.
MATUMIZI YA LUGHA
Diwani ya malenga wapya imetumia lugha yenye ubunifu bora wa kisanaa.Vilevile ni lugha rahisi na sanifu inayoeleweka kwa hadhira lengwa.
Tamathali za Semi
  • Tashibiha:“Nizikwe kama wezangu, nisitupwe kama paka” -Shairi la“Nini wanangu”.“Hata pamoja muweko, ubaguzi umezama,kama nguzo” -Shairi la“Tunzo ubeti wa nne”.“Mfanowe kama radi, chini inapoanguka”.-Shairi la“Nipate wapi mwingine”.“Nikabaki kama ng’onda” -Shairi la“Nipatieni dawa”.“Maisha ni kama njia”-Shairi la“Maisha ni kama njia”.“Yameotewa na kombe, mithili gome la mti”-Shairi la“Bahari ubeti wa pili”.
  • Tashihisi:“Ewe ulimi sikia” -Shairi la“Ulimi”.“Haki wa tutisha,tusikuandame,kwa matendo yetu” –Shairi la“Haki ubeti wa kwanza”.“Njiwa ameishanitoka, nipate wapi mwingine”-Shairi la“Nipate wapi mwingine”.“Samaki wasikitika, kudai walikotoka, Wote wamekasirika, uhuru wanachotaka,”-Shairi la“samaki mtungoni”.
  • Sitiari:“wamejipa uwezo wa Rabuka” – “Mpaka lini”“Paka shume jigeuza” – “Kwanini?”“mshumaa ” – “Hali halisi”
Mbinu nyingine za kisanaa
  • Onomatopea/ tanakali sauti:“kokoriko”- “Mkulima”“Parakacha” – “kwanini”.
  • Takriri:“Charuka” – “charuka”
  • Tashititi:“Nasikia mnatunga mwatungani washairi?” “mwabwaja mwasema nini”
Matumizi ya semi
  • Methali:“Simwamshe asilani aliyelala usingizini” – “Payuka”“Fahali wapiganapo, nyasi ndio huumia”- “Sokomoko baharini”“Subira yavuta heri”- “Siharakie maisha”
Matumizi ya taswira
  • “Samaki” – wanyonge – “samaki mtungoni”
  • “Ua” – mpenzi – “Ua”
  • “Punda”-wanyonge – “Punda”
  • “Mvuvi” – wanyonyaji – “Samaki mtungoni”
  • “Njiwa” – mpenzi – “Nipate wapi mwingine”
  • “Baharini” – nchi – “Sokomoko”
  • “Abiria”- wananchi –“Sokomoko”
Fani katika Ushairi wa Mashairi ya Chekacheka
Hakiki fani katika Ushairi wa Mashairi ya Chekacheka
MWANDISHI: THEOBALD A. MVUNGI
WACHAPISHAJI: EDUCATIONAL PUBLISHERS AND DISTRIBUTORS LTD.
MWAKA: 1995
MUUNDO
Mwandishi ametumia muundo wa tarbia, mashairi yake yote yamefuata muundo huu. Beti za mashairi yake zina mistari minne. Mengi ya mashairi yake, mistari imegawanyika katika vipande viwili yaani mistari ina vina vya kati na vya mwisho. Mfano katika shairi la “Mashairi ya “Ngulu”;
Pia katika baadhi ya mashairi yake ameyaumba katika kipande kimoja, yaani yana kina cha mwisho tu. Mfano ni mashairi kama vile ya“Dhahabu ya fahari”, “Utu umekuwa kima”,“Seng’enge”mfano katika shairi la“Utu umekuwa kima”
MTINDO
Mtindo aliotumia mwandishi ni mtindo wa kimapokeo kwani amezingatia vigezo vya vina na mizani katika utunzi wa mashairi yake. Mfano katika shairi la”“Tuambae ukasuku”
MATUMIZI YA LUGHA
  • Tashibiha:“Mshairi jihadhari, usishikwe kama fimbo.” – “Tuambae ukasuku.”“Na wasiothaminiwa, wapimwao kama nyasi”- “Raia si mali kitu”“Mapenzi yasinadiwe, kama shati dukani” – “Penzi lisilo heshima”“Utaliwa kama pumba” – “Utaliwa kama pumba”“Kaburu si mtu hata, kwake sisi sawa punda” – “Utumwa huru”.“Pungufu akili yake, mla punje kama kuku” – “Tuambaeukasuku
  • Tashihisi:“Mejaribu kujongea, ndege awe mkononi,Yeye juu hurukia, namuomba samahani.” – “Njiwa kiumbe mtini”“Moyo nimeshauri, lakini umekaidiMoyo kiburi hatari, mfanowe kama radiMoyo mefumbata shari, unayakwepa marudi,Moyo u mwilini mwangu, jirudi tuwe pamoja.” – “Moyo”Nipishe wewe senge’nge” – “Seng’enge”.“Kijiji kisichoringa” – “Mashairi ya Ngulu”.“Akili yamsaliti, kikongwe haoni kweli.”- “ Ni wapi ushauri?”
  • Sitiari:“Mshairi awe Nyati”- “Tuambae ukasuku”“Sisi ni miamba gogo”- “Raia si mali kitu”“Ile chai kikombeni, rangi yake Mwafrika” – “Chai”.“Kwetu ulikuwa mama” – “Indira”“Utu umekuwa kima” – “Utu umekuwa kima”“Uroho umekujaa, watu mefanya kondoo” – “Utaliwa kama pumba”
Matumizi ya semi
  • Misemo:“Fedha fedheha” – “Chanzo cha huo uozo”
  • Methali:“Akishaoza samaki, busara ni kumtupa” – “Chatu mmeza matonge”
  • Nahau:“Wabunge waote meno, wasivilambe viatu” –wawe na mamlaka– “Tuambae ukasuku”Mbinu nyingine za kisanaa
  • Takriri:“Chai ninaipa hati, kwa kutukidhia haja,Chai imewekwa kati, kwetu sisi sote waja,Chai majani ya miti, hii miti yenye tija.” – “Chai”Neno“njiwa” limejirudia katika kila ubeti –“Njiwa”Neno “moyo” limerudiwa katika kila ubeti. – “Moyo”Neno “mauti” limejirudia katika ubeti wa kwanza – “Utaliwakamapumba”Neno “Ngulu” katika mashairi ya “Ngulu”.
Ujenzi wa Taswira
Matonge”- madaraka-“Mwinyi umewasha moto”Nyati”– watawala –“Tuambae ukasuku”“Mfugaji”– mwananchi – “Tuambae ukasuku”“Jiko”– madaraka “Kuna nini huko jikoni”“Chatu”– watawala –“Chatu mmeza matonge”“Chura”– mtu asiye na msimamo - “Chura umegundulika”
Fani katika Ushairi wa Malenga Wapya
Hakiki Fani katika Ushairi wa Malenga Wapya
MWANDISHI: TAASISI YA KISWAHILI, ZANZIBAR
WACHAPISHAJI: OXFORD UNIVERSITY PRESS
MWAKA: 2001
JINA LA KITABU
Jina la kitabu linasadifu yaliyomo katika kitabu. Kwa upande wa maudhui mambo yanayoelezwa mengi yanaigusa jamii ya sasa. Masuala ya maadili, siasa, uchumi, ukombozi wa kiutamaduni changamoto na suluhisho ya matatizo yanayoikumba jamii yanaendana na wakati wa sasa. Hivyo upya wa malenga wapya ni kweli. Kifani pia Malenga wapya wameweka muundo na mtindo wa kisasa.
MUUNDO
Tunapohakiki muundo katika ushairi tunaangalia idadi ya mistari katika ubeti. Ubeti huweza kuwa na mistari miwili, mitatu, minne na kuendelea. Aina za muundo zimepewa istilahi maalum kuutofautisha aina moja na nyingine mfano mashiri yenye mistari miwili katika ubeti ni Tathnia. Imetumika miundo tofautitofauti katika diwani hii. Mfano:
Tathlitha
Haya ni mashairi ambayo yana mistari mitatu kwa kila beti, mengi ya mashairi haya ni ya kisasa. Mfano ni shairi la“Hali halisi”, “Puuzo”, “Ua”, “Kuunge”, “Tunzo”.
Tarbia
Haya ni mashairi yenye mistari mine. Mfano ni shairi la“Kitendawili”, “Mkulima”, “Majonzi”, “Bahari”, “Samaki mtungoni” “Kifungo”,na mengine mengi.
Takhmisa
Haya huwa na muundo wa mistari mitano katika kila ubeti. Mfano ni mashairi ya“Siharakie maisha”, na “Israfu”.
Sabilia
Haya ni mashairi yenye mistari kuanzia sita na kuendelea. Mfano ni shairi la“Punda”na “Pasua uwape ukweli”
MTINDO
Imetumika mitindo ya aina zote mbili. Kwanza wametumia mtindo wa kisasa. Huu ni mtindo ambao haufuati kanuni za urari wa vina na mizani katika beti pia huitwa mashairi huru. Mtindo mwingine ni mtindo wa kimapokeo, huu hufuata kanuni na sheria zote za vina na mizani katika utunzi wake. Mara nyingi huwa na mistari minne katika kila ubeti.
Mfano wa mashairi yaliyotumia mtindo wa kisasa ni mashairi ya“Pasua uwape ukweli”, “Haki”. “Payuka”. Mfano shairi la Pasua uwape ukweli
Pia mfano wa mashairi ya kimapokeo ni shairi la“Mkulima”, “Bahari”, “Tuyazingatie haya” “Nipate wapi mwingine”.
MATUMIZI YA LUGHA
Diwani ya malenga wapya imetumia lugha yenye ubunifu bora wa kisanaa.Vilevile ni lugha rahisi na sanifu inayoeleweka kwa hadhira lengwa.
TAMATHALI ZA SEMI
  • Tashibiha:“Nizikwe kama wezangu, nisitupwe kama paka” -Shairi la“Nini wanangu”.“Hata pamoja muweko, ubaguzi umezama,kama nguzo” -Shairi la“Tunzo ubeti wa nne”.“Mfanowe kama radi, chini inapoanguka”.-Shairi la“Nipate wapi mwingine”.“Nikabaki kama ng’onda” -Shairi la“Nipatieni dawa”.“Maisha ni kama njia”-Shairi la“Maisha ni kama njia”.“Yameotewa na kombe, mithili gome la mti”-Shairi la“Bahari ubeti wa pili”.
  • Tashihisi:“Ewe ulimi sikia” -Shairi la“Ulimi”.“Haki wa tutisha,tusikuandame,kwa matendo yetu” –Shairi la“Haki ubeti wa kwanza”.“Njiwa ameishanitoka, nipate wapi mwingine”-Shairi la“Nipate wapi mwingine”.“Samaki wasikitika, kudai walikotoka, Wote wamekasirika, uhuru wanachotaka,”-Shairi la“samaki mtungoni”.
  • Sitiari:“wamejipa uwezo wa Rabuka” – “Mpaka lini”“Paka shume jigeuza” – “Kwanini?”“mshumaa ” – “Hali halisi”Mbinu nyingine za kisanaa.
  • Onomatopea/ tanakali sauti:“kokoriko”- “Mkulima”“Parakacha” – “kwanini”.
  • Takriri:“Charuka” – “charuka”
  • Tashititi:“Nasikia mnatunga mwatungani washairi?” “mwabwaja mwasema nini”Matumizi ya semi
  • Methali:“Simwamshe asilani aliyelala usingizini” – “Payuka”“Fahali wapiganapo, nyasi ndio huumia”- “Sokomoko baharini”“Subira yavuta heri”- “Siharakie maisha”
  • Taswira:Matumizi ya taswira“Samaki” – wanyonge – “samaki mtungoni”“Ua” – mpenzi – “Ua”“Punda”-wanyonge – “Punda”“Mvuvi” – wanyonyaji – “Samaki mtungoni”“Njiwa” – mpenzi – “Nipate wapi mwingine”“Baharini” – nchi – “Sokomoko”;“Abiria”- wananchi –“Sokomoko”

Maudhui katika riwaya ya Takadini
Hakiki Maudhui katika riwaya ya Takadini
DHAMIRA
  • Suala la imani potofu na ushirikina:Wanakijiji wa kijiji cha Sekai na wanakijiji wa kijiji cha Mtemi Makwati, wana imani potofu juu ya binadamu aliye na ulemavu wa ngozi yaani albino “sope” wanaamini kuwa kuzaliwa kwa mtoto wa aina hiyo ni laana na hapaswi kabisa kuishi. Hawaamini kuwa ni binadamu wa kawaida. Mfano uk.8Ambuya Shungu anasema“mtoto ni Musope.Ni wajibu wetu kumuharibu”.Mwandishi amelionesha suala hili makusudi ili jamii iweze kupinga na kuacha mila hizi potofu mara moja! Anaiasa jamii kuwapenda, kuwajali na kuwasaidia watu wenye ulemavu wa ngozi na si hivyo tu bali pia anaona upo umuhimu wa jamii kuwapa nafasi watu wa aina hiyo kwani wanaweza kuwa na umuhimu mkubwa na mchango katika jamii.
  • Ubaguzi kwa watu wenye ulemavu:Hii ni dhamira nyingine ambayo imejadiliwa ndani ya riwaya hii. Mwandishi anaonesha kuwa ubaguzi si mzuri kwani huwafanya watu wenye ulemavu wa ngozi wajisikie vibaya na kujiona si sehemu ya jamii wanayoishi. Tunaona jinsi Nhamoalivyombagua nakumtenga Takadini, uk. 62 “huwezi kukimbia na huwezi kupigana…..tena hata huoni vizuri. Ha! Wala hufanani hata na mmoja kati yetu, watu wanasema una laana, sitaki kuwa rafiki yako....anaendeleakumwambia“wewe ni sope, sope, sope!”kumbe tunapaswa kuwapenda na kuwajali watu wote bila ubaguzi.
  • Ndoa za mitara:Wanaume wa kijiji cha Sekai wana desturi ya kuoa mke zaidi ya mmoja. Mfano Makwati alikuwa na wake wanne ambao ni Sekai, Pindai, Dadirai na Rumbdzai. Wake hawa si wote walipendana bali walijitenga na kuoneana wivu mfano Dadirai na Rumbdzai hawakumpenda kabisa Sekai walimsimanga na kumsengenya. Mfano uk.15 Dadirai alisema kwa chuki “lazima atimuliwe hapa…. arudi kwao” “Ha! Atimuliwe tena? Ni mchawi!”hivyotunaona kuwa ndoa za mitara ni tatizo katika jamii kwani huweza kusababisha migogoro na ugomvi tena huweza kusababisha hata kuambukizana magonjwa hatari hasa katika kizazi cha leo ambapo magonjwa ni mengi ya hatari.
  • Mapenzi ya dhati na huruma:Mzee Chivero ni mzee aliyeonesha mapenzi ya dhati kwa Sekai na mwanae kwani aliwapokea na kuishi nao, pamoja na hali waliyokuwa nayo bila kuwabagua. Alimhurumia Takadini akampenda, kumsaidia na kumshauri vyema siku zote. Pia tunaona Sekai alikuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanae Takadini kwani aliweza kumkinga na kumuokoa asiuawe. Mfano uk.10 Sekai anasema“hapana Ambuya mtoto lazima aishi. Hapana Ambuya mtoto ni wangu na sitamwachia mtu”…… sitamwachia mtu yeyote mwanangu”.
Nafasi ya mwanamke
Mwanamke amechorwa katika nafasi mbalimbali katika riwaya hii kukamilisha ujumbe wa mwandishi kwa jamii kuhusu wanawake.
  • Mwanamke amechorwa kama kiumbe jasiri: Sekai ameonekana kuwa na ujasiri wa hali ya juu kwani aliamua kupingana na mila za jamii yake na kuamua kutoroka na kitoto bila kujua alipoelekea ili tu kumuokoa mwanae. Hivo anapaswa kuigwa na jamii.
  • Amechorwa kama mwanamapinduzi:Sekai na Shingai wamechorwa kama wanawake wanamapinduzi kwa kuubadilisha mtazamo wa wanajamii wenzao kuhusu baadhi ya mila potofu. Mfano Shingai aliamua kuolewa na Takadini bila kujali ulemavu wake. Hakuogopa wazazi wake wala hakuogopwa kutengwa na ndipo badae jamii ilimkubali. Pia Sekai ni mwanamapinduzi kwa kuzikataa mila potofu ya kuwaua albino, alimtunza mwanae na kumlea mapaka akakua.
  • Amechorwa kama chombo cha starehe: Mwanamke katika jamii hizi alionekana kama chombo cha starehe tu kwani waliolewa wanawake wengi kwa mwanaume mmoja na lengo nikumburudisha tu na kumzalia watoto.
  • Amechorwa kama kiumbe dhaifu asiyeweza kusema chochote wala haki yoyote: Wazazi wa Shingai hawakumpa kabisa Shingai uhuru wa kuchagua mwanaume aliyempenda. Walimlazimisha kuolewa na mwanaume waliyemtaka. Mfano uk.118 Shingai anasema“huyu ndiye mtu ninayeteka anioe. Hakuna aliyeniuliza kama nampenda Nhamo. Wewe na baba mlikuwa na hamu ya kuniozesha katika familia ya Manyamombe hata matakwa yangu hayakusikilizwa. Sasa nimechagua”.
  • Amechorwa kama mtu mwenye mapenzi ya dhati: Sekai alikuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanae Takadini. Pia Shingai alikuwa na mapenzi ya dhati kwa Takadini na hata kuamua kuolewa naye.
  • Amechorwa kama mtu mvumilivu: Mfano mzuri ni Sekai alivumilia kwa muda mrefu bila kukata tamaa kukosa uzazi, masimango ya wake wenzake na hatimaye alipata mtoto. Pia alivumilia kumlea Takadini wala hakuthubutu kumtenga hata mara moja bali alimvumilia mpaka alipokua.
MIGOGORO
  • Mgogoro kati ya Sekai na Rumbdzai na Dadirai: Sababu ya mgogoro huu ni kwamba, wanawake hawa wawili hawakumpenda kabisa Sekai na walimuonea wivu kwa kitendo cha kupendwa sana mumewe. Walimsimanga na kumsengenya muda mwingi na hasa kutokana na tatizo la Sekai la kukosa mtoto kwa muda mrefu. Walimwita mchawi.
  • Mgogoro kati ya Sekai na Makwati mumewe:Sababu ya mgogoro huu ni Sekai kujifungua mtoto mwenye ulemavu wa ngozi ambapo katika jamii yao ni laana. Mumewe hakumwamini alimgombeza na kumtishia kumuua akidhani Sekai ni mchawi. Sekai na mwanae anaamua kutoroka ili kuondokana adha ile.
  • Mgogoro kati ya Nhamo na Takadini:Sababuni kuwa Nhamo alimpiga na kumdhalilisha Takadini mara kwa mara mbele ya vijana wengine kwakuwa ni Sope. Alimkejeli na kumdhihaki mfanouk.62 “wewe ni sope umelaaniwa”Nhamo alimwambia Takadini. Pia sababu nyingine ni kutokana na Shingai mchumba wa Nhamo kuwa na mapenzi ya dhati kwa Takadini na kumkataa yeye. Takadini alivumilia na kutolipiza kisasi na baadae alifanikiwa kumuoa Shingai na kuzaa naye mtoto wa kiume.
  • Mgogoro kati ya Nhariswa na mkewe:Nhariswa alimpiga na kumgombeza mkewe kwa kitendo cha kutomfuatilia binti yao na kumwacha aanzishe uhusiano na kijana aliyeaminiwa kuwa amelaaniwa.
  • Mgogoro kati ya Shingai na mama yake:Mgogoro huu ulitokana na Shingai kuamua kuolewa na Takadini jambo ambalo hawakulitaka kabisa kutokana na hali ya Takadini. Mama yake anaamua kumkana Shingai hadharani kuwa si mtoto wake tena.
  • Mgogoro kati ya Nhamo na Tapfumaneyi.Vijana hawa walipigana ili kumtafuta mshindi na shujaa bingwa wa mapigano. Vijana walipigana sawia na walitoka sawia.
  • Mgogoro wa nafsi kwa Sekai.Sekai alisumbuliwa na mgogoro wa nafsi kwa muda mrefu juu ya mwanae ambaye alitengwa na kubezwa kutokana na hali yake. Alilia na kuhuzunika mara nyingi akiilaumu Miungu yao kuwa “Sisi tumefanya nini” hatimaye mgogoro wake uliisha baada ya Takadini kujenga heshima yake upya mara alipomuoa Shingai na kubahatika kupata mtoto wa kiume tena asiye Sope. Na hapo ndipo ilirejea faraja na furaha mpya.
  • Mgogoro wa nafsi kwa Takadini:Huu ulisababishwa na hali yake ya ulemavu wa ngozi iliyopelekea yeye kutengwa na kubaguliwa na wanajamii na mara kadhaa kutishiwa kuuawa. Hali hii ilimtesa ka muda mrefu kwani alitengwa na hakuwa na rafiki toka utotoni hadi ujana wake. Lakini mgogoro huu unaisha baada ya kupata mke aliyempenda kwa dhati na kumzalia mtoto wa kiume. Hii inampa faraja na kujiona mwanaume halisi na kuithibitishia jamii kuwa alikuwa sawa na wanajamii wengine.

  • FALSAFA:Falsafa ya mwandishi Ben Hanson, anaamini kwamba watu wenye ulemavu wa ngozi wana haki ya kuishi kama binadamu wengine kwani wana akili, utashi, uwezo wa kufanya kazi kama binadamu wengine na ni sawa na binadamu wengine.Wao kuwa na ulemavu wa ngozi si kigezo cha kuwaua na kuwabagua. Hana imani juu ya mila potofu kwani katika masimulizi yake anaonesha kushindwa kwa mila potofu kama vile kuamini kuwa albino ni viumbe waliolaaniwa na hawatakiwi kuishi. Anaamini kuwa wakipewa nafasi ya kuishi na kushirikishwa katika shughuli za kijamii, kupewa elimu na mahitaji yote wanaweza kuwa ni watu muhimu sana katika jamii na hili analidhihirisha kupitia Takadini.
  • MTAZAMO:Mtazamo wa mwandishi ni wa kiyakinifu. Tunaweza kusema hivyo kwa sababu ya mambo ambayo mwandishi anayamulika katika kazi yake. Mambo kama vile kuzaliwa kwa albino haoni kuwa ni laana bali ni kawaida tukutokana na masuala tu ya kimaumbile. Haoni kuwa kuna haja ya kuwatenga au kuwabagua albino kwakuwa ni binadamu sawa na sisi.
  • MSIMAMO:Msimamo wa mwandishi ni wa kimapinduzi kwani analenga kuyapindua mawazo na imani potofu za baadhi ya jamii kuwa albino hafai kuishi. Anakemea suala la kuwatenga na kuwabagua albino, anakemea pia suala la ndoa za lazima na mila zingine potofu. Anataka jamii ibadilike na kuendana na wakati kuwapa usawa watu walio na ulemavu wa ngozi, anatetea haki za wanawake anataka wapewe nafasi sawa katika jamii wasibaguliwe. Hivyo msimamo wa mwandishi ni mzuri na unatakiwa kufanyiwa kazi katika jamii.
UJUMBE
  • Albino au watu wenye ulemavu wa ngozi wanatakiwa kupewa haki ya kuishi, kupendwa kusaidiwa na kulindwa.
  • Mila na desturi potofu si budi kupigwa vita katika jamii.
  • Upendo na huruma ni mambo ya msingi katika jamii.
  • Wanawake wapewe uhuru wa kuchagua wanaume wanaowapenda kuishi nao katika ndoa.
  • Wanawake wapewe nafasi na kushirikishwa katika masuala ya jamii.
Maudhui katika Riwaya ya Joka la Mdimu
Hakiki maudhui katika Riwaya ya Joka la Mdimu
DHAMIRA
  • Ugumu na hali ngumu ya maisha:Suala la ugumu wa maisha limejadiliwa katika riwaya hii kwa kiasi chake. Mwandishi ameonesha jinsi wananchi wanavyopata shida ya vyakula, mavazi nk. Yote haya yakisababishwa na mfumuko wa bei za bidhaa kutokana na uhaba wa bidhaa. Mfano. Uk.1“jiji la Mindule lilikabiliwa na uhaba mkubwa mno wa petroli, dezeli na mafuta ya taa nyumba nyingi zisizo na umeme zilibaki kiza usiku maana mishumaa ilikuwa ghali na adimu kupatikana, usafiri ulisimama isipokuwa kwa wale wachache waliojua mbinu za kupata dizeli na petrol”.Mwandishi ameonesha jambo hili ambalo linaakisi maisha ya hali ya kiuchumi miaka ya 80, ambayo kwa upande mwingine inaangazia maisha ya mtanzania wa leo ambapo bidhaa ni nyingi maasokoni lakini tatizo ikiwa ni mfumuko wa bei na upatikanaji mgumu wa fedha.
  • Suala la utabaka:Utabaka uliojadiliwa ni kati ya walionacho na wasionacho (matajiri na maskini). Hili limeoneshwa pale ambapo wananchi wanaishi maisha ya dhiki na makazi duni mfano uk.29 mwandishi anaeleza,“nyumba yenyewe ya Tino ilikuwa bondeni juu tu kidogo ya mtaro mkubwa uliokuwa ukipitisha maji machafu”.Hii inatuonesha wazi hali mbaya ya makazi ya Tino na wakazi wengine, wakati hawa maskini wakiteseka na kuhangaika hata katika suala la huduma za kijamii kama matibabu ya gharama kubwa, matajiri wao walinufaika kwa kuwa na fedha nyingi, mali za kujilikimbikizia na za magendo. Mfano uk. 103 – 104 mwandishi anaeleza kuhusu makazi au nyumba ya Brown“ilisimama na kuzibeza nyumba zote jirani na hapo kwa haiba yake na bwawa lake la kuogelea”.
  • Ufisadi: Suala la ufisadi limeoneshwa na mwandishi kwani amejadili kuhusu viongozi ambao wanahujumu mali za umma kwa maslahi yao binafsi, viongozi mfano wafanyakazi wa serikali kama vile Brown Kwacha amechorwa kuwa ni mtumiaji mbaya wa mali za umma, anasafiri safari za nje kwa pesa nyingi za serikali na kwa matumizi binafsi. Licha ya hivyo anafanya biashara ya magendo na pesa za kigeni katika ofisi yake. Alimudu kujenga nyumba za kifahari kwa pesa za serikali. Mfanouk.102“gharama ya nyumba iliyokuwa ikijengwa na Wafaransa ilikuwa shilingi milioni mia mbili na nusu na ile nyingine milioni mia tatu”.Hizi ni pesa nyingi ambazo zote alizichukua serikalini.Hili ni tatizo kubwa kwa jamii yetu ya leo. Viongozi wetu wa serkali wanatumia pesa vibaya za serikali kwa manufaa binafsi, hivyo kusababisha umaskini usioisha kwa Watanzania wa hali ya chini. Mwandishi amelionesha hili ili wanaohusika wabadilike.
  • Biashara haramu na uharibifu wa mali za taifa:Suala hili limejadiliwa katika riwaya hii. Mhusika Brown ambaye ni mfanyakazi wa serikali anajihusisha na biashara za magendo mfano uuzaji na uwindaji wa wanyama na kuchukua pembe, ngozi na meno. Mfano uk.122-123 muwindaji kinara wa Brown anasema“sawa ziko pembe ishirini za faru na sitini za ndovu, unaweza kuzichukua zote maana vitu hivi ni hatari”.Wanyama muhimu katika hifadhi za taifa wanazidi kupungua na kutoweka kabisa kutokana na biashara hii. Mwandishi ameliangazia ili mamlaka husika na jamii viweze kuweka mikakati na sheria madhubuti za kuangamiza suala hili kwani hupelekea nchi kuendelea kuwa maskini.
  • Rushwa na kutowajibika:Mambo ya hongo na rushwa na kutowajibika kwa viongozi ambao wamepewa mamlaka na wananchi ili wafanye kazi kwa maslahi ya taifa yamejadiliwa. Mfano mhusika Brown si mfanyakazi bora kwani hakutimiza wajibu wake bali alifanya kazi kwa upendeleo mkubwa bila kujali haki. Alipokea rushwa na kutoa pia. Mfano uk.100 anasema“……lakini Brown Kwacha alikuwa mtu wa nyendo akajua karata gani acheze na ipi aibakishe. Alisema kwa kiburi suala si kupata kiwanja ila mahali panapofaa kuporomoshwa kasri la kifahari”. Hivi ndivyo hali ilivyo, wenye uwezo wa kutoa rushwa ndio waliopatiwa huduma haraka. Pia anatuonesha jinsi Brown Kwacha alivyofanya kazi kwa upendeleo uk.97 mwandishi anasema “katibu wa Brown Kwacha alimtazama mkuu wake wa kazi akastaajabia namna alivyoweza kukaidi kuwahudumia wengine ila alivyolainika mbele ya wasichana kama jani la mboga au bufalo ndani ya maji.” Suala hili ni tishio kwa Wananchi kwani hupoteza wa haki, mwandishi anakemea suala hili vikali, na viongozi wanashauriwa kuenenda kwa mujibu wa maadili ya kazi zao.
  • Mapenzi: Mapenzi aliyoyajadili mwandishi katika riwaya hii ni ya sura mbili tofauti.Mapenzi ya dhati;Hili limeoneshwa na mhusika Amani kwa rafikiye Tino, kwani alibeba suala la Tino kuuguliwa na mwanae kama lake, alimsaidia katika shida na raha, hakumuacha peke yake mfano uk.145. mwandishi anasema Tino akawaza“akawaza dunia hii ya leo nani atajitoa kwa hali na mali kumsaidia kapuku kama yeye. Nitamlipa nini Amani?”hii inaonesha fadhila alizokuwa nazo Amani. Pia mapenzi ya dhati yameoneshwa kwa Tino kwa mwanae Cheche na familia yake. Tino aliipenda sana familia yake hata kuhangaika kwa hali na mali kumtibu mwanae Cheche kwa kila gharama kwani alidiriki kuiba fedha benki ili amudu kumpeleka mwanae nje kwa ajili ya matibabu. Mwandishi anatufundisha kuwa na mapenzi ya dhati kwani ni ishara ya mafanikio na amani. Kwa upande wa pili amejadili juu ya mapenzi yasiyo ya dhati au ya kweli. Mhusika Brown amechorwa kutokuwa na mapenzi ya dhati na kukosa uaminifu kwa mkewe na watoto kwani ni muhuni sana. Alikuwa na mahusiano ya mapenzi na wanawake wengi hakujali familia yake kabisa. Hakuonesha hata chembe ya upendo kwa familia yake. Mfano uk.109“mabinti zake walitamani sana kusafiri na baba yao. Lakini licha ya safari zake nyingi mno hawakupata fursa hiyo.”Pia uk.106 anasema watoto walikosa upendo“walitapia mno, lau kungekuwa na maelewano na upendo mkubwa baina ya baba na mama yao!fauka ya hayo baba yao alikuwa mkali”.Pia mapenzi yasiyo ya uaminifu kwa Brown na wapenzi wake kama vile Leila, Josephine. Mapenzi haya yalikuwa ya pesa tu! Uk 112 mwandishi amemzungumiza Leila “badala ya kumfikiria zaidi Brown Kwacha akatarajia zaidi faraja kuangalia nwanyama kwenye hifadhi ya Kwale”.Piauk.99Josephine anaomba fedha kwa Brown“.. cha kutosha kununua vitu vya harusi kama paundi alfu sita hivi”Mapenzi yasiyo ya dhati na ukosefu wa uaminifu katika ndoa ni janga katika jamii za sasa kwani wazazi hujisahau na kukiuka maadili ya ndoa jambo ambalo ni hatari mno kwani husababisha migogoro na ugomvi katika familia (mafarakano) na hata kuambukizana magonjwa hatari.
Nafasi ya mwanamke katika jamii
  • Amechorwa kama chombo cha starehe: Mfano ni Josephine na Leila, Brown Kwacha aliwatumia kujiburudisha kwa uasherati, pia wanawake walijiuza katika moja ya sehemu ambazo Amani alipenda kwenda.
  • Amechorwa kama kiumbe mwenye upendo: Mwema mke wa Tino ni mwanamke ambaye alikuwa na upendo wa dhati kwa mumewe na watoto kutokana na matunzo aliyowapa.
  • Amechorwa kama mlezi: Mfano mzuri ni Mwema na mke wa Brown ambaye yeye alikuwa ndiye mwangalizi mkuu wa familia kwani mumewe hakuwa na muda huo zaidi ya kuponda starehe na anasa kwa mda wa ziada aliopata badala ya kukaa na familia yake.
  • Amechorwa kama mtu mvumilivu: Mke wa Brown alivumilia sana mateso ya mmewe, hakuamua kumuacha bali alivumilia pamoja na kumdharau kote, kumdunisha na kutomthamini kama mke.
  • Amechorwa kama kiumbe duni: Brown hakumshirikisha mkewe katika maamuzi yoyote yale wala hakutaka ushauri wowote kutoka kwake alimdharau na kumpuuza tu.
  • Kama mtu jasiri na mwenye msimamo: Pamela anaoneshwa kuwa ni mwanamke jasiri kwani aliweza kumkataa Brown kimapenzi pamoja na vishawishi vya kila aina. Mfano uk.99 mwandishi anasema“lakini Pamela kama mwanariadha stadi, aliviruka viunzi vyote vya Kwacha…… mwanzo alimchukia lakini taratibu alianza kumheshimu”.
MIGOGORO
Mwandishi Safari pamoja na kujenga visa vyake vya kusisimua pia hakuacha kuibua migogoro ili kukamilisha masimulizi ya visa vyake.
Mgogoro baina ya pande mbili
  • Mgogoro baina ya Josephine na mke wa Brown: Sababu ya mgogoro huu ni Josephine kujihusisha na uhusiano wa kimapenzi na Brown Kwacha na kufumaniwa na mke wa Brown. Walipigana na kuumizana lakini Josephine hakuacha mahusiano hayo.
  • Mgogoro kati ya wafanyakazi wawili wasukuma makwama: Sababu ya mgogoro huu waligombaniana matenga ya kubeba na mwishowe kuishia kupigana.
  • Mgogoro baina ya Jinja Malon na vibaka: Jinja Malon aliwapiga vibaka baada ya kutaka kumkwapulia mwanamke mmoja hereni, mkufu na hata kutaka kumbaka kichochoroni. Uk 51-52.
  • Mgogoro kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya mila na utamaduni na kijana mmoja: Walipigana kugombania mwanamke ambaye alikuwa na mahusiano na wanawaume wote wawili. Uk.102.
Mgogoro wa nafsi wa Tino
Tino alisumbuliwa na mgogoro wa nafsi kutokana na hali ya ugonjwa wa mwanae Cheche. Hakujua apate wapi pesa za kumtibia kwani hakuwa na pesa na alitakiwa kupelekwa nje kwa ajili ya matibabu. Lakini baada ya kushauriwa na Amani akaibe pesa alifanya hivyo na kufanikiwa na ndipo alipata amani baada ya kumudu gharama za matibabu ya mwanae.
  • FALSAFA: Mwandishi anaamini kuwa chanzo cha matatizokatika jamii ni upotofu wa maadili, kutowajibika, mifumo mibovu ya uchumi, rushwa, ufisadi na biashara haramu na mengine mengi. Anaamini kuwa endapo jamii itabadilika basi hayo matatizo hayatakuwepo. Anatoa suluhu ya matatizo hayo kama vile kupinga utabaka, rushwa, matumizi mabaya ya mamlaka na kuwa na usimamizi mzuri wa mali za umma.
  • MTAZAMO: Mtazamo wa mwandishi ni wa kiyakinifu. Ameonesha matatizo ndani ya jamii na kuonesha suluhu ya matatizo hayo. Anaonesha matatizo ya uhujumu uchumi, ufisadi, kutowajibika kwa viongozi, ukosefu wa huduma za jamii, matabaka na hali ngumu ya maisha. Anaona kuwa sababu ya matatizo haya si ya kidhanifu tu au ni mipango ya Mungu tu! Ila anonesha sababu za matatizo hayo kama vile kukithiri kwa rushwa, mifumo mibaya ya kiuchumi na anatoa suluhu kwa kuwapiga vita viongozi wasowajibika. Mifumo mibovu ya uchumi inayoendelea kutengeneza utabaka katika jamii.
  • MSIMAMO: Mwandishi A. Safari ana msimamo wa kimapinduzi, hili linajidhihirisha wazi kutokana na mambo anayoyaeleza ambayo yanalenga kuibadili jamii. Analeta mapinduzi kwa viongozi wasiowajibika, mifumo mibovu ya uchumi inayoendelea kusababisha umaskini na kuwakweza wachache.Anatoa suluhu ya matatizo mbalimbali. Anakemea malezi mabaya kama ya Brown pia anasa na starehe na mengine mengi.
UJUMBE
  • Viongozi na watumishi wa umma wanapaswa kuwajibika kulingana na majukumu yao.
  • Rushwa, ufisadi na biashara za magendo ni vikwazo vya maendeleo hivyo si budi kupigwa vita.
  • Serikali na mamlaka husika vinapaswa kusimamia vyema sheria na taratibu ili kuwawajibisha wanaoenda kinyume kama vile wahujumu uchumi.
  • Uaminifu katika ndoa na mapenzi ya dhati ni jambo la msingi kwani huongeza Amani katika familia.
  • Jamii inapaswa kutambua nafasi ya mwanamake na kumshirikisha na sio kumdunisha bali apewe nafasi ya kuamua na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kimaedeleo.
Maudhui katika Riwaya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe
Hakiki maudhui katika Riwaya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe
DHAMIRA
  • Suala la kuchanganya kazi na mapenzi:Mhusika Ngoswe ambaye alitumwa na serikali kwenda kufanya zoezi la sensa la sensa kijijini anajiingiza katika mapenzi na binti Mazoea uk.5 na hivyo kusababisha kutokuwa makini na kazi yake. Anaamua kutoroka na Mazoea jambo ambalo linamfanya Mzee Mitomingi ateketeze karatasi za takwimu kwa kutoroshewa mwanae uk.28. hivyo tunaona jinsi mapenzi yallivyohaaribu kazi.Suala hili ni halisi katika jamii yeetu ya leo kwani watu wamekuwa wakijisahau na kuchanganya kazi na mapenzi, mwandishi ameliweka jambo hili wazi ili jamii iweze kubadilika na kuacha tabia hiyo mbaya inayodidimiza maendeleo ya jamii.
  • Hasara za ulevi:Suala la ulevi na hasara zake limejadiliwa na mwandishi akiwachora wahusika kama Ngoswe na Mzee Mitomingi na wanakijiji ambao ni walevi. Mfanouk.6 Mzee Mitomingi anasema “haya matatizo yote ni shauri ya pombe, sina shaka yuko kilabuni”.Ngoswe naye anapata hasara kutokana na ulevi kwani analewa sana na kuchoma karatasi za takwimu na kusababisha kuhesabu upya watu tena jamo ambalo lilipoteza mda zaidi.uk.18-19.Katika jamii yetu suala laulevilina hasara kubwa kama vile kurudisha nyuma suala zima la maendeleo, kusababisha vifo na ajali, migogoro ya kifamilia na matatizo mengine mengi. Jamii inaaswa kujirekebisha na kukemea suala hili kwani lina madhara makubwa katika koizazi cha sasa.
  • Umuhimu wa elimu:Wanakijiji wa kijiji cha Mzee Ngengemkeni hawana elimu na wala hawatilii maanani juhudi za kupata elimu. Huduma za kielimu ni mbovu kama vile shule iko mbali sana hazipo kijijini kwao. Familia nyingi na watoto wao hawasomi. Uk.16. zoezi la uhesabuji watu linakuwa gunu zaidi kuutokana na watu kutokuwa na elimu.Ili kupata maendeleo katika jamii yoyote ile si budi suala la elimu kupewa kipaumbele na wanaoelimika wanapaswa kutumia vyema elimu yao. Wanapaswa kurejesha mchango chanya katika jamii na sio kurudisha nyuma maendeleo.Mfano Ngoswe ambaye hakutumia vizuri elimu yake. Elimu lazima itumike kuibadilisha jamii na kusukuma mbele zaidi maendelo.
  • Suala la umaskini:Wanakijiji wanaelezwa kuwa na maisha duni sana ya hali ya chini, makazi duni. Mfano wanalala kwenye vibanda vibovu mfano Ngoswe anakaribishwa kulala katika moja ya kibanda kibovu kinaachovuja. Mwandishi amelionesha hilo makusudi kwani maeneo mengi ya mijini yamesahaulika na bado wapo nyuma kimaendeleo. Serikali iangazie maeneo ya vijijini na kutoa elimu ya namna ya kupambana na umaskini, kujenga makazi bora. Pia wanakijiji wanaaswa kuacha uvivu na kujishughulisha ili kumpinga adui maskini.
  • Suala la malezi na ndoa za mitara:Wanakijiji wa Balozi Mitomingi wana utamaaduni wa kuoa mke zadi ya mmoja. Pia suala la malezi si la baba bali la mama pekee. Mzee Mitomingi aliwaachia wakeze suala la kulea watoto na kuwa watazamaji wa familia, hali kadhalika Mzee Jimbi mda wote alishinda kilabuni kwenye pombe na hakuwa na mda wa kufanya kazi yoyote ya kimaendeleo wala kuangalia familia suala hilo aliwachia wake zake. Hili si jambo zuri.Kuhusu ndoa za mitara kwa jamii ya leo zina athari kwanikatika malezi ni vigumu kumudu ukubwa wa familia, usalama wa kiafya huwa ni mdogo kwani wanandoa wana hatari kubwa ya kuambukizana magonja hatari.
  • Imani potofu na ushirikina:Uk.14 tunaona wanawake wanakataa zoezi la kuhesabiwa kutokana na imani kuwa mtu anayehesabu watu ni mchawi. Kutokana na hili, zoezi la uhesabuji watu linakuwa gumu.Wanaamini kuwa mtu akifa basi amerogwa. Mfanouk.16 “wamemroga bure mume wangu. alikufa akiwa na nguvu zake”.Mambo mengine ya kimaendeleo hushindikana kutokana na imani potofu wanazoshikiliawanajamii. Mwandishi amelionesha ili jamii ijikomboe kutoka katika imani hizo potofu. Pia anaona upo umuhimu wa serikali kuelimisha jamii juu ya hili, kuacha kushikilia ukale na kuchangamkia maendeleo.
  • Utabaka kati ya mjini na vijijini:Katika tamthiliya hii suala la utabaka kati ya mjini na vijijini. Kuna tofauti kubwa kati ya mjini na vijijini katika masuala ya huduma za jamii kama vile elimu, afya na mengineyo. Uk.29 Ngoswe anasema:“Shurti vijiji kurekebishwa,Ujinga, magonjwa naUmaskini kupigwa vita,Na njia ni moja tu!Kuishi pamoja kijamaa.”Hivyo mwandishi amelionesha jambo hili ambalo linahalisika katika jamii yetu ya leo, hivyo si budi serikali kulitazama jambo hili kwa jicho pevu. Teknolojia na mawasiliano yaboreshwe kwani ni msingi wa maendeleo.
Nafasi ya mwanamke
Tamthiliya ya Ngoswe imemchora mwanamke katika sura zifuatazo:
  • Kama mlezi na muangalizi wa familia:Mama Mazoea na mama Inda na akina mama wengine ni waangalizi wa familia.
  • Kama chombo cha starehe:Wanaume wameonekana kuwatumia wanawake kwa ajili ya starehe. Hii inathibitishwa na tabia ya kuoa mitara.
  • Kama kiumbe duni asiyeweza kutoa maamuzi yoyote ndani ya jamii yake: Mfano Mitomingi anasemauk.26 “nyie wanawake akili zenu wote sawa si Mazoea si mama yake….”Jamii inashauriwa kumpa mwanamke nafasi na kumthamini hasa katika masuala ya uamuzi.
  • Kama mtu asiye na msimamo: Mfano ni Mazoea ambaye anaamua kutoroka na Ngoswe huku alijua ametolewa mahari.
MIGOGORO
  • Mgogoro kati ya Ngoswe na Mzee Mitomingi: Mgogoro huu unatokea baada ya Ngoswe kuamua kumtorosha binti wa Mitomingi. Mitomingi anaamua kuchoma moto karatasi za takwimu.
  • Mgogoro baina ya Mazoea na wazazi wake: Sababu ya mgogoro ni Mazoea kujihusisha na mapenzi na kutoroka na Ngoswe hali akijua alishatolewa mahari. Baba yake alimuadhibu kwa kumchapa.
  • Mgogoro kati ya Ngoswe na serikali: Sababu ya mgogoro ni kutokana na Ngoswe kushindwa kupeleka hesabu ya watu kama alivyoagizwa. Uk.28-29.
  • Mgogoro wa nafsi wa Ngoswe. Ngoswe alisononeka na kuwaza kuwa angejibu nini serikalini kwani karatasi za takwimu ziliteketea kutokana na uzembe wake.
  • FALSAFA: Imani ya mwandishi anaamini kuwa mabadiliko na maendeleo katika jamii yanawezekana kama watu watajishughlisha na pia kama serikali itagawanya vyanzo vya maendeleo bila ubaguzi nchini. Pia anaamini kuwa jamii inaweza kuingia matatizoni kama itachanganya mambo mawili kwa pamoja. Hivyo anashauri watu kuheshimu na kushikilia jambo moja ndipo utafanikiwa.
  • MTAZAMO: Mtazamo wa mwandishi ni wa kiyakinifu kwani anayaona mambo kiyakinifu, anaona kuwa kufanya kazi kwa bidii, kuheshimu kazi, kuwa na msimamo katika maisha ni suluhisho na chachuya maendeleo.
  • MSIMAMO: Mwandishi ana msimamo wa kimapinduzi kwani anapingana na mambo mabaya na kuyaweka wazi mfano uvivu, uzembe, kuchanganya kazi na mapenzi. Pia anapinga suala la ushirikina na imani potofu. Anaona kuwa ipo haja jamii kuwa na msimamo wa kimapinduzi kwa kupinga mambo yanayodidimiza maendeleo.
UJUMBE
  • Si vyema kuchanganya kazi na mapenzi kwani husababisha kazi kuharibika.
  • Ulevi huleta madhara na matatizo ndani ya jamii hivyo si budi jamii kupinga ulevi.
  • Elimu ni muhimu sana kwa jamii yoyote.
  • Kufanya kazi kwa bidii ni msingi wa maendeleo.
  • Wanawake wanapaswa kupewa nafasi ya kufanya maamuzi katika jamii.
  • Serikali na jamii vinapaswa kugawanya maendeleo sehemu zote za vijijini na mijini ili kuwa na maendeleo yasiyopishana sana ili kufifisha umaskini uliokithiri.
  • Wanaume wanaowavuruga wasichana kwa tamaa zao ipo siku watafikia tamati na kupata machungu ya ubaya wao.
  • Msimamo katika maamuzi ya mambo na kufikiri kabla ya kutenda ni jambo la msingi.
  • Nidhamu ya woga haijengi.


Maudhui katika Tamthiliya ya Kilio Chetu
Hakiki maudhui katika tamthiliya ya Kilio Chetu
DHAMIRA
  • Athari za gonjwa la ukimwi.Suala la ugonjwa wa ukimwi na athari zake limeajadiliwa katika kitabu hiki. Vijana wadogo kama Joti anaathirika na gonjwa hili kutokana na ukosefu wa elimu ya jinsia na magonjwa. Mwandishi anaelezea dalili,jinsi na ueneaji wa ukimwi jinsi ulivyo,pia athari za zake na namna ya kuwatunza wagonjwa wa ukimwi. Suala hili limekumba jamii yetu kwa kiasi kikubwa, mwandishi ananafananisha janga hili na dubwana uk.1. Jamii yetu ya sasa inaapaswa kuwakinga vijana wadogo na mambukizi haya kwa kuwaelimisha zaidi na kuwaasa bila kuwaonea haya.
  • Elimu ya jinsia:Elimu ya jinsia imejadiliwa kuwa na umuhimu mkubwa kwa kizazi cha leo, kinachokumbwa na mabadiliko makubwa ya kijamii hususani utandawazi. Kijana Ana alipatiwa elimu ya jinsia na ikamsaidia katika kupambana na vishawishi. Uk.25. hii ni kinyume na kwa mtoto Suzi na Joti, Mwarami na wengine ambao hawakubahatika kupata elimu hiyo. Wanaishia kupata madhara makubwa mfano Joti anakufa kwa ukimwi na Suzi anapoteza masomo kwa kupata ujauzito. Jamii haina budi kutoa elimu ya jinsia kwa vijana bila aibu kwani ndio mkombozi wa maisha ya ujana yenye changamoo nyingi, na tusiwe kama mama Suzi anaposemauk.9 “tena ishia hapohapo kaka! Huko si ndiko mkunifundishia mwanangu habari za ngono ilitoka wapi hiyoo….?”Hakubaliani kabisa kutoa elimu ya jinsia kwa mwanae kwani anaona ni kama uchuro na kufumndisha uhuni.
  • Mapenzi katika umri mdogo.Vijana wadogo hawapaswi kushiriki katika mapenzi mpaka pale wanapokuwa tayari. Kilio chetu kimejadili na kuonesha jinsi vijana wadogo Joti na Suzi wanavojiingiza katika ngono jambo ambalo ni kinyume na maadili yetu. Uk.16-17, 19-21. Si hivyo tu bali wanajiingiza katika mapenzi mpaka na watu waliowazidi umri mfano mwandishi anamsemea Jotiuk.23“sasa ndiyo kuparamia mpaka wasichana wakubwa wa mitaani? Fikiri juu ya Chausiku yule msichana mjuvi wa mji ambaye pia anachukuliwa na yule Mpemba muuza duka”Vijana wanaaminishana kuwa mapenzi ni halali yao, mfano uk.22 Jumbe anasema“MAPENZI NI TIBA”.Si budi jamii kukemea suala hili vikali kwani hupoteza nguvu kazi ya taifa la leo na kesho.
  • Athari za utandawazi.Masuala ya intaneti, sinema na picha za ngono, leo hii zina madhara mabaya kwa vijana wetu. Hutolewa bure bila kizuizi chochote wala hamna taratibu zozote zile zinazowabana watoto kuangalia mambo hayo. Vijana wa sasa wamekuwa wakipoteza mda mwingi na hata kufeli katika masomo yao kutokana na hili. Jumbe anasemauk.17 “leo si ndio siku ya picha ya “X”? umesahau?”.Ipo sababu sababu ya msingi kwa jamii kutafuta namna ya kuwaokoa vijana na kuweka taratibu zitakazowalinda juu ya hili.
  • Suala la malezi:Malezi bora yanayozingatia maadili ya jamii husika ni jamo la msingi sana. Jamii nzima inapaswa kushiriki katika malezi ya watoto.Katika kitabu Mama Ana na Baba Ana na Mjomba wameonesha mfano bora wa wazazi wazuri mfanouk.11 mjomba anasema “mzazi ndiye mwalimu wa kwanza” pia Baba Ana anasema “….mzazi usipomfunza, walimwengu watamfundisha tena sasa si maadili mema bali njia potofu”Hivyo tunaona kuwa mzazi ndio msingi wa maadili mema kwa mtoto, wazazi wanaaswa kuwa makini zaidi katika malezi.
  • Mapenzi na ndoa.Mapenzi na ndoa zimejaa udanganyifu na ulaghai siku hizi kwani uaminifu limekuwa jambo gumu ka wanandoa mfano uk.6-7 Mama Joti anaonesha wasiwasi wa kuchukuliwa mume wake na wanawake wengine anasema“huu ndiyo mwisho wa kumvumilia huyu Nguru anayeichimba ndoa yangu”.Hii inaonesha wazi suala la wanandoa kuwa na wapenzi wengine nje ya ndoa ni tatizo kwa jamii. Mwandishi amelionesha hili makusudi ili jamii iepuke haya kwani huleta madhara makubwa katika familia na jamii kama vile kutojali familia, kuambukizana magonjwa hatari na hata mafarakano ya wazazi.
  • Mila na desturi potofu.Mila na desturi potofu zikiendelea kushikiliwa na jamii yetu ya leo ni tatizo kwani zinasababisha madhara. Tunamuona Mama Suzi ambaye anaona suala la kumuweka wazi mwanae kuhusu mambo ya ukuaji, mapenzi na athari zake ni gumu. Anasemauk.10 “mie nikae hapa nafungua kinywa changu (anaigiza): sasa mwanangu mafanye hivi na vile…. Na vile mimba itatokea… uchuro huo!”.Anaona suluhisho ni kumpiga tu pale atakapokosea, jambo ambalo si sahihi kabisa kumbe tunapswa kuzitupilia mbali na kuendana na mabadiliko yenye tija kwa jamii yetu.
  • Huduma kwa wagonjwa wa UKIMWI.Hii pia ni dhamira muhimu iliyojadiliwa katika tamthiliya hii kwa jamii. Jamii ya sasa yenye watu waaathirika na gonjwa hili sekta na asasi mbalimbali zinatoa ushauri wa namna ya kuwatunza wagonjwa hawa.Mwandishi amelionesha hili ili jamii iwapende, kuwajali, kufurahi pamoja nao na kutowatenga kabisa. Faraja na matumaini ni jambo la msingi kwa wagonjwa wa Ukimwi, mfano uk.11 maelezo ya Mjomba juu ya kumtunza mgonjwa.
Nafasi ya mwanamke katika jamii
  • Amechorwa kama mtu mwenye msimamo na tabia njema: Mfano mzuri ni Ana. Aliweza kupinga vishawishi na aliwaelimisha wenzake juu ya elimu ya jinsia.
  • Amechorwa kama muelimishaji: Mama Ana ni mwanamke ambaye anatambua umuhimu wa elimu ya jinsia na alielimisha vyema, mfano mwanae Ana alikuwa na tabia njema na alifanikiwa.
  • Kama mtu muhuni: Msichana Chausiku alikuwa na wanaume wengi na tamaa, kwani aliweza hata kuwa na mahusiano na kijana mdogo Joti.
  • Mtu asiyependa mabadiliko (anayeshikilia mila na desturi potofu): Mfano mzuri ni Mama Suzi anashikilia mambo ya zamani, hataki kumuweka wazi mwanae Suzi kuhusu masuala ya jinsia, mapenzi na athari zake. Hafai kuigwa na jamii.
  • Kama kiumbe duni asiye na kauli (mwoga). Mama Joti alishindwa kuwa muwazi kupigania ndoa yake iliyovamiwa na wanawake wengine, bali anapitia njia za pembeni kutatua taizo hili kama vile kununua na kuvaa kanga zenye maandishi ya kejeli kumsema mwanamke anayemuibia bwana wake.
  • Kama mlezi bora wa familia. Mama Ana alishiriki kikamilifu katika malezi ya bintiye Ana na kumuokoa toka katika wimbi la vishawishi na maradhi, mimba za utotoni na matatizo mengine. Anafaa kuigwa na jamii kwani ni mfano bora.
MIGOGORO
  • Mgogoro kati ya Suzi na Mama Suzi. Mama Suzi alimwadhibu Suzi kwa kipigo baada ya kukuta Suzi akiwa na vidonge vya kuzuia mimba kaika mfuko wa sare za shule. Hii haikuwa suluhisho bora la mgogoro huu.
  • Mgogoro kati ya Joti na Chausiku. Sababu ya mgogoro huu ni Joti kuwa na mahusiano na Suzi ilihali pia alikuwa na Chausiku. Suluhisho Chausiku anamuonya Joti achane na Suzi.
  • Mgogoro kati ya Suzi na Joti. Sababu ya mgogoro ni Suzi kukataa kuendelea na mahusiano na Joti baada ya kugombezwa na mama yake. Suluhisho la hili Suzi anaamua kuendelea na mahusiano hayo baada ya ushawishi kutoka kwa Joti alihofia kumpoteza Joti.
  • Mgogoro wa nafsi wa Suzi: Suzi alijuta na kuwaza juu ya maisha yake. Alijihoji maswali yasiyo na majibu kuwa je alikuwa ameambukizwa virusi na Joti? Alikuwa pia haaamini kuwa tayari ana mimba alijihoji nafsi yake na kulia. Hakuwa na suluhu ya mgogoro huo zaidi ya kurudisha lawama kwa mama na jamii yake ambao hawakumuelimisha juu ya magonjwa na athari za mapenzi katika umri mdogo.
  • MTAZAMO: Mtazamo wa mwandishi ni wa kiyakinifu anayaona mambo kwa udhati wake. Anaona kuwa kutolewa kwa elimu ya jinsia kwa vijana ni suluhu tosha juu ya mimba za utotoni, maambukizi ya magonjwa yazinaa na tabia nyingine potofu.
  • FALSAFA: Mwandishi anaamini kuwa endapo vijana na watoto wataelimishwa kuhusu elimu ya jinsia wataokoka toka katika wimbi hatari la magonjwa na mmonyoko wa maadili. Haamini juu ya imani poofu kwani anazipinga kwa kuonesha ukweli na uhalisia wa mambo yalivyo mfano haamini kuwa ugonjwa wa ukimwi hupatikana kwa kurogwa ila kupitia kujamiiana na muathirika au kuchangia vyombo vyenye ncha kali au hata akuongezewa damu yenye virusi. Ila anaamini kuwa njia hatari zaidi ni kujamiiana hivyo anaiasa jamii kuepuka.
  • MSIMAMO: Msimamo wa mwandishi ni wa kimapinduzi, mambo anayoyakemea na kuyapinga yanalenga kuibadilisha jamii kutoka katika ukale na kushikilia mila potofu. Anaipinga tabia ya wazazi wasiotaka kuwa wazi kwa watoto wao na kuwaelimisha juu ya mabadiliko ya jamii yanayokumbwa na magonjwa hatari, utandawazi na mengineyo.
UJUMBE
  • Wazazi wanapaswa kutoa malezi bora kwa watoto wao.
  • Elimu ya jinsia ni muhimu kwa vijana na wazazi
  • Elimu ya ukimwi ni muhimu kwa jamii
  • Mila na desturi potofu si budi kupigwa vita
  • Uaminifu katika ndoa ni jambo jema
  • Mapenzi katika umri mdogo ni sumu
Maudhui katika Tamthiliya ya Orodha
Hakiki maudhui katika tamthiliya ya Orodha
DHAMIRA
Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi
Hii ni dhamira kuu iliyojadiliwa katika tamthiliya hii. Mwandishi analenga katika mapambano ya Ukimwi hasa katika maeneo ya vijijini ambapo bado elimu kuhusu ugonjwa huu haijafika vyema. Anamtumia mhusika Furaha kutuonesha jinsi binti huyu mdogo wa kijijini anavopata ugonjwa huu na hatimaye kufa. Furaha bila kujua alijiingiza katika mapenzi na wanaume tofautitofauti mfano Bwana Ecko, Padre James, Salim, Kitunda na wengine.
Mwandishi anaona upo umuhimu wa jamii kueleweshwa vyema kuhusu mambo yanayopelekea kupatikana kwa ugonjwa huu hatari kama vile kuwa na mahusiano na wapenzi wengi. Mwandishi anapendekeza mambo ambayo anaona ni suluhisho la kuenea kwa ugonjwa huu zaidi. Mambo hayo ni pamoja na uwazi na ukweli katika hili, kutolewa kwa elimu juu ya Ukimwi, uadilifu, uaminifu katika ndoa, ngono salama, upendo kwa wagonjwa wa Ukimwi, msamaha na welewa. Hii ni kupitia barua ya Furaha aliyoiacha isomwe katika mazishi yake. Uk.44-45,
“Nawashukuru kwa kufika kwenu na kuyasikiliza maneno yangu ya mwisho. Msiogope kwani nadhani maneno haya yanaweza kuwasaidia.katika hii miezi ya mwisho nimelala kitandani nikifa,nikizidi kuugua. Nilipata muda mwingi wa kufikiri, kubadilika, kukua kama mtu; hata ninapokuwa ninakufa. Katika ukurasa unaofuata kuna orodha ya vitu ambavyo vilisaidia kuyafupisha maisha yangu, orodha ambayo inaonesha kwenu nyote ukweli juu ya kifo changu mama tafadhali wasomee watu wote orodha hii.”
Mmomonyoko wa maadili
Mmonyoko wa maaadili ni pale ambapo wanajamii huenda kinyume na makubaliano ya jamii yao, yaani taratibu, kanuni mila na desturi zao. Mwandishi anaona kuwa suala la mmonyoko wa maadili ni kichocheo cha maovu katika jamii. Anamtumia muhusika Mery na Furaha ambao ni vijana wadogo kabisa lakini wanajiingiza katika tabia zisizofaa kwani katika jamii yao waliwasema juu ya hili kwani walipotoka. Wazazi wa Furaha wanalipigia kelele suala hili lakini kijana wao tayari alishaharibika, mfano tunaona uk. 11 baba Furaha analaumu juu ya tabia ya Furaha anasema “ nilichokuwa nafahamu …. Hadi sasa Furaha… ni kwamba umekuwa ukitoroka nyumbani wakati wa usiku wa manane! Kuna jambo lingine ambalo anapaswa kulifahamu” anaendelea kusema “kutoroka… bila ruhusa… baa wanaume.. wewe …. Malaya usiye na shukrani!”.
Katika jamii ya leo wazazi wanapewa ujumbe kuwa suala la kuwaangalia watoto na kufuatilia nyendo zao ni jambo la msingi sana hasa katika kipindi kigumu cha makuzi. Kwa kufanya hivyo kutasaidia kuikoka jamii toka katika hatari ya kupoteza vijana wengi zaidi.
Uaminifu katika ndoa na mahusiano
Mhusika Bwana Ecko hakuwa mwaminifu kwa mkewe kwani alikuwa malaya na aliyewaharibu mabinti wadogo waliokuwa kama wanae wa kuwazaa kiumri. Furaha anarubuniwa na kujikuta akitumbukia katika mapenzi na baba huyu. Mfano uk.6 tunaona Bwana Ecko anavosema“karibuni kwenye baa yangu. Karibuni kae nami, wapenzi!Bia mbili kwa ajili ya wasichana warembo”.Hali kadhalika katika kitabu Furaha anaelezwa kukosa uaminifu kwani licha ya kutembea na Bwana Ecko ila pia alijihusha na wanaume wengine kama Kitunda na Salim na hivyo kusababisha kuenea zaidi kwa ugonjwa huu.
Suala la upotofu wa uaminifu ni janaga katika jamii ya leo, kwani tunaona watu wazima sasa badala ya kuwa mstari wa mbele kuwasaidia mabinti wadogo kimaadili ila wao ndio wamekuwa mstari wa mbele katika kuharibu maisha yao. Ni tabia mbaya na inapaswa kupigwa vita.
Umaskini na hali ngumu ya maisha
Katika kitabu tunaona kuwa sababu mojawapo iliyopelekea Furaha kupata maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi ni hali ya umaskini. Furaha alitamani vitu vizuri na hakujua madhara yake na namna ya kuvipata, alifurahia kuvipata na kujiona mwenye bahati. Mery anasemauk.7 -8 “nimekwambia hawa jamaa ni burudani…hata yule mshamba Juma. Sikia, pata burudani na kuwa mwema, kwa Ecko. Anaweza kukununulia vitu vingi sana! Unadhani wasichana wadogo hapa mjini wanapataje viatu vipya, magauni na mabegi mapya ili wapendeze….wapendeze kiasi cha kuwavutia vijana wazuri wa kiume?”
Mwandishi anaonesha hili kwani wasichana wengi hutumbukia katika janga la Ukimwi kutokana na umaskini. Anaona ipo haja ya watu kuelemishwa kuwa kila jambo lina wakati wake hasa kwa mabinti, washauriwe juu ya mambo mbadala ya kujipatia pesa na sio kujirahisisha kwa wanaume. Kumbe ni muhimu elimu ya ukimwi inapotolewa katika jamii basi pia watu hasa vijana waelekezwe pia namna ya kujikomboa kiuchumi, na waone kuwa ngono sio chanzo cha mapato bali wanapaswa kujibidisha ili kuwa na vipato vya kukidhi mahitaji yao ya muhimu.
Ukosefu wa uadilifu katika kazi
Padre James katika kitabu ameonekana kutokuwa muadilifu kuendana na maadili ya kanisa akiwa kama Padre. Anajisahau na kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na mtoto Furaha hali akijua kabisa ni kinyume na maadili na kazi yake ya upadre.Uk.10 “Furaha alikuja kama alivyoagizwa….ee.. Ekaristi takatifu ilipatikana lazima uelewe jinsi ilivyo vigumu kwa mtu wa hadhi yangu na wadhifa wangu”
Tofauti na ilivyotegemewa kuwa Padre James angekuwa mstari wa mbele kuiongoza jamii katika maadili mema. Lakini yeye ndiye anakuwa chanzo cha uharibifu wa maadili, suala hili lipo katika jamii kwani wapo watu ambao wameteuliwa kuwa kioo na taa ya jamii kumulika maovu lakini wao hutumia mwamvuli huo kujifunuika kufanya maovu kwa urahisi zaidi. Mwandishi ameona kuwa hili ni tatizo na anapingana kukemea vikali watu wa aina hii.
Umuhimu wa kusema ukweli na kuwa wazi
Hii ni suluhu mojawapo ambayo mwandishi anaamini kuwa ikitumika vyema basi ni kinga tosha dhidi ya Ukimwi. Baadhi ya watu hujielewa wazi kuwa tayari ni waathirika ila hawapendi kuwa wazi na kusema ukweli juu ya hilo, bali hunyamaza na kuendelea kuambukiza wengine. Mwandishi amemtumia mhusika Furaha na Mama Furaha kuwa mfano wa kuigwa kwani hawakuona haya juu ya kusema ukweli kuhusu ugonjwa uliomuua Furaha. Wanalisema hili mbele ya wanakijiji wote wakiwa na lengo la kuikomboa jamii yao.
Barua ya Furaha ni mfano toshauk.44-45. “kondom,uaminifu, elimu,welewa, uwazi,uadilifu, uwajibikaji, ukweli, upendo na msamaha,…ukosefu wa mambo yote haya ndio ulioniua. Ufuatiliaji wa mambo yote haya unaweza kuwaokoa ninyi nyote…wanusuruni watu wetu….wanusuruni watoto wetu ili wasiwe yatima. Muinusuru Afrika…yetu nzuri.”Pia hakumficha mchumba wake salim bali alimwambia ukweli uk.29 Furaha anasema“Nina Ukimwi Salim”
Suala la upendo
Upendo wa kweli ni ule ambao hujali kitu au mtu katika shida na raha, kujitolea kwa moyo wote bila kujali lolote. Ni kujitoa kwelikweli. Mwandishi analizungumzia jambo hili kama suala muhimu sana katika jamii. Tunapaswa kuonesha upendo kwa wagonjwa wa Ukimwi kwa kuwafariji na kuwapa matumaini, pia hata wahanga wa gonjwa hili kama vile watoto yatima ambao huachwa na wazazi wao wakiwa wadogo wanapaswa kupewa msaada na matunzo mazuri. Hawapaswi kunyanyapaliwa ila kupendwa.
Katika kitabu mhusika Mama Furaha ameonesha upendo wa kipekee kwa mwanae pamoja na hali aliyokuwa nayao Furaha jambo ambalo si rahisi kwa watu wengi. Mfanouk.30-31 Mama Furaha anaongea na mwanae akiwa hoi kitandani katika hali ya upendo na kujali anasema, “hakuna mtu aliye kamili. Lakini uliwaangalia wadogo zako. Na kila mahali ulipokuwapo, kulikuwa na nuru ya jua! Ulikuwa binti mzuri…binti yangu mzuri…. Inaelekea kama umezaliwa jana tu. Na hata wakati huo ulizidi kunifanya nisubiri, wakati nikiwa na mimba yako. Nakumbuka jinsi ulivyokua. Ukikmbia shambani mwetu, ukijaribu sana kumfurahisha baba yako…unajua anakujali kwa namna yake…..amelala sasa lala mwanangu”.
Imani potofu juu ya ukimwi
Wanakijiji katika kijiji cha Furaha wengi wao hawakuwa na elimu juu ya ugonjwa huu hatari, Furaha alipougua kila mmoja alisema lake wengine wakidai kuwa ni kurogwa. Pengine pia ujinga ulichangia wao kutoelewa kuhusu Ukimwi. Mfano uk.25-26 majibizano ya wanakijiji juu ya habari za kuumwa kwa Furaha.
  • Mwanakijiji wa 1: Bi Furaha anaumwa sana…
  • Mwanakijiji wa 2: Tulijua anaumwa
  • Mwanakijiji wa 1: Ndiyo lakini katibu katika ofisi ya daktari kanambia ana huu ugonjwa wa AIDS
  • Mwanakijiji wa 4: Hicho si kitu kizuri
  • Mwanakijiji wa 1: Wanauita slim kwa sababu ugonjwa wenyewe hukufanya ukondeane
  • Mwanakijiji wa 3: Lakini amewezaje kuupata ugonjwa kama huo!
  • Mwanakijiji wa 1: Rahisi! kuna mtu kamroga…. Pengine rafiki msichana mwenye wivu.
  • Mwanakijiji wa 2: Nasikia unaupata kwa kugusana tu!
  • Mwanakijiji wa 4: Au hata kuwa nao katika chumba kimoja!
Mazungumzo hayo yanatuweka wazi kuhusu haliiliyoko kijijini juu ya elimu kuhusu Ukimwi, wapo baadhi ya watu bado wanaamini kuwa Ukimwi ni kurogwa tu, serikali na mamlaka husika vinapaswa kutoa elimu ya kutosha katika jamii ili kuwakomboa watu walioko vijijini.
MIGOGORO
  • Mgogoro kati ya Furaha na wazazi wake: Sababu ya mgogoro huu ilitokana na Furaha kuanza kupotoka kimaadili. Kwani alitoroka nyumbani usiku na kwenda kwa wanaume baa kunywa pombe. Baba yake na mama yaake walimuadhibu kukemea suala hili.
  • Mgogoro kati ya Padre James na Mama Furaha: Sababu ya mgogoro huu ni orodha, Padre James alimzuia mama Furaha asisome barua yenye orodha kwani alihofia pengine jina lake lingetajwa miongoni mwa watu waliokuwa na mahusiano ya mapenzi na Furaha. Suluhisho la mgogoro huu Mama Furaha alimuweka wazi Padre juu ya umuhimu wa kuisoma barua hiyo kuwa hana la kuficha bali aliisoma kwa lazima uk.3 na 43.
  • Mgogoro kati ya Salim na Mama Furaha: Salim hakutaka orodha isomwe hivyo alichana barua yenye orodha mazishini. Mama Furaha hakusita bali aliisoma barua hiyo kwa kukusanya vipande na kuviunga. Uk.43 na 44.Mgogoro kati ya Furaha na Dada mdogo.Huu ulitokea pale ambapo Furaha alitaka kutoroka usiku na mdogo wake kubaini na hivyo kutishia kusema kwa wazazi. Suluhisho Furaha alimkemea na hata kutishia kumchinja uk.6 Mdogo wake aliogopa na kutosema lolote tena.
  • Mgogoro kati ya Slim na Furaha: Huu ulitokana na Salim kumlazimisha Furaha amsomee orodha yeye kwanza lakini Furaha aligoma na kumsihi asubiri. Ndipo Salim alipokasirika na kuanza kutupiana maneno. Mama Furaha anasuluhisha mgogoro huu kwa kumuamuru Salim atoke nje. Uk.30
  • Mgogoro wa nafsi: Huu uliwakuta Padre James, Salim, Kitunda, Bw Ecko baada ya kuhofia juu ya orodha ambayo Furaha aliiandika ili isomwe katika mazishi yake. Walihofia endapo wangetajwa katika orodha hiyo kwani wangeaibika mbele ya kijiji kutokana na kujua fika kuwa mambo waliyoyafanya ni kinyume na maadili. Wanajitahidi kuzuia orodha hiyo isisomwe kwa hali na mali, lakini hawafanikiwi. Mama Furaha anafanikiwa kusoma orodha hiyo na kutoa ujumbe kwa jamii nzima. Wanapata amani baada ya kujua kuwa orodha iliyosomwa haikuwa na majina yao.
  • FALSAFA: Mwandishi anaamini kuwa endapo jamii itaelimishwa juu ya ugonjwa wa Ukimwi ni rahisi kuepuka na kujikinga na maambukizi mapya. Hii ni kupitia mambo anayoyapendekeza mwandihi kama vile uwazi, uadilifu, ukweli, upendo, matumzi ya kondomu, elimu, welewa, msamaha, uaminifu.
  • MTAZAMO: Mwandishi ana mtazamo wa kiyakinifu kwani anayaona mambo kwa udhati na uhalisia wake. Anapinga mtazamo wa kidhanifu juu ya ugonjwa wa Ukimwi kama vile kuamini kuwa ugonjwa huu unapatikana kwa kurogwa. Anaweka wazi sababu za upatikanaji wa ugonjwa huu.
  • MSIMAMO: Msimamo wa mwandishini wa kimapinduzi kwani analenga kuikomboa jamii kutoka katika hatari ya gonjwa la Ukimwi. Anapendekeza mambo ya kufanya ili kuepukagonjwa hili. Kama vile uaminifu, uadilifu, upendo, ukweli na uwazi nk.
UJUMBE
  • Elimu ya ukimwi ni muhimu kutolewa katika jamiiya leo.
  • Wagonjwa na wahanga wa Ukimwi wanapaswa kupendwa na kujaliwa.
  • Ukweli na uwazi ni suluhu mojawapo ya kuepusha maambukizi mapya.
  • Watu wazima wanaoharibu maisha ya watoto wadogo wanapawa kupigwa vita.
  • Upendo ni jambo la msingi kwa wahanga wa Ukimwi.Wazazi wanapaswa kuwa makini katikamalezi bora kwa vijana .Watu wanapaswa pia kukombolewa kiuchumi kama njia dhidi ya kupinga ukimwi.Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu.Ulevi ni kichocheo cha maovu.
Maudhui katika Tamthiliya ya Watoto wa Mama N’tiliye
Hakiki maudhui katika tamthiliya ya Watoto wa Mama N’tiliye
DHAMIRA
  • Umaskini na hali ngumu ya kimaisha:Watoto wa Mama Ntilie wanaishi katika hali ngumu sana kwani wanakosa shule sababu ya kukosa fedha, malazi, mavazi, chakula ni duni sana kwao. Tunaona kuwa hata kazi anazofanya Mama Ntilie ni kazi za vijungujiko kama anavyosema mwandishi uk.14, faida yake ni ndogo kwani haikidhi mahitaji ya familia. Mwandishi amejadili hili ili serikali na jamii kwa ujumla wake viweze kubuni mbinu za kuwakomboa akina mamawasiliano na ajira, wasio na kipato chochote au kipato cha chini sana. Ili kuepusha athari hasi za umaskini kama vile uhalifu, wimbi la watoto wa mitaani nk. Pia wakazi wengine wanalezwa kuwa na maisha magumu mfano uk.26 “watu walisongamana wakasukumana kugombania mchele ambao ….” Hii inatuonesha kuwa walikula vyakula vya jaani.
  • Jangala watoto wa mitaani:Katika kitabu hiki watoto Dan, Doto na Kurwa ni watoto wa mitaani. Hali hiyo imewakuta baada ya kukosa wazazi na malezi yao.. maisha yao ni ya shida mno yanayoenda kwa kudra za mwenyezi Mungu, kwani hula na kuvaa jalalani. Mfanao uk. 20,21-25-26. Suala hili ni janga sugu kwa nchi yetu kwani badala ya kupungua linaongezeka kwa kasi kwani watoto wa aina hii ni wengi mtaani na hawana dira yoyote ya maisha yajayo na kuwafanya kujiingiza katika shughuli zisizo halali ili kujipatia kipato.Suala hili limeoneshwa ili jamii na mamlaka husika viweze kuchuka hatua kwa kuwakomboa watoto hawa mfano kuwapatia elimu na mahitaji mengine ya msingi kwa watoto.
  • Suala la ukosefu wa elimu:Watoto wote wanaoelezwa katika riwaya hii kama Dan, Doto, Kurwa, Musa, Peter na Zitta hawana elimu na wala hawana ndoto za kusoma baadaye kutokana na hali halisi ya maisha yao. Wazazi wao hawamudu kuwapeleka shule, tunaona wanafukuzwa shule kutokana na kukosa sare za shule! Na ada!Uk.1 mwalimu Chikoya anasema “wote ambao hamna ada na hamna sare! hakunashule! nisizione sura zenu bila ada na sare waambieni hivyo wazazi wenu”.Suala la kuwafukuza watoto shule si jukumu lao bali la wazazi wao, kwani ni kumnyima mtoto haki yake ya msingi. Jamii na serikali inapashwa juu ya hili ili watambue kuwa elimu kwa mtoto ni muhimu kwani ndio msinngi wa maisha yao. Na kuwasaidia wazazi wasio na uwezo wa kusomesha.
  • Uhalifu, wizi na ujambazi na uuzaji wa madawa ya kulevya:Katika riwaya, watoto wadogo sana wameoneshwa kujiingiza katika sula la uhalifu mfano uuzaji wa madawa ya kulevya, wizi nk. Tunawaona vijana Dan na Doto wanajihusisha na wizi na hata kuhatarisha maisha yao na kufa. Uk.42-45. Kwa upande mwingine tunamuona mtoto Musa ambaye anajiingiza kwenye biashara haramu ya madawa ya kulevya. Anamshawishi pia Peter na kusababisha maisha yao kuishia jela.. mwandishi ameliangazia hili ili jamii iweze kuwa makini katika mienendo ya watoto kwa kuwalinda hasa kwa jamii ya sasa, ambapo vigogo huwatumia vijana wadogo katika biashara hii haramu. Wanatakiwa kuchukuliwa hatua na kuwajibishwa vikali.
  • Ulevi: Ulevi ni kikwazo cha maendeleo. Usemi huu unatokana na mambo aliyoyaonesha E. Mbogo katika riwaya kwani Mzee Lomolomo ni mlevi wa kupindukia na mwandishi anaeleza uk.10-13, juu ya Lomolomo ambaye hajui wanae wanaishije anachojua yeye ni pombe tu.Uk.49 “ratiba ya baba yao Mzee lomolomo………Ni mwanaume lofa kama asemavyo mwandishi kwani hajibidishi na kazi yoyote, naye anachangia ugumu wa maisha ya watoto wake. Suala la ulevi linahalisika katika jamii yetu ya leo katika familia zetu kwani baadhi ya wazazi huhusudu pombe na kusahausuala zimala malezi ikiwa ni wajibu wao! Wengi huishia kuharibu kazi, kuzua ugomvi, wizi nk. Mfano tunaona Mzee Lomolomo anakufa kutokana na tamaa ya pombe kwani anakunywa pombe ambazo zimepitwa na wakati na kumfanya afe.
  • Mapenzi: Katika riwaya mhusika Peter alionesha mapenzi ya dhati kwa Kurwa, kwani alimsaidia Kurwa uk.65 Peter anasema“tungoje mama arudi, lakini siwezi…. Hatuwezi kumfukuza, tukamwacha ateseke tu huko mtaani”.Pia tunaona mapenzi ya dhati ya Mama Ntilie kwa mumewe Mzee Lomolomo, kuwa pamoja natabia mbaya ya ulevi, kutofanya kazi na kutojali familia, kumsimanga na kumtukana lakini baado alimpenda na kumheshimu kama mumewe mfano alimpa chakula. Uk.13 pamoja na kuwa alilewa.
Nafasi ya mwanamke
Katika riwaya mwanamke amechorwa katika mtazamo tofautitofauti nzuri na mbaya:
  • Amechorwa kama mlezi na mhimiliwa familia. Mama ntilie ndiye aliyekuwa mlezi mkuu wa familia, bila yeye hakuna kilichowezekana katika familia, yeye ndiye aliyejua kula, kulala na kuvaa kwa wanawe. Wanawake wengi katika jamii huachiwa jukumu la kulea na wanaume kujisahau. Jamii imeoneshwa hili ili pande zote mbili zishiriki katika malezi.
  • Kama mtu mvumilivu: Mama ntilie ameoneshwa kuwa mvumilivu kwani alimvumilia mumewe pamoja na tabia yake mbaya. Anafundisha wanawake wengine kuwa wavumilivu kwani mvumiliivu hula mbivu!
  • Amechorwa kama muwajibikaji/ mchapakazi: Tofauti na wanawake wengine mama ntilie amekuwa machapakazi wa aina yake kwani pamoja na kipato kidogo alikuwa mfanyabiashara wa chakula katika kiwanda cha urafiki ambapo alipata pesa ndogo ya kujikimu yeye na wanae.Katika jamii ya leo wanawake wanaaswa kuwa wajasiriamali kwa kutafuta vyanzo vya riziki halali.
  • Amechorwa kama mtu mwenye huruma na roho nzuri: Mfano ni Jane ambaye alichukua jukumu la kuwalea watoto Kurwa na Doto ambao walifiwa na mama yao, kweli ni upendo wa kipekee. Pia Zenabu aliwahurumia Peter na Zita na ndiye aliyemsaidia Zita kwenda hospitali alipoumwa kichaa cha mbwa.
  • Amechorwa kama mtu mwenye wivu na roho mbaya: Mfano ni Zita, hii ni baada ya kuona Peter amemleta Kurwa nyumbani kwao. Hakuwa na upendo hata kidogo na hivyo kupigana naye kwa sababu ya chuki. Wanawake wanashauriwa kutokuwa na roho mbaya.
MIGOGORO
Riwaya ya watoto wa Mama Ntilie imejadili migogoro ya aina zote mbili ya nafsi na migogoro ya pande mbili.
  • Mgogoro kati ya Peter na Doto. Uk.20-22: Watoto hawa wawili walipigania masalia ya chakula jaani, Kurwa alisuluhisha ugomvi huo kwa kumzuia Doto kuendelea kumpiga Peter.
  • Mgogoro kati ya Mama ntilie na mzee lomolomo: Sababu ya mgogoro huu ni mzee lomolomo kuwa mlevi na kutoa matusi kwa mkewe aliporudi usiku.
  • Mgogoro kati ya Zita na Kurwa. Uk.60-64: Sababu ya mgogoro huu ni kuwa Zita hakumpenda Kurwa aje kwao mmoja wa familia yao. Walipigana hadharani, Peter alisuluhisha ugomvi huo kwa kumueleza Zita ukweli na kumkanya asimpige tena Kurwa.
  • Mgogoro kati ya zita na na Peter: Zita na Peter waliingia katika mgogoro baada ya Peter kufika nyumbani na Kurwa jambo ambalo halikumpendeza kabisa Zita. Peter alisuluhisha mgogorohuu kwa kumuambia hali halisi ya maisha ya Kurwa.
  • Mgogoro wa nafsia wa Kurwa: Kurwa aliwaza na kuihoji nafsi yake bila kuwa na majiu kuhusu ugumu wa maisha waliyokuwa nayo, kukosa wazazi hakuwa na jibu la mgogoro wake na hivyo kuendelea kujutia tu kuzaliwa. Uk.37-38.
  • Mgogoro wa nafsi kwa Peter: Aliwaza na kusumbuka ni lini angerudi shule kwani baada ya kufukuzwa na mkuu wa shule aliwaza ni vipi angepata pesa na wapi?, ili aweze kulipia karo na sare kwani wazazi wake hawakuwa na uwezo huo.
  • FALSAFA: Imani ya mwandishi ni kuwa endapo watu watakombolewa na kufanya kazi kwa bidii wataukwepa umaskini na hali ngumu ya kimaisha. Mambo mengi anayoyaeleza anaishauri zaidi serikali kuwatazama wanawake kwa macho mawili na kuwasidia katika mitaji yao midogo.
  • MTAZAMO: Emmanuel Mbogo ana mtazamo wa kiyakinifu. Anayaona mambo kwa uhalisia wake ndani ya jamii. Anaona kwa umaskini na matatizo mengine ya kiuchumi na maisha hayatokei tu kwa kudra za mwenyezi Mungu bali ni mipango mibovu ya serikali, wananchi kutojishughulisha, malezi mabaya ya watoto.
  • MSIMAMO: Mwandishi ana msimamo wa kimapinduzi kwani mambo anayoyaeleza ni kupiga vita kama vile umaskinina hali ngumu ya maisha, suala la ulevi, biashara ya madawa ya kulevya, wimbi la watoto wa mitaani. Haya ni mambo yanayotishia maendeleo ya jamii hivyo anasema makusudi ili jamii na mamlaka husika viweze kubadilika na kusaidia panapowezekana.
UJUMBE/MAFUNZO AU MAADILI
  • Tunafundishwa kuwa ulevi ni kikwazo cha maendeleo. Hivyo si budi kuupinga.
  • Suala la malezi ni jukumu la wazazi wote wawili na si la mama tu kama alivyofanya mzee Lomolomo.
  • Kuwafukuza watoto shule kwa ukosefu wa ada na sare ni makosa kwani ni kuwadidimiza watoto kielimu na kuwakosesha haki yao ya msingi.
  • Serikali na jamii vinaaswa kupunguza wimbi la watoto wa mitaani kwa kuwasaidia, si kuwaacha wateseke.
  • Uhalifu si mzuri kwani mwisho wake ni mbaya.
  • Tunafundishwa kuwa kujishughulisha na kufanya kazi kwa bidii ni suluhu ya maendeleo, tunamuona mama ntilie kupitia kazi yake ndogo aliweza kuikimu familia yake.
  • Umaskini na hali ngumu ya maisha ni tishio kwa jamii hivyo mwandishi anatuasa kufanya kazi kwa bidii ili kuushinda umaskini.
  • Upendo na huruma ni mambo mema na mazuri kwa jamii. Mfano Peter alimhurumia Kurwa na kumsaidia.
  • Wazazi wanaaswa kuwa makini katika malezi ya watoto na kutowaacha wajiamulie mambo. Mfano mzazi wa Musa alimuacha Musa na kupotea.


Maudhui katika Ushairi wa Wasakatonge
Hakiki maudhui katika Ushairi wa Wasakatonge
DHAMIRA
Kupinga unyonyaji na ukandamizwaji.
Mashairi ya“Wasakatonge”, “Mvuja jasho”, “Sikuliwa sikuzama”, “Madikteta”ni mashairi yanayopinga na kukemea sula la unyonyaji na ukandamizwaji wa watu wanyonge wa tabaka la chini. Mwandishi amesema haya makusudi ili kukomesha mambo haya kwani huendelea kukuza utaaka katika jamii. Anaishauri serikali kuweka mikakati ya kuwakomboa wanyonge. Mfano katika shairi la“wasakatonge”anasema:
Pia katika shairi la“Mvuja jasho”mwandishi anawashauri wanyonge kushirikiana ili kujikomboa.
Kupigania haki na ukweli
Mwandishi pia anaona upo umuhimu wa jamii kutafuta na kuisimamia haki ya kweli. Anaona kuwa suala la haki likizingatiwa katika jamii itaepusha matatizo kama vile ya migogoro nk. Mfano wa mashairi ni shairi la“Kosa”, “Marufuku”.Mfano katika shairi la“Kosa”anasema:
Mwandishi ameonesha hali halisi ya baadhi ya wananchi walio wengi ambao kipato chao bado ni duni. Anaona sababu ya hali hii ni mifumo mibovu ya kiuchumi inayoendelea kukuza utabaka katika jamii kati ya walio nacho na wasio nacho mfano katika shairi la “Walalahoi”anasema:
Mashairi mengine ni“Waasakatonge”na“Mvuja jasho”
Kupiga vita matabaka katika jamii
Matabaka ni suala lisilo zuri katika jamii kwani husababisha walio chini kuendelea kukandamizwa na walio juu kiuchumi, kisiasa nk. Mfano wa mashairi yanayopinga ni “Miamba” na “Wasakatonge”. Mfano akatika shairi la “Miamba”
Umuhimu wa kutunza amani
Mwandishi analizungumzia suala la amani katika shairi la“Afrika”.Bado anaona jamii bila amani haiwezi kuendelea. Watu huhitaji amani ya kuishi pamoja na sio kwa vigezo vya ukabila au utaifa. Mfano anasema katika moja ya beti zake:
Suala la uongozi
Hapa uongozi umejadiliwa katika pande zote yaani uongozi mzuri na mbaya. Lakini mwandishi ana lengo moja la kuwafanya viongozi wasio waadilifu kubadilika na walio waadilifu kuacha. Anazungumzia kiongozi bora anatakiwa aweje anamfananisha na nahodha katika shairi la“Nahodha”anasema;
Mwandishi anafananisha nahodha wa ngalawa na nahodha wa nchi. Anaona kiongozi bora ni Yule anayeongoza kwa matakwa ya wananchi na sio matakwa yake binafsi. Anawataka viongozi walioshindwa kutawala waachie madraka kwa wenye uwezo huo. Pia yapo mashairi mengine kama vile“Madikteta”, “Saddam Hussein” ‘Unyama”ambayo yanakemea uongozi wa mabavu na unyonyaji. Haoni umuhimu wote kwaviongozi kutawala kwa mabavu bali watumie sheria na demokrasia ya kweli.
Vilevile anazungumzia viongozi walio wasaliti. Anaona kuwa viongozi wa aina hii ndio wanaokwamisha mendeleo. Walipewa madaraka lakini wanayatumia vibaya na kushindwa kutekeleza waliyoahidi. Mfano wa mashairi ni“asali lipotoja” na “waramba nyayo
Ukombozi wa wanawake
Wanawake wakiwa ni watu muhimu sana katika jamii mwandishi anaona kuna umuhimu wa wao kuheshimiwa na kupewa nafasi ya kushiriki katika shughuli za kimaendeleo. Anayasema haya katika mashairi ya “Wanawake wa Afrika”, “tohara”, “Mwanamke”, na “Mama ntliye”.Mfano katika shairi la“wanawake wa Afrika” anasema.
Pia mwandishi anapinga mila mila potofu kama vile tohara kwa wanawake katika shairi la“Tohara”.Kwani ina madhara makubwa kwa mwanamke kama vile kifo.
Suala la mapenzi na ndoa
Mwandishi amejadili kwa kiasi kikubwa kuhusu mapenzi ya kweli na ya dhati. Mfano katika mashairi ya “Nakusabiliya”, “Tutabakia wawili” “Nilinde” “Mahaba”.Mfano katika shairi la“mahaba”anasema;
Anakemea mapenzi yasiyo ya kweli ya usaliti. Mfano katika shairi la“Sili nikashiba” ”Si wewe?Mfano katika shairi la“Sili nikashiba”anasema juu ya usaliti;
Kupinga ukoloni mamboleo
Huu ni ukoloni ambao pamoja na nchi kupata uhuru wa kujitawala lakini bado huendelea kupitia njia zingine kuwakandamiza watu. Mwandishi anakemea hili na kuitaka serikali kuaangalia kwa makini suala hili.mfano katika shairi la“Wafadhiliwa” “Bundi”,na“Fahali la dunia”.Mfano katika shairi la “Wafadhiliwa”anasema;
Ukombozi wa kiuchumi
Suala la jamii nkukomboka katika masuala ya uchumi ni jambo la msingi sana. Mwandishi ankisemea hili katika shairi la“Klabu
Maadili mema na maonyo
Maadili mema ndio msingi jkatika jamii. Mtu anapoenda kinyume na makubaliano ya jamii huyo huhesabiwa kuwa amepotoka kimaadili. Mwandishi amejadili mambo mbalimbali kuhimiza maadili mema na maonyo. Mfano ni;
  • Kupinga uovu:Katika shairi la “Kansa”, “Mtemea mate mbingu” anapinga suala la uovu nahimiza kutenda wema. Mfano katika shairi la“Mtemea mate mbingu”.
  • Kupinga mapenzi ya jinsia moja:Hili ni tatizo kubwa kwa jamii ya sasa. Kwani tamaduni ambazo si zetu zinavamia kwa kasi jamii ya leo. Mwandishi ameliona hili na kulisema katika jamii. Anaeleza matatizo ya kuwa na mapenzi ya jinsia moja katika shairi la“Jiwe si mchi.”
  • Tamaa sio nzuri:Mwandishi anakemea suala la tamaa. Anawashauri watu kuridhika na walivyojaliwa kwani tamaa mbele mauti nyuma. Anayasema haya katika shairi la “Si wewe?”
  • Umuhimu wa kujibidisha katika kazi:Ili upate mafanikio si budi kujibidisha tena kwa moyo wote. Mwandishi anasema kuwa vitu vizuri havipatikani bure tu. Bali mtu anapaswa kushughulika haswa. Mfano katika shairi la“Mcheza hawi kiwete”anafananisha bidii katika kazi na uchezaji wa ngoma.
  • Umuhimu wa kusoma na kuitumia vizuri elimu:Mwandishi pia anaona kuna umuhimu wa wanajamii kuwa na elimu kwani elimu ndio dira ya maisha. Si hivo tu anawaasa wanajamii kuitumia vizuri elimu pindi wanapoipata. Watoemchango chaya katika maendelo na maadili ya jamii badala ya kuchochea mmomonyoko wa maadili na kukwamisha uchumi. Amebainisha haya katika shairi la “Wasomi”;
  • FALSAFA: Mwandishi wa kitabu hiki anaamini kuwa matatizo katika jamii yanasababishwana watu wachache wanaonyonya watu wengine mfano katika masuala ya uchumi. Tabaka la wasakatonge linaendelea kukandamizwa na kuwa chini zaidi kwa sababu ya wachache tu. Anaamini ili jamii iweze kuwa na haki na usawa upo ulazima wa kufuta matabaka na kuboresha vipato vya watu wa chini. Aidha anaamini pia jamii ili iwe na amaendeleo na amani watu wanapaswa kuenenda katika maadili yaliyo mema.
  • MTAZAMO: Mtazamo wa mwandishi katika diwani hii ni wa kiyakinifu. Kwa sababu matatizo kama vile, hali ngumu ya kimaisha na kuwepo tabaka la walalahoi ni mifumo mibovu ya kiuchumi ikienda sambamba na matumizi mabaya ya pesa za umma, uzembe katika kazi, unyonyaji na unyanyasaji. Anatoa suluhisho linalowezekana katika jamii kwa kukemea yote yale yanayoenda kinyume na maadili sambamba na kuwawajibisha viongozi wasiotimiza wajibu wao. Anaona wanyonge wanaweza kukomboka kwa kuwa na ushirikiano nakusimamia ukweli popote pale.
  • MSIMAMO: Msimamo wa S. Khatib ni wa kimapinduzi. Analenga kupindua maovu, kupindua viongozi wasio waadilifu, anapindua mambo ambyo ni kinyume na maadili ya jamii zetu lakini pia anapinga suala la utabaka kataika jamii. Mambo hayo yanatufanya tuone kuwa kweli mwandishi analenga kuibadilisha jamii. Hajayafumbii macho maovu na dhuluma zinazoendelea katika jamii bali ameyaweka bayana ili watu wayafahamu na kujirekebisha.
UJUMBE
  • Kufanya kazi kwa bidii ndio msingi wa maendeleo.
  • Suala la utabaka katika jamii si zuri, hivyo si budi kulipiga vita.
  • Unyonyaji, ukandamizwaji na unynyasaji haufai kwani unadidimiza walio chini na kuwatweza wachache.Elimu ni ufunguo wa maisha.
  • Wasomi wanapaswa kutumia vizuri elimu walizopata.Haki na amani ni vitu muhimu hivyo si budi kuvidumisha.
  • Viongozi wasiowajibika wanapaswa kuachia madaraka na sio kung’ang’ania.
  • Mwanamke anatakiwa kukombolewa kutoka katika mila na desturi potofu.
  • Mataifa ya Afrika ili yaendelee yanapaswa kupiga vita ukabila.
  • Wanajamii wanapaswa kuwa waaminifu katika mapenzi na kuwa na mapenziya dhati.
  • Usaliti ni pigo katika mapenzi.
Maudhui katika Ushairi wa Malenga Wapya
Hakiki Maudhui katika Ushairi wa Malenga Wapya
DHAMIRA
Suala la uongozi bora na uwajibikaji
Suala la uongozi limejadiliwa katika pande zote mbili za uongozi mzuri na uongozi mbaya. Waandishi wameonesha yote haya wakiwa na lengo la kuikomboa jamii. Wamesisitiza kuhusu uongozi bora mfano katika shairi la “Payuka” anawaasa viongozi kuwa watekelezaji wa yale wanayoyaahidi na sio kuwa wapayukaji tu. Mfano ubeti wa pili anasema
Anakemea mapenzi yasiyo ya kweli ya usaliti. Mfano katika shairi la“Sili nikashiba” ”Si wewe?Mfano katika shairi la“Sili nikashiba”anasema juu ya usaliti;
Pia katika shairi la “Puuzo” anawakanya viongozi wasiowajibika kutekeleza majukumu yao na kuacha uzembe. Anawaasa kujituma na kufanya kazi kwa bidii kwani ni wajibu wao. Anasema katika ubeti wa kwanza
Ukombozi wa kiuchumi
Mwandishi anaona kuwa ili jamii ikomboke kiuchumi yapo mambo ya msingi kutekelezwa. Miongoni mwa mambo hayo ni kufanya kazi kwa bidii na kuacha uvivu. Mfano katika shairi la “Charuka” tunaambiwa kuwa.
Pia anakazia suala la kilimo kama ndio msingi wa kujikomboa kichumi katika shairi la “Adui” na katika shairi la “Mkulima”anaonesha umuhimu wa kumthamini mkulima na kilimo. Vikiwa kama vigezo vya maendeleo nchini mwetu. Mfano katika shairi la “Adui” anasema;
Pia katika shairi la“Tuyazingatie haya”mwandishi anatajamambo ambayo anaamini kuwa yakizingatiwa yataweka uchumi kuwa imara kama vile, kuchapa kazi, kukomesha ubaguzi kutopora mali za serkali, kushirikiana, kukosoana na kuepuka tamaa. Mfano ubeti wa pili anasema;
Ukombozi wa mwanamke
Mwandishi kwa kutambua nafasi muhimu ya mwanamke katika jamii, hakusita kuikumbusha jamii juu ya kuwaheshimu, kuwathamini, kuwapa uhuru na kupinga tamaduni zote zinazomkandamiza mwanamke. Anaamini kuwa kumkandamiza mwanamke ni kuikandamiza jamii. Anayazungumzia haya katika shairi la “Kifungo”, “Hina inapapatuka”, “Raha”.Mfano katika shairi la“kifungo”ubeti wa saba anasema:
Suala la maadili mema na maonyo
  • Umuhimu Wa kuwa na kauli nzuri.Mwandishi katika shairi la “Ulimi” anawaasa watu kuwa ulimi mzuri kwa maana ya kuongea vizuri na watu kwa adabu, na heshima. Anaona kuwa ulimi ni kiungo kidogo lakini kinaweza kusababisha matatizo au mambo mazuri. Anauasa ulimi akisema;
  • Umuhimu wa kutenda wema kwa binadamu wenzetu:Mwandishi anaona kuwa wanajamii wanapaswa kutenda wema kwa wanajamii wenzao kwani matokeo ya wema ni mafanikio na shukrani. Anasema katika shairi la“Hisani hulipwa”
  • Umuhimu wa kuwa na subira katika maisha:Mwandishi anawaasa wanajamii kutokurupukia maisha hasa vijana. Katika shairi la “Siharakie maisha”Anaona upo umuhimu wa kufanya mambo kwa wakati na kuacha tamaa kwani kila jambo na wakati wake. Anawaasa wanafunzi kushikilia masomo na kutolimbukia mambo ambayo si wakati wake. Anasema;
  • Umuhimu wa kuishi vyema duniani:Katika shairi la “Ulimwengu”na“Maisha ni kama njia”mwandishi anaiambia jamii kuishi vizuri katika dunia kwani dunia ni mapito tu. Mfano katika shairi la“Maisha ni kama njia”anasema;
  • Uaminifu katika ndoa:Suala ndoa kwa jinsi anavyosema mwandishi uaminifu ndio jambo la msingi kwani huleta upendo na amani kwa familia. Anawashauri wanaume kujali familia zao na kuwa na mahusiano mengine nje ya ndoa. Katika shairi la“Kwanini”anasema;
  • Matumizi mazuri ya pesa:Mwandishi anaona upo umuhimu wa kutofuja pesa. Anashauri watu kuwa na utamaduni wa kuweka akiba. Anaona kuwa ufujaji pesa ni dhambi na si haki. Katika shairi la“Israfu”
  • Kuzingatia dini na kumuabudu Mungu:Mwandishi anawaasa wanadamu kutii maadili ya dini zao. Kwani misingi ya dini huelekeza watu katika mema. Anasema haya katika shairi la“Maisha ni kama njia”.Ubeti wa tano anasema;
  • Suala la Mapenzi:Katika shairi la “Ua” na katika shairi la “Nipate wapi mwingine”waandishi wanaona kuwa mapenzi ya dhati na ya kweli ni jambo jema. Anawataka watu kuthamini na kuwaheshimu wapenzi wao na binadamu wengine. Mfano katika shairi la“Ua”anasema;
  • Pia katika shairi la“Nipate wapi mwingine” mwandishi anazungumzia jinsi ilivyo kazi kupata mpenzi wa kweli. Dunia sasa imebadilika watu hupenda vitu vingine badala ya kuwa na mapenzi ya kweli yanayojali utu wa mtu. Mwandishi anayaita kuwa hayo ni mapenzi ya ulaghai. Mashairi ya“Utanikumbuka”linaasa juu ya usaliti katika mapenzi kuwa haufai. Shairi la “Kuunge” na“kitendawili”yanakazia zaidi juu ya kuwa na msimamo katika mapenzi.Anafananisha watu wasio na mapenzi ya kweli na Njiwa anayerukaruka asiyetulia. Mwandishi anasema;
  • Umuhimu wa wosia:Suala la kutoa wosia kwa mwanadamu ni jambo la muhimu sana pindi anapokufa. Suala hili huepusha migogoro na malumbano kwa wanafamilia wanaobaki. Katika shairi la “Niniwanangu” anasema:
  • Suala la ukombozi wa kifikra:Mwandishi anaitaka jamii kukomboka kifikra. Mambo haya anayazungumzia katika shairi la “Usiwebendera”. Suala la kuwa na msimamo binafsi na thabiti katika maamuzi ya mambo ni jambo la msingi katika maisha ya kila siku. Anaona kuna athari ya kuendeshwa au kuamuliwa mambo kama bendera inavofuata upepo.
  • Utetezi wa haki.Mashairi ya“Mpaka lini”, “Samaki mtungoni” “Sokomoko”yanazungumzia juu ya ukosefu wa haki. Mahali popote hapawezi kuwa na amani bila kuwepo haki. Hivyo mwandishi anaeleza;
  • Katika shairi la“Samaki mtungoni”mwandishi anaona kuwa kwa sababu ya ukosefu wa hik watu hudhulumiwa na kuteswa anafananisha wadhulumu haki na wavuvi anasema;
  • Utabaka na unyonyaji na unyanyaswaji:Mambo ya matabaka ndiyo yanayochangia kunyanyaswa, kunyonywa na kukandamizwa. Matabaka ambayo waandishi wanayazungumiza ni matabaka ya kiuchumi, kijamii na kisisasa. Katika shairi la“Samaki mtungoni”samaki anachorwa kama mtu mnyonge na mvuvi akiwa ni mwenye mabavu. Anaonesha jinsi watu wasivokuwa na uhuru bali kundamizwa na kuteswa. Hili limewekwa wazi ili kupiga vita mambo hayo katika jami. Anasema;
  • Vilevile katika shairi la“Punda” mwandishi anaelezea jinsi ambavyo watu wa hali ya chini wanavyoendelea kuonewa na kuteswa kama Punda. Anaishauri jamii kukemea suala hili na kusaidiana kuwainua wanyonge na sio kuendelea kuwanyonya.
FALSAFA
Falsafa ya waandishi wa mashairi ya “Malenga wapya” ni kuwa jamii inaweza kubadilika kiuchumi na kupata maendeleo kama itafanya kazi kwa bidii bila kuzembea, wanaamini kupingwa kwa utabaka na unyonyaji ni suluhu ya amani na maendeleo. Wanaamini pia ukiishi vizuri duniani utafanikiwa, wanasisitiza kutenda wema. Haki usawa na ushirikiano ni chachu ya maendeleo.
MTAZAMO
Mtazamo wa waandishi ni wa kiyakinifu kwani mambo wanayoyaeleza kama vile namna ya kutatua matatizo katika jamii. Mambo wanayoyapendekeza yanawezekana kutimizika mfano uwepo wa haki, kupinga utabaka, unyonyaji, kufanya kazi vizuri kuweka akiba na matumizi mazuri ya pesa na mambo mengine mengi.
MSIMAMO
Msimamo wa kimpinduzini msimamo wa waandishi wa diwani hii. Mambo wanayoyaeleza yanalenga kuleta mapinduzi katika jamii mfano kupiga vitu adui uvivu, kupinga dhuluma, kupinga maovu yote. Hiyo ni ishara kuwa wanalenga kuibadilisha jamii. Wanatoa pia changamoto na suluhu ya matatizo katika utekelezaji wa mambo mbalimbali ya kimaendeleo katika jamii kama vilekufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maadili.
UJUMBE
  • Kufanya kazi kwa bidii ni chachu ya mendeleo.
  • Uaminifu katika ndoa, mapenzi ya kweli ni jambo lamsingi.
  • Matumizi mazuri ya pesa husaidia kuwa na akiba nzuri na kupunguza umaskini usio na tija.
  • Kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi, si budi kukithamini.
  • Kauli nzuri huepusha migogoro na chuki.
  • Kumkomboa mwanamke ni kuikomboa jamii, hivo si budi kupinga tamaduni zinazomkandamiza.
  • Tunaaswa kupinga utabaka.
  • Kutetea haki na kupuuza unyonyaji ili kuleta usawa katika maisha.Viongozi walaghai na wasaliti hawafai kwa maendeleo hivyo tunaaswa kuwa makini kuchagua vingozi bora na kuwawajibisha wasiofaa.
Maudhui katika Diwani ya Chekacheka
Hakiki maudhui katika Diwani ya Chekacheka
DHAMIRA
Mwandishi amejadili dhamira mbalimbalizinazosawiri jamii yetu ya leo. Dhamira hizo ni pamoja na hizi zifuatazo:
Uongozi bora
Suala la uongozi bora limejadiliwa na mwandishi wa diwani hii ikiwa kama jambo la msingi sana katika maendeleo ya Nchi. Mashairi ya“Mwinyi umewasha moto”na“indira”yanaelezea vyema juu ya viongozi ambao ni mfano wa kuigwa katika jamii.Mfano katika shairi la “Indira” anasema juu ya kiongozi Indira ambaye aliongoza vyema katika uongozi wake. Anawataka viongozi wa sasa kuiga mfano huo, anasema:
Pia hakuacha kugusia suala la viongozi wasiotimiza majukumu yao. Haya anayasema katika shairi la“Muwapi nawauliza”, “Utaliwa kama pumba” “Gunia la mikutano”mfano katika shairi la“Muwapi nawauliza”anawaamsha viongozi ili watimize majukumu yao:
Kupinga unyonyaji
Mwandishi anakemea masuala ya unyonyaji wa tabaka la chini. Shairi la“Kuna nini”, “Chatu mmeza matonge” “Chunguzeni walo mbele”, “Kazi yetu harakati”.Mfano katika shairi la“Chatu mmeza matonge”mwandishi anazungumzia jinsi wanyonge wanavyoteseka katika hali ngumu ya maisha. Amelionesha hili ili jamii na serikali viweze kuwasaidia na kuwainua watu hawa.
Kupinga udikteta na ukosefu wa demokrasia
Suala la ukosefu wa demokrasia na haki ya kweli ni mambo ambayo yanafanya wanajamii kushindwa kujadili na kuweka wazi masuala nyeti ya kijamii pale inapobidi. Mwandishi kwa kuliona hili kama jambo la muhimu amelizungumzia katika mashairi ya“Raia si mali kitu”, “Dhahabu ya fahari”.
Kupinga ukoloni mamboleao
Mashairi ya“Lazima mniamini” na “Utumwa huru”ni mashairi ambayo yanaelezea juu ya ukoloni mamboleo. Mwandishi anaonesha kuwa nchi nyingi za kiafrika zimepata uhuru lakini ni uhuru wa maneno tu na si vitendo. Nchi hizi bado zinaamuliwa na kupangiwa mambo. Mwandishi anasema katika shairi la“Utumwa huru”anasema;
Ukombozi wa kiuchumi
Suala la ukombozi wa kiuchumi ni jambo ambalo huendana na maisha ya kila siku ya mwanadamu. Uchumi bora ndio huleta maendeleo zaidi katika jamii. Mwandishi analisema hili katika shairi la“Muwapi nawauliza”, “Kweli ilojaa udi”mfanokatika shairi la“Kweli ilojaa udi” anasemea juu ya uhaba wa bidhaa miaka ya themaninikwani uchumi ulizorota.
Kupiga vita matabaka
Shairila“Chunguzeni walo mbele”, “Kazi yetu harakati”na“Gunia la mikutano”. Mfano katika shairi la “Gunia la mikutano”
Hapa mwandishi anajaribu kutuonesha utofauti kati ya wenye navyo au watawala na wasio nacho. Maisha yao ni tofauti kabisa. Wakati wengine wakifanya mambo ya anasa na starehe zisizo na tija wengine waumia kwa njaa na dhiki. Hivyo si budi jamii kwa pamoja kupinga suala hili kwa kuziba mifumo yote ya kitabaka.
Umuhimu wa Washairi kutunga mashairi bora
Bila kugusia masuala ya fani katika mashairi, Mashairi bora ni yale ambayo yanasema ukweli juu ya mambo jinsi ulivyo bila kificho. Ni mashairi yanayoangazia maisha ya kila mmoja katika jamii, hukosoa bila upendeleo wala hayasiti kusema na kutetea haki mara inapobidi. Shairi la“Tuambae ukasuku”ni shairi ambalo linawataka washairi kutunga mashairi wakiangalia matatizo ya jamii.
Suala la maadili mema na maonyo
  • Kuepuka tamaa: Katika shairi la “Moyo”mwandishi anauasa moyo kutokuwa na tamaa kwani unaweza kudhurika sababu ya tamaa.
  • Kuwa na uadilifu katika dini: Shairi la“Chanzo cha huo uozo”linaeleza juu ya aupotofu wa maadili kwa viongozi wa dini anawaasa kuzingatia misisngi ya imani zao na kuwa mfano katika jamii.
  • Kuthamini utu: Utu kuthaminiwa ni sehemu ya mambo muhimu sana kwa mwanadamu. Katika shairi la“Utu umekuwa kima”mwandishi naonesha jinsi ambavyo watu siku hizi hawatahmini utu na kuizingatia mambo mengine. Anaikumbusha jamii kuwa utu wa mtu ni muhimu sana kuthaminiwa.
  • Umuhimu wa kuwa na msimamo katika maisha: Shairi la“Chura umegundulika”linafananisha watu wasio na msimamo katika maisha na chura. Anawaasa watu kutokuwa kama chura kwa tabia yake ya kutoeleweka kama anaishi majini au nchi kavu.
  • Umuhimu wa kuwajali wazazi: Mwandishi kwa kutambua umuhimu mkkubwa wa wazazi, anaielimisha jamii kupitia shairi lake la“Ni wapi ushauri?”kuwa vijana wanapaswa kuwatunza na kuwasaidia wazazi wao pindi wanapozeeka.
  • Umuhimu wa kujiheshimu katika mapenzi: Shairi la “Penzi lisilo heshima”linakemea juu ya tabia mbaya ya watu wasiojiheshimu katika ndoa au mapenzi. Anakemea mapenzi ya pesa. Anashauri jamii kupendana kuthamini utu wa mtu na sio pesa.
  • Umuhimu wa kuwa na busara na hekima: Hekima ni jambo jema kwa mwanadamu. Mwandishi anaona kuwa kwa ktutumia hekima kuamua mambo ni vyema kuliko kukurupuka. Anayasema haya katika shairi la“Moyo”.
  • Kuepuka shari: Mwandishi katika shairi la“Moyo”anaiasa jamii kuepuka shari na ugomvi wala kutoichochea. Anawataka watu kuwa chanzo cha amani na mapatano.
  • FALSAFA: Mwandishi anaamini kuwa masuala ya haki na uwajibikaji ni suluhu ya maendeleo.
  • MTAZAMO: Mtazamo wa mwandishi ni wa kiyakinifu kwani kero na matatizo anayoyazungumzia katika jamii yapo kweli. Kama vile matabaka, uhujumu uchumi na hali ngumu ya maisha. Anatoa suluhu muafaka kwa matatizo hayo.
  • MSIMAMO: Msimamo ni wa kimapinduzi kwani mwandishi analenga katika kuibadilisha jamii. Anapinga masuala ya unyonyaji na ukandamizwaji. Pia anaona ipo haja ya viongozi na watawala kujituma kadiri inavowapasa. Mwandishi pia aligeuzia jicho masuala ya kimaadili kwani hakusita kuwakanya wavivu, waliopotoka katika uadilifu nk.
UJUMBE
  • Uadilifu katika dini na imani ni muhimu kuzingatiwa.
  • Haki na usawa ni suluhu ya migogoro ya kisiasa.
  • Wanajamii wanapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kukomboka kiuchumi.
  • Busara ba hekima ni mambo ya kuzingatia katika uamuzi wa jambo fulani.
  • Utu wa mtu unapaswa kuthaminiwa.
  • Washairi wanapaswa kuandika mashairi yanayoipasa jamii badala ya kuwa na ukasuku.
  • Mapenzi ya heshima na dhati ndio mapenzi ya kweli.
  • Matabaka katika jamii ni kikwazo na kichocheo cha unyonyaji hivyo si budi kupiga vita

Strategies for answering exam and test questions

Click on the accordions below to see more information about how best to tackle the following question types in your exam.

Multi-choice questions

Things to remember about multi-choice questions

  • Read through the options and try to eliminate the ones that aren’t right. Multi-choice questions usually have one option that is obviously wrong, and three or four others that are similar.  It is important to look carefully at how they are worded in order to select the correct  answer.
  • Don’t struggle over a question. Do all of the easy questions first and come back to harder ones later to maximise efficient use of test/exam time.
  • Answer all the questions. Even if you are not sure, your educated guess may well be correct. It is better to have a go at answering a question than potentially miss out on a mark.
  • When you check back through your paper and think an answer is wrong - change the answer. Research indicates that you will probably be correct in doing so.

Short answer questions

Short answer questions range from a sentence or two through to a paragraph in length.

  • Keep to the point. Short answers are usually two-three sentences.
  • Main ideas. Your answers should incorporate the key points, words, ideas and phrases the marker will be looking for.
  • Leave one or two lines after each answer. This is so you can add important points later on.
  • Try to answer all the questions.  If you don’t know the complete answer, put down what you do know, as this is likely to get you some marks.

Exam essay questions

The advice here is in four parts: Time allocation | Task analysis | Planning | Presentation

Time allocation
  • Use the reading time at the start of the exam to choose which essay questions you will answer.
  • Check how much time you might have to answer each essay question, and stick to it. You can come back and add more to your answer in your revision time at the end of the exam session.
  • If you haven’t finished your answer, jot down the rest in note form. This will show the marker what you know, and you might get some marks for it.
Task analysis
  • Read the question carefully.
  • Underline or highlight the content words. What is the topic?
  • Pick out the instruction words in the question, e.g. identify, describe, compare and contrast, evaluate. What are you being asked to do with the topic?
Planning
  • Take some time to think and plan your answer. For example: use the reading time to select which essay questions you will answer. Then use the start of the writing time (5-20mins) to make notes of all the points you remember that are relevant to the essay.
    General guide for timing: for 30 minutes of writing, allow 5-7 minutes for planning.
  • Plan out the structure by organising your points into a logical order:e.g. by numbering them according to intended sequence.
  • General writing rule for exam essays - one paragraph = one point. Follow standard essay-writing procedure, e.g. start with a topic sentence that contains your key point, and then support this with examples, explanations, and evidence.
Presentation
  • Make sure your handwriting is legible. Markers should not have to decipher your handwriting. If your handwriting is illegible, it could compromise your marks.
  • Make sure that you can express ideas effectively in terms of sentence structure and word use.  Incoherent sentences and incorrect terminology will likely result in the marker not being able to understand your answer properly.
  • Don’t worry too much about punctuation, grammar and spelling. Getting your ideas down is more important than ‘perfect’ writing (and markers usually take this into account given that students are writing under pressure in an exam situation). However, you do need a basic level of competency in these areas: an answer that lacks any punctuation and is full of spelling mistakes will probably be incoherent for the marker.
  • Don't waffle. Get straight to the point in terms of your answer so that you don’t waste time and word space on unessential or irrelevant detail. Planning your essay beforehand is key to avoiding waffle.

Problem solving questions

Usually these types of questions target formulae, steps in a process, or rules.

  • Make sure you write down relevant formulas, equations, and rules. Important: For numerical problems involving computation, make sure you include the appropriate mathematical units in your final answer (e.g. ml, m/sec).
  • Clearly show the steps you have taken in working out the answers.
  • If necessary, write notes to explain your answers.
  • Do the easier answers first, and return to the difficult ones later.

logoblog

No comments:

Post a Comment