EDUCATION

Form Five Selection: Jinsi ya Kuangalia Waliochaguliwa Kidato cha Tano na Vyuo vya Kati

MWL …

Baada ya matokeo ya kidato cha nne (CSEE), Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI hupanga wanafunzi wenye sifa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya kati (vyuo vya ufundi na vya kati vya Serikali). Mwongozo huu unaeleza jinsi ya kuangalia kama umechaguliwa, combination au kozi uliyopangiwa, na jinsi ya kupata joining instructions.

Jinsi uchaguzi unavyofanyika

  • Wakati wa kidato cha nne, wanafunzi hujaza machaguo ya combination, shule na vyuo (selform) kupitia shule zao.
  • Baada ya matokeo ya CSEE, TAMISEMI hupanga wanafunzi kulingana na ufaulu, machaguo yao na nafasi zilizopo.
  • Kabla ya kujaza machaguo, soma mwongozo wa kuchagua combination ili uchague combination inayoendana na ndoto yako ya chuo na kazi.

Jinsi ya kuangalia waliochaguliwa kidato cha tano na vyuo vya kati

  1. Fungua mfumo rasmi wa TAMISEMI: selform.tamisemi.go.tz, kisha bofya Selection Results.
  2. Chagua toleo la uchaguzi (Choose Selection Version), mf. "First Selection" ya mwaka husika.
  3. Tumia kisanduku cha Search kutafuta kwa jina au kwa shule/kituo ulichofanyia mtihani.
  4. Jedwali litaonyesha: kituo cha mtihani, jina, jinsi, halmashauri ya nyumbani, shule/chuo ulichopangiwa (Selection) na kiungo cha Joining Instructions.

Joining Instructions

  • Bofya kiungo cha joining instructions kwenye safu ya jina lako ili kupakua fomu ya shule au chuo ulichopangiwa (PDF).
  • Soma kwa makini: tarehe ya kuripoti, mahitaji, michango na fomu ya uchunguzi wa afya.
  • Ukishindwa kuifungua, wasiliana na shule/chuo husika moja kwa moja au ofisi ya elimu ya mkoa.

Hujachaguliwa au unataka kubadilisha?

  • Subiri awamu ya pili ya uchaguzi (Second Selection), ambayo hutolewa mara nyingi baada ya ile ya kwanza.
  • Maombi ya kubadilisha shule au combination hufanyika kwa utaratibu unaotangazwa na TAMISEMI kwa mwaka husika. Fuata tangazo rasmi pekee.
  • Njia mbadala: vyuo vya kati vinavyodahili kupitia NACTVET, shule binafsi, au kurudia mtihani kama mtahiniwa wa kujitegemea.

Jiandae kwa kidato cha tano mapema

Soma pia: Jinsi ya kuangalia matokeo ya NECTA | Form One Selection | Past papers za NECTA na mock

📚 Browse More Resources

Share This Post

Related Posts

Comments

Post a Comment